Wasioujua ukweli kuhusu Corona Tanzania

Ashasembeko

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
225
910
Leo baada ya kuapisha viongozi mbalimbali Ikulu ya Chamwino Dodoma, Dr. Magufuli alitamka kuwa Corona imeshapotea na kuongeza kuwa "tuko salama". Kuna ukweli gani juu ya madai haya?

Swali langu ni je tunajuaje tuko salama wakati hatujui hali halisi na serikali haijatoa takwimu rasmi za ugonjwa huu toka tarehe 29/04/2020? Ukweli ni kwamba hamna anaejua hali ya Corona nchini, ikiwemo serikali yenyewe kwasababu wameacha kufanya testing toka mwezi wa tano.

Vyanzo vyangu vya kuaminika vimeniambia kuwa baada ya wagonjwa wenye dalili kutiririka mahospitalini kutaka kupimwa, serikali ilikataza madaktari kupima na kupokea wagonjwa wa corona (Madaktari wa Hospitali za Temeke na Amana wanaelewa hili vizuri). Na waliambiwa kuwa kama kuna wagonjwa watafariki kwa matatizo ya kupumua wasiandike hivo kwenye vyeti.

Mimi ninaamini kuwa Corona imepungua sana, ni kwa sababu ya watu kupata immunity na pia kutumia tiba asili ila ninaamini pia huu ugonjwa bado upo japo si sana kama ilivyokuwa awali.

Katika wiki mbili zilizopita Mwalimu wangu Professor Mbwete alifariki kwa matatizo ya kupumua na aliugua ghafla. Wiki iliyopita, Jaji Bongole naye alifariki kwa matatizo ya kupumua. Huyu Jaji, vyanzo ndani ya familia vinasema alikua na dalili za corona kwa takribani wiki na alitambua hilo, sema alikua muumini sana wa kujifukuzia, na aliwaambia familia yake wafanye hivo pia.

1595256782354.png
1595256875463.png

Kama nilivosema mwanzoni ni vigumu kujua hali ya Corona nchini ikoje kwa sababu hamna takwimu na serikali yenyewe haijui pia maana hawafanyi testing kabisa. Balozi na mashirika ya kimataifa hapa nchini yote bado yanafanyia kazi nyumbani kwa kushauriwa na WHO kuwa hali haitabiriki. Serikali haitoi ushirikiano wowote ule kwa mashirika haya na imeamua kufocus kwenye campaign

Nawaombeni tuwe makini na tuendelee kuchukua tahadhari. Tuwe makini na kauli za wanasiasa, Corona bado ipo, jilinde wewe jirani yako na familia yako
 
Safi, ila kumbuka Mzee wetu likimpata ana access na the best health services, wewe? Sijui
 
5% ya watu million 60 ni ngapi?? Mi najua ipo sana tu, ila Dr. John kasema leo imeisha.
 
Hawafanyi testing!! Believe me, I know sector person. Na kama wanafanya mbona hizo takwimu hawatoi
 
Hawafanyi testing!! Believe me, I know sector person. Na kama wanafanya mbona hizo takwimu hawatoi
Mbona unataka takwimu za corona tu kwani ndio ugonjwa pekee tulionao? Kwanini usiombe kuletewa takwimu za wanaoumwa Malaria!?
 
Ashasembeko,
Kuna sehemu umesema sawa lakini ulikokosea ni pale ulipopost tangazo la tanzia.kuugua gafla na kufariki haimanishi umekufa kwa korona.
 
Back
Top Bottom