Wasiokubali Kukosolewa Ni Watu Aina Gani?

Wasiokubali Kukosolewa Ni Watu Aina Gani?

Nimeanza kuona maneno ya dizaini hii yakiongezeka kwa wana jf, kuna mmoja alisema anatamani ku-comment ila moyo unaenda mbio, vidole vinatetemeka na kutoa jasho, ni kusema hata ukitumia fake ID unadukulika humu jf?

Ha ha ha ha...yawezekana mahirizi ya Sumbawanga yanatumika kuwajua watu hao...wenye fake ID.
 
CHA The GREAT

hamna mtu anayependa kukosolewa. Mimi binafsi ukinikosoa urafiki unapungua kama siyo kwisha kabisa. hasa kama mtu anayenikosoa hajatumia njia yenye staha, kwa lengo la kunidhalilisha na kutafuta umaarufu au kiki. huyo mara nyingi tunaishia kwenye bifu. hata wewe mkeo hapo nyumbani hawezi akakukosoa bila staha hata pengine mbele za watoto na watu wengine halafu ukaona sawa tu. au hawa wewe kumfanyia hivyo mkeo naye akaona sawa tu. mkiona hivyo ujue nyie ni majuha.
kwa watu wenye hekima wanatumia njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa mlengwa ili ufanye KAZI.
MAANA hasara ya kukosoa na matusi mhusika hatoi ushirikiano, ZAIDI atajihami (kuwa defensive)
na kuwa na hasira na chuki.
Mimi mtu ambaye nampenda ni yule anayenishauri kwa njia yenye staha. huyo namheshimu SANA. hata wakati ananishauri akinipa makavu tukiwa wawili nitaishia kujitetea na kumshukuru kuwa nitajitahidi kufanyia KAZI ushauri wake kulingana na hali zitakavyoniruhusu.
 
Mkuu wasiokubali kukoselewa ni Watu wasiojulikana na amri kutoka juuuuuu.
 
Back
Top Bottom