Wasiomjua Dr. Slaa soma mada hii, kabla ya uanasiasa na baada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasiomjua Dr. Slaa soma mada hii, kabla ya uanasiasa na baada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 30, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160


  [​IMG]
  Dr. Slaa

  Dr. Slaa si mtu mwenye maneno mengi, ni mtulivu na mkimya kiasi chake, lakini akipanda jukwaani na kuanza kulishambulia huku na kule huwezi kuamini kinachotoka ubongoni mwake. Kimya kingi kina mshindo.

  Wengi hawamfahamu Dr. Slaa vilivyo, wengi wanamwona sasa baada ya kuingia bungeni na sasa katika majukwaa ya siasa, ukweli ni mtu mbunifu, mpenda maendeleo na mwenye kujitoa kwa ajili ya wengine bila kujibakiza. Ufahamu wangu wa huyu Dr. Slaa ni wa muda mrefu, lakini wengi wetu wanachukulia mambo ya juu juu tu bila kujua undani na utendaji uliotukuka wa mtu huyu.

  Machache kati ya mengi kuhusu Dr Slaa kabla ya kuwa mwanasiasa, kuwa Mwanasiasa na hatimaye kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ana mlolongo wa mambo mengi ambayo yanaonyesha ubunifu wa hali ya juu, na pia mwepesi kuwaelewa vijana na kuendana nao tofauti na watu wengine wa kizazi chake.

  Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM, baada ya kuombwa na Wanakaratu agombee ubunge kule baada ya kuchoshwa na mbunge aliyekuwepo wakati huo, CCM iliendelea na mizengwe ile ile kama iliyotokea juzi pale Dodoma kuwaengua watu wanaofaa kwa uongozi. Wanakaratu wakiamua hawataki longolongo, wakamsihi kwamba wameamua awe mbunge wao na wakamwomba achague chama kingine agombee kwani hawamtaki kabisa mbunge aliyepo. Kwa ridhaa ya wananchi akaamua kujitoa CCM na kujitosa kujiunga na Chadema ili agombee ubunge kuridhia matakwa ya wanakaratu.

  Kabla ya kuwa mwanasiasa
  kuna mengi ya maendeleo ambayo wengi tunayaona huku tusijua kama Dr. Slaa ndiye aliyebuni na kuyaendesha kama ifuatavyo.
  1. Dr. Slaa ndiye amekuwa wa kwanza Tanzania kuagiza big truck for load and unload makontena bandari ya Dar es Salaam wakati akiwa Katibu Mkuu TEC. Ilikuwa ni miaka ya 1980th, hakukuwa hata kampuni au watu binafsi waliothubutu kufanya hivyo. Truck hilo lilikuwa na crane za kupakia na kupakua bila taabu kokote linalokifkishwa container na kwa truck hilo. Baadaye makampuni yakabembeleza wauziwe gari ile, ndipo Barala La maaskofu likawauzia.
  2. Kwa mara ya kwanza baraza la Maaskofu Tanzania lilipoanza kuwa na matumizi ya computer ikiwepo ofisi yake Dr Slaa kama katibu Mkuu, na taasisi za upashanaji habari ambazo zilikuwa chini ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na:

  • Gazeti la kiongozi kuanza kutumia mfumo wa computer katika idara ya set up
  • TMP (Tanganyika Mission Press) Kipalapala idara ya uchapishaji (printing) wakitumia Apple computers.
  • TMP Book deparment Tabora mjini) idara ya maduka ya vitabu na usambazaji vitabu wakitumia Apple computers
  • TAPRI idara ya tungo za mawasiliano vitabu TEC iliyokuwa na ofisi zake Seiminari kuu Kipalapala Tabora.

  Idara hizo zilikuwa na matumizi ya computer na PageMaker & QuakExpress software ambazo kwa graphic designers ilikuwa kitu kigeni kisichozoeka bado Tanzania ukitilia maanani wakati huo tulikuwa na chuo kimoja tu cha ardhi kule Tabora kujifunzia Graphic Design kabla ya Ardhi Dar haijaanza kukamilika. Huo ni ubunifu wa Dr. Slaa kwa wakati huo wakati wengi Tanzania hawajafunguka kuhusu matumizi ya teknologia ya ulimwengu wa dot com.

  NB.
  Wakati huo chuo pekee cha mawasiliano (journalism) Tanzania kilikuwa ni Nyegezi-Mwanza pekee kilichokuwa kikiongozwa na AMECA (Balaza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati kimoja kikiwa Kitwe - Zambia, cha Nyegezi kiliendeshwa na TEC Dr. Slaa akiwa msimamizi mkuu kama Katibu Mkuu.​

  Dr. Slaa atakumbukwa sana kwa makubwa aliyofanya kujenga na kuikuza TEC

  1. Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tunayoona siku hizi ni matunda ya ubunifu wa Dr. Slaa alipokuwa Katibu Mkuu pale. Jengo la awali ni lile lililo upande wa mbele zinapotumika ofisi siku hizi ambapo yalikuwa madarasa ya shule ya sekondari ya Masisita Tanzania, ambayo baadaye ilihamishiwa Bigwa Morogoro kupisha kiwanja hicho kuwa makao ya Maaskofu Katoliki Tanzania, awali yalikuwa pale ofisi za St. Joseph, Dar es Salaam. TEC aliyoikuta DR. Slaa ilikuwa na jengo hilo la madarasa na jengo lilolokuwa la utawala wa shule. Dr. akabuni majengo ambayo tunayoana sasa, hata kama hayakukamilika yote waliofuata walikamilisha kazi alioyoianza.
  2. Kaone maendeleo na majengo katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja walifanya makubwa.
  3. Kaangalie jimboni kwake huduma za kijamii ambazo amezifanya, utachoka mwenyewe kiasi ambacho CCM imekimbiwa kabisa huko sababu utendaji wa Slaa huko na CCM ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.
  4. Dr. Slaa kwa tunaomfahamu ni mwanamapinduzi na mpenda maendeleo, na pengine mengi alikuwa anayafanya yakaonekana mapya mno kwani alikuwa anaona mbali kuliko hawa wakubwa wake, ila sipendi kuliongelea sana hilo.

  Chadema yaimarika baada ya Dr. Slaa kuwa mgombea urasi uchaguzi Mkuu uliopita.

  Siyo siri Chadema hakikuwa na nguvu tunayoona sasa hivi licha ya kuwa na sera nzuri, lakini leo tunaona nguvu ya Chadema inayoogopewa mno na CCM ni kutokana na Chadema katika dakika za majeruhi kuamua kumwangukia Dr. Slaa agombee urasi ambao Samweli Sitta aliingia mitini baada ya makubaliano nao. Tangu hapo Chadema imekuwa na nguvu ya ajabu.

  Je, vijana hao waliokuwemo ndani ya Chadema kabla ya Dr. Slaa kugombea Urais kwa nini hawakuipaisha juu Chadema kama sasa? Baada ya Dr. Slaa kuipaisha Chadema juu sasa tunakuja na kauli mbiu ya kubeza makubwa yaliyofanywa na hawa mnaowaita kizazi cha kabla ya uhuru. Hapana tuwe waungwana, pamoja na kila mmoja kuwa na haki za kugombea nafasi tusigeuze uhuru huo kuwabeza hawa ambao wametufikisha tulipo, na bado tunahitaji mchango wa ushauri, uongozi, hekima na busara zao. Uongozi bora ni kuchanganya mapya na ya kale kwani
  viatu vya zamani vyaijua njia.

  Ubunifu wa Chadema viongozi wakiwa mojawapo waliozaliwa kabla ya Uhuru Dr Slaa na Kamanda Mbowe:

  • Dr. Slaa ndiye mbunge ambaye baada ya kuingia bungeni alianza kuchangamcha kwa kuichambua serikali na kasoro zake kitu ambacho katika mabunge yaliyotangulia wabunge walikuwa ni rubber stamp ya serikali.
  • Chadema wakiwemo hao unaoona walizaliwa kabla ya uhuru wamebuni mapya katika shughuli na kampeni za uchaguzi Tanzania kuwa zenye mvuto kuanzia mkuktano wa ufunguzi wa kampeni uchaguzi Mkuu uliopita ulifanyika Kidongo Chekundu baada ya Dr. Slaa kushusha makumbora mazitomazito kuituhumu serikali, watendaji wa serikali na CCM, tuhuma ambazo CCM wanazidi kubabaika kuwanyoshea kidole wahusika kisha kuwakumbatia tena hivi karibuni kule Dodoma.
  • Mkutano wa Kidongo chekundu Dar es Salaam ndio ulioanza kutufungua macho na masikio Watanzania na kuanza kujifunza elimu ya uraia ambayo tulikuwa tunazibwa na CCM tusiijue.
  • Dr. Slaa ndiye aliyetufunza na kutufunua kwamba raia wanayo nguvu ya kuiadabisha serikali haki zao za msingi zinapokiukwa kwa kauli mbiu ya nguvu ya umma (peoples power).
  • Utumiaji wa chopper kufikia maeneo magumu kufikika kwa magari na kurahisisha kazi ya kampeni, CCM wakaiga.
  • Kuwa na magari yanayotumika kama majukwaa ya mikutano badala ya kupoteza gharama na muda kujenga majukwaa yatakayotumika kwa dakika chache.

  Ilani ya Uchaguzi Chadema ndiyo inayotumika na yenye uzito sasa hivi:


  • Fukuto la Katiba mpya linaloendelea sasa nchini ni uzao wa ilani ya Chadema na ilani ya Dr Slaa kwamba kinachofuata baada ya Uchaguzi mkuu ndani ya siku 10
  • Kikwete kufanya mabadiliko ya barala la mawaziri mara kadhaa ni kutokana na shinikizo la wabunge wa Chadema bungeni.
  • Serikali kubana matumizi ya ziada ili kuokoa pesa za walipa kodi

  Kuna mengi tu wachangiaji wengine watachangia, ni dhana potovu kuwa na fikra za aina hiyo na kuwabeza wabunifu wa mengi, waliongoza nchi hii, wenye kuturithisha mengi kwa uzoefu na busara zao na walioongoza nchi hii hadi kuwa na utulivu wa aina yake. Leo vijana mnaowasema yanayojilia ni amani kusambaratika na mauaji ambayo ilikuwa hadithi za kusimuliwa kutoka nchi nyingine, leo serikali ya CCM inayoongozwa na Rais kijana kuliko Rais mwingine aliyemtangulia imetwishwa na aibu kubwa ya kitaifa na kimataifa ya mauaji ya raia wasio na hatia.

  Kuna nchi ambazo ni kielelezo cha vijana ambao mimi ningewaita watoto kukabidhiwa madaraka ya kuongozia nchi na kusababisha maafa makubwa kwa nchi husika kama Liberia, Ujerumani chini ya Hittler, na kinachoendela huko Zaire ya sintofahamu.

  Vijana achaneni na uroho wa madaraka, vema kubaki watumishi na watendaji wazuri serikalini na vyamani kujifunza mbinu za uongozi na kupata uzoefu katika kuongoza nchi.

  Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika kuongoza nchi.

  • Vijana wana papara,
  • wanataka njia ya mkato,
  • pagumu wanataka kulazimisha bila busara wala kutumia akili
  • Vijana wanalipuka kama moto wa gas
  • mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika.


   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Thanks for a very good analysis.Kati ya mashujaa na mkombozi wa Taifa aliyebaki.Mungu ampe maisha marefu atupeleke salama nchi ya Ahadi.
   
 3. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thanks a lot for the updated details of Dr. Slaa
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Poor analysis
  Fool of bias.
  Wewe na molemo mkajipange upya!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Thanks, lakini hapa tunajadili hoja, ungetulitea hoja zako kupambanisha na zetu tungekuona una fanya analysis iliyotukuka, lakini kuproromosha mtusi bila hoja za kukabiliana na hoja zetu kuna dalili ya kupwaya kidogo.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Msalimie Tuntemeke.
   
 7. m

  mujitahid Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kumbe nyigi jitihada zilikuwa kukuza na kulienndeleza kanisa dah vp sasa bado au kashamaliza kulitumikia..kwa kuwa mafanikio yake hayatupi nafasi kuwa atayafanya kwa nchi....hizi n zamu za vjana na ndio taifa la leo kama cdm ilivyo basi pia vijana ndio walivyo ndani yake
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tunachotaka ukoma uliopo CCM kutuuruhusu kuambukiza wengi Chadema kuhangaikia kuafuta madaraka na kupiga vita vya chini chini badala ya kuhangaika na kukijenga chama. Tukiendekeza hayo yatabaki ya miaka yote kugombania nafasi za uongozi kwa kupigana vikumbo bila mafanikio kwa vile ukiangalia wanaohangaikia kutafuta uongozi hawaelezi ababu za wao kufanya hivyo wakati muda muafaka haujawa.

  Muda ukifika kila mtu atakuwa huru kuchukua form za kugombea uongozi na ngazi huzika zitapitisha majina ya wanaofaa. Tukiendekeza haya ya kuanza kampeni za kuongoza tutabaki na vita vya kupigania naasi za uogozi badala ya kukijenga chama.

  Tusipoangalia wengi wanaochangia kutetea mambo ya kugombania madaraka na wale wa kutumwa toka CCM ili kuichafua Chadema. tuailinda Chadema kwa hali na mali, kwani sasa hivi hatudanganyiki tena.
   
 9. Miaghay

  Miaghay JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hii history haina timeline na details pia hazitoshi.
   
 10. aminiusiamini

  aminiusiamini JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,416
  Likes Received: 1,298
  Trophy Points: 280
  Wewe mwenye hujui kuandika naamini hata kuongea kwako tabu. So leta hoja kukataa hoja na anavyomfaham Dr Slaa. Hii sio analysis ni jinsi anavyomfaham.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  00000000000

  Hatuaandika kitabu cha historia, vinginevyo we utakosa cha kuongezea au kujadili. La sivyo ingekuwa ni kitabu cha kusoma tu si kitu cha kujadilika hapa jamvini.
   
 12. d

  dada jane JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe kwa hii analysis naenda kuwamegea wenzangu.
   
 13. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Umenena vema
   
 14. chelsea fc

  chelsea fc JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 835
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  dr.slaa ndio mtu sahihi kwa mustakhabali wa maendeleo ya nchi hii.....maendeleo yataletwa na upinzani....nyerere..1997
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kuna tofauti kubwa sana ya description na analysis. amefanya description bwana,analysis hajagusa hata angle moja mkuu.
   
 16. c

  chama JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi ni mtanzania kama hao wengine labda kama sina haki kuielewa ; imeandikwa kwa kiwango cha chini sana labda kama iliandaliwa kwa wanafunzi wa shule za kata; kujishusha daraja siwezi game yangu nyingine kabisa wewe ndio unapaswa upandishe kiwango

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mbona unaeleza vitu nusu nusu mkuu, ujasema kama Dr Slaa ana wake wawili ujasema Dr ana watoto wa ngapi ebu tufahamishe, umetaja mambo ya kanisa tu.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Usingeielewa kwa kiwango chako usingechangia, unavyoijibu kuna kila dalili ya kuielewa vizuri tu, ila kuna vipengere ambavyo kwa sababu zako binafsi za itikadi zetu katika masuala ya siasa yanakufanya ufikie hatua ya kusema sizitaki mbichi hizi.

  Hii mada si tesisi ya kuitetea kwa wahadhiri ili kupata degree, na mada yenye dondoo zilizodondoshwa na mwenye kuzifahamu kwa ajili ya kuufahamisha umma na kuzijadili. Pale usipopaelewa tuambie tukufafanulie. Tumejaribu kuiweka ielelweke katika uwanja ambao wetu tupo, la sivyo ingekuchangaya ziadi.
   
 19. c

  chama JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu pandisha kiwango tujadili mada; ni afadhali ya mbichi zinalika hizi zimevunda na kuoza kabisa; mkuu tunakula vitu FDA approved hivi vya majalalani hata Matonya (R.I.P) vilimshinda.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 20. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hongera kwa kuelimisha maana wengi kweli hawamjui Dr. Slaa kwa undani ndio maana wanampinga sana lakini kiukweli Dr. Slaa ni jembe anaupeo wamaono ya kimaendeleo
   
Loading...