'UDINI WA CCM NA SERIKALI YA KIKWETE' SASA HADHARANI:
VYOTE VYA KIKRISTO NA MIJUMBA TAKATIFU YA IBADA VYAGEUKA MAJIVU KWA KASI YA AJABU BILA MTU KUTIWA HATIANI HADI KESHO
Ni simanzi tena sikitiko kubwa kwa jamii nzima ya Kikristo nchini kuona jinsi gani makanisa yetu moja baada ya nyingine, na mali za wakristo zisizokadirika thamani, yanavyodondoka chini katikati ya msitu mkubwa wa moto lakini bila kuona utetezi wowote wa dhati toka seriklini.
Mficha maradhi siku zote mauti humuumbwa mbele ya kandamnasi; UDINI wa serikali yetu tumeupigia sana kelele sasa mwishowe mambo ndio haya Tanzania Visiwani huku Wabara tukikimbizwa kama mmbwa mwizi shauri ya imani zetu kuwahi boti kurudi makwetu - na yote haya yanaendelea bila serikali yetu ya muungano kutenganisha UHALIFU WA UDINI mbali kabisa na madai halali ya mtu yeyote kusikilizwa maoni yake kuhusu Muungano wetu.
Naam, nasemaa hivi hii hapa NDIO SURA MOJAWAPO YA UDINI SERIKALI YA KIKWETE wengine tuliowahi kuupigia kelele kwa sana na badala yake baadhi ya viongozi wetu wa imani nao walisikika wakidai kwa sauti za unyonge gizani kwamba eti nchini mwetu Tanzania hakuna UDINI
Suala la mtu yeyote au kikundi kuwa na dukuduku juu ya Muungano wetu wa Tanzania ni swala ambalo ni haki yao ya msingi kutafuta kusikilizwa kwenye vikao halali kitaifa pindi wanapojitokeza bila ya kuumiza haki za wengine wasiokalia haki yao hiyo.
Ni vigumu tena sana kwa mtu yeyote kuridhisha jukwaa hili kwamba siku hizi njia sahihi kwa Mtanzania yeyote wa Bara au Visiwani anapotafuta kusikilizwa kwa DUKUDUKU JUU YA MUUNGANO basi njia ya mkato ni kuchoma Kanisa na au chochote kilicho cha Mkristo nchi au kuchoma Msikiti na au chochote kilicho cha Muislamu nchini.
Naam, nasema hivi mwelekeo kama huu wa KUTENDA DHAMBI YA UDINI na kuipa jina DUKUDUKU YA MUUNGANO kamwe haikubaliki duniani hata mbinguni naapa hapa!!!
Katika haya yote yanayoendelea kule Tanzania Visiwani, Serikali yetu ya Muungano yenye jukumu la Ulinzi na Usalama wa WaTanzania wote na maali zetu iwajibike haraka kwa (1) kutokomeza kabisa hii hulka ya UDINI kwa kisingizio cha DUKUDUKU ZA MUUNGA, (2) Serikali ya Muungano iombe radhi Wakristo hadharani kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake wa ulinzi na usalama vya kutosha kule Visiwani, (3) Serikali ya Muungano itoe fidia ya asilimia 100 kwa mali zote zilizochomwa moto Zanzibar kutokana na visingizio vya kiayawani hizi.
Kitendo cha Kiongozi wetu wa kiroho, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheik Shaaban bin Simba kutaka WAUMUNI WAKE WASIKILIZWE NDIPO AMANI IPATIKANE huku bila ya kujitokeza hadharani kukemea maovu yaliotendeka kwa jamii ya kikristo ambao kamwe hawahusiki na sheria ya Kikwete ya kukataza Muungano usijadiliwe kwenye Tume ya Katiba nchini, ni UNAFIKI wa hali ya juu kwa kiongozi wa hadhi hiyo katika jamii.
Hivi inakua vipi Ndugu Simba aone HAKI YA KUSIKILIZWA KWA WAISLAMU WAKE wanaochoma mali na NYUMBA ZA IBADA za wenzao na hapo hapo akose kuona HAKI YA USALAMA WA MALI NA NYUMBA ZA IBADA ZA WAKRISTO zilizoteketezwa huku polisi Zanzibar waakidaiwa kuwa ni sehemu muhimu wa zoezi hilo zima????
Ndio, ni haki ya wenzetu wa Tanzania Visiwani na hata Bara kusikilizwa kwa DUKUDUKU lolote lile lakini KAMWE WASITAFUTE KUSIKILIZWA HUKO kwa njia ya KUCHOMA NYUMBA ZETU ZA IBADA NA MALI ZA KANISA.
WaTanzania tujiulize kwamba laiti picha hii ya kinachoendelea Zanzibar hivi sasa kingegeuzwa upande wa pili eti kwamba huku Bara ndio Wakristo wanachoma Misikiti kibao na mali za ndugu zetu Waislamu na kuwafukuza ndugu zetu wa kule Visiwani wakaondoke mara moja, bado Askofu yeyote Mkuu angeendelea kueleweka pindi anapotumia maneno ya kichochezi kama hivi eti wanaokataa Muungano wasikilizwe???
Kwa kuwa haku kumbukumbu zozote katika historia zinazoonyesha ama Wakristo au Waislamu, popote pale duniani, kunufaika na laana hizi za kuchomeana Mijumba Takatifu za ibada, WaTanzania wapenda amani tunayo nia ya dhati, sababu na uwezo wa kuishinikiza serikali yetu ikomeshe mara moja mambo kama haya YASIRUDIE TENA KATIKA TAIFA LETU na kwamba taifa la Iran ikatazwe mara moja kutumia fedha zake kuchochea udini VIsiwani.
Hili tunaomba litekelezwe kwa haraka tena sana kabla MAMBO HAYAJACHUKUA SURA ISIOPENDEZA SANA katika ngazi ya taifa na kimataifa kuhusu hicho kinachofadhiliwa kwa nguvu nyingi sana pale Zanzibar.
Ni vema pia leo hii tukaumie fursa ya ugeni huo wa kiongozi wa juu sana wa Iran kuja nchini mwetu na tukamwambie kabisa usoni mwake kwamba kweli sisi ni sehemu ya mataifa yenye mahitaji sana kusaidiwa kifedha ila Ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo UBAGUZI WA KIDINI WaTanzania hatujayazoea hata siku moja hivyo watusamehe katika hilo.
Na kwa mtaji wa kile kilichotokea Zanzibar majuzi, na kauli zenye uhaba wa hekima na busara kutoka kwa Mhe Zitto Kabwe na sasa kwa Mufti Mkuu wa Tanzania huku Zanzibar ikiteketea kwa moto, WaTanzania kila mmoja tukatafakari haya yote kwa sala na mfungo ili Mwenyezi Mungu atujalie salama nchi ipate viongozi wenye busara zaidi kuendeleza mshikamano wetu kitaifa usioegemea ubaguzi wa aina yoyote ile.