Wasiokubali Kukosolewa Ni Watu Aina Gani?

Ukiwa na hirizi kiunoni ni marufuku kuhudhuria misibani. Ova
 
Msemo wa hakuna aliyekamilika una maana pana sana. Msemo huu hutumika kwa binadamu na siyo Mungu.

Maana ya msemo huu ni kwamba, haijawahi kutokea binadamu akafanya mambo yake kwa ukamilifu kwa asilimia zote mia, kwa maana ingine mwanadamu ni FALLIBLE. Kadhalika (kwa tulio na imani) tunaamini kuwa haijawahi kutokea Mungu akakosea, hii maana yake Mungu ni mkamilifu kwa kila jambo. Hajawahi kukosea, hawezi kukosea, na kamwe hatokuja kukosea kwa maana ya INFALLIBLE.

Vilevile kutokana na ukamilifu wake, Mungu ana sifa zote nzuri ambazo mwanadamu hana. Kwa mfano yeye ndiye mwema kuliko, mwenye nguvu kuliko, mwenye upendo kuliko, yupo popote, mwenye huruma kuliko pia anajua vitu vyote; yaani The Omniscient, The Omnipresent, The Omnibenevolent, na The Omnipotent. Pamoja na sifa zake zote hizo ambazo sisi wanadamu hatuna uhalali wa kumkosoa, ila wapo wanaomkosoa MUNGU na wala hana hasira nao, na hii ni kutokana na yeye Mungu kutokuwa dikteta. Nasema Mungu si dikteta kwa sababu alimpa mwanadamu free-will.

Ukiangalia mifano hiyo miwili kati ya ukamilifu wa Mungu na mapungufu ya mwanadamu, utagundua kwamba mwanadamu siku zote lazima akosolewe haijalishi ni mkubwa, ni mdogo, ni tajiri, ni masikini, ni mwanamke au mwanaume, ni mweusi au mweupe. Ni lazima akosolewe ili mambo yaende sawa. Na lazima akosolewe kwa sababu hana sifa kuu ambazo Mungu anazo yaani The Omnipresent, The Omnibenevolent, The Omnipotent, na The Omniscient.

Wakati Mungu mwenye sifa zote nzuri hana ghadhabu na wanaomkosoa, wapo wanadamu hawataki kukosolewa as if wao wana sifa kama za Mungu. Je, wanadamu hawa ni aina gani, au wanaitwaje?
Wanaitwa KOLERIKI [emoji35] [emoji35]
 
Ni tabia za kisaikolojia..wapo watu wanapenda kuona MTU akiteseka....Yericko aliwahi leta bandiko na nika comment tabia tofauti za wanadamu..japo nimeanza kubashiri kusudio la Uzi huu! watu wakifunguka utawalipia Mil.7?

Angalizo: comment mashudu ukipelekwa central..kutoka mwakani!
hahaaaa watu wakifunguka
yeye atakuwa busy kufungua Uzi mwingine wakuchangisha Rambi rambi ..ml.7 zitapatikna tu mkuu ONDOA mashaka
 
Hahahahaaa!Hivyohivyo kimtindomtindo tu.Mkistukia anajitetea kuwa kabeba bastola kwa ajili ya self-defense!
aiseeee
naskia shart kuu kwenye misiba hapaswi Ku appeared. ??
dunia inamambo

[HASHTAG]#Atubu[/HASHTAG]
 
Wasiotaka kukosolewa wa asili ya kutojiamini. Ukiangalia historia yao hata kipindi wakiwa shuleni wanajifanya wajuaji sana na akisolve swali ukimkosoa tu kesho hatakusaidia swali kingine. Mnakosana kabisaaa. Ni wa asili ya udictator.
 
Mtoa mada ni ukweli usio pingika hakuna binadamu asiyekosea na kujisahau kwa binadamu kupo ila tatizo lililokuwepo namna ya kumweka sawa mtu aliyekosea au kujisahau kunahitajika busara. Baba amekosea kwenye familia mbele ya mke wake na watoto wake unataka kumuweka sawa hapo ni vita tuu japo unachomwambia ni cha kweli ila ukimchukua pembeni ukimwambia makosa yake hapo mtaelewana vizuri sanaa, hata mtoa mada siku ukateleza ukaandika mambo ya hovyo wale watakao kufata pm utawaona wamaana sanaaa.
 
Msemo wa hakuna aliyekamilika una maana pana sana. Msemo huu hutumika kwa binadamu na siyo Mungu.

Maana ya msemo huu ni kwamba, haijawahi kutokea binadamu akafanya mambo yake kwa ukamilifu kwa asilimia zote mia, kwa maana ingine mwanadamu ni FALLIBLE. Kadhalika (kwa tulio na imani) tunaamini kuwa haijawahi kutokea Mungu akakosea, hii maana yake Mungu ni mkamilifu kwa kila jambo. Hajawahi kukosea, hawezi kukosea, na kamwe hatokuja kukosea kwa maana ya INFALLIBLE.

Vilevile kutokana na ukamilifu wake, Mungu ana sifa zote nzuri ambazo mwanadamu hana. Kwa mfano yeye ndiye mwema kuliko, mwenye nguvu kuliko, mwenye upendo kuliko, yupo popote, mwenye huruma kuliko pia anajua vitu vyote; yaani The Omniscient, The Omnipresent, The Omnibenevolent, na The Omnipotent. Pamoja na sifa zake zote hizo ambazo sisi wanadamu hatuna uhalali wa kumkosoa, ila wapo wanaomkosoa MUNGU na wala hana hasira nao, na hii ni kutokana na yeye Mungu kutokuwa dikteta. Nasema Mungu si dikteta kwa sababu alimpa mwanadamu free-will.

Ukiangalia mifano hiyo miwili kati ya ukamilifu wa Mungu na mapungufu ya mwanadamu, utagundua kwamba mwanadamu siku zote lazima akosolewe haijalishi ni mkubwa, ni mdogo, ni tajiri, ni masikini, ni mwanamke au mwanaume, ni mweusi au mweupe. Ni lazima akosolewe ili mambo yaende sawa. Na lazima akosolewe kwa sababu hana sifa kuu ambazo Mungu anazo yaani The Omnipresent, The Omnibenevolent, The Omnipotent, na The Omniscient.

Wakati Mungu mwenye sifa zote nzuri hana ghadhabu na wanaomkosoa, wapo wanadamu hawataki kukosolewa as if wao wana sifa kama za Mungu. Je, wanadamu hawa ni aina gani, au wanaitwaje?
Mkosoe mbowe ukione cha moto
 
Wanahirizi mkuu zinawapa kiburi
Hizo mambo si kutumainia zingekuwa na nguvu zingemsaidia yule wa Gambia asiondoke madarakani, na alikuwa gwiji wa waganga.Ni sawa ni kuchezea puto kwenye miba litapasuka tu,hizo mambo uleta utumwa, kutokujiamin,uoga, wasiwasi,ukosefu wa Amani na utulivu wa nafsi.Pia zinapay back maana hela ya shetani aipotei bure lzm uilipie.
 
IMG-20171230-WA0014.jpg
 
Ni tabia za kisaikolojia..wapo watu wanapenda kuona MTU akiteseka....Yericko aliwahi leta bandiko na nika comment tabia tofauti za wanadamu..japo nimeanza kubashiri kusudio la Uzi huu! watu wakifunguka utawalipia Mil.7?

Angalizo: comment mashudu ukipelekwa central..kutoka mwakani!
Nimeanza kuona maneno ya dizaini hii yakiongezeka kwa wana jf, kuna mmoja alisema anatamani ku-comment ila moyo unaenda mbio, vidole vinatetemeka na kutoa jasho, ni kusema hata ukitumia fake ID unadukulika humu jf?
 
Back
Top Bottom