Wasiokubali Kukosolewa Ni Watu Aina Gani?

Wasiokubali Kukosolewa Ni Watu Aina Gani?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Msemo wa hakuna aliyekamilika una maana pana sana. Msemo huu hutumika kwa binadamu na siyo Mungu.

Maana ya msemo huu ni kwamba, haijawahi kutokea binadamu akafanya mambo yake kwa ukamilifu kwa asilimia zote mia, kwa maana ingine mwanadamu ni FALLIBLE. Kadhalika (kwa tulio na imani) tunaamini kuwa haijawahi kutokea Mungu akakosea, hii maana yake Mungu ni mkamilifu kwa kila jambo. Hajawahi kukosea, hawezi kukosea, na kamwe hatokuja kukosea kwa maana ya INFALLIBLE.

Vilevile kutokana na ukamilifu wake, Mungu ana sifa zote nzuri ambazo mwanadamu hana. Kwa mfano yeye ndiye mwema kuliko, mwenye nguvu kuliko, mwenye upendo kuliko, yupo popote, mwenye huruma kuliko pia anajua vitu vyote; yaani The Omniscient, The Omnipresent, The Omnibenevolent, na The Omnipotent. Pamoja na sifa zake zote hizo ambazo sisi wanadamu hatuna uhalali wa kumkosoa, ila wapo wanaomkosoa MUNGU na wala hana hasira nao, na hii ni kutokana na yeye Mungu kutokuwa dikteta. Nasema Mungu si dikteta kwa sababu alimpa mwanadamu free-will.

Ukiangalia mifano hiyo miwili kati ya ukamilifu wa Mungu na mapungufu ya mwanadamu, utagundua kwamba mwanadamu siku zote lazima akosolewe haijalishi ni mkubwa, ni mdogo, ni tajiri, ni masikini, ni mwanamke au mwanaume, ni mweusi au mweupe. Ni lazima akosolewe ili mambo yaende sawa. Na lazima akosolewe kwa sababu hana sifa kuu ambazo Mungu anazo yaani The Omnipresent, The Omnibenevolent, The Omnipotent, na The Omniscient.

Wakati Mungu mwenye sifa zote nzuri hana ghadhabu na wanaomkosoa, wapo wanadamu hawataki kukosolewa as if wao wana sifa kama za Mungu. Je, wanadamu hawa ni aina gani, au wanaitwaje?
 
Ni tabia za kisaikolojia..wapo watu wanapenda kuona MTU akiteseka....Yericko aliwahi leta bandiko na nika comment tabia tofauti za wanadamu..japo nimeanza kubashiri kusudio la Uzi huu! watu wakifunguka utawalipia Mil.7?

Angalizo: comment mashudu ukipelekwa central..kutoka mwakani!
 
Nikiamka kabisa nitakuandikia kwa kilugha chetu na kuchanganya na kihindi uelewe vizuri..
 
Kumbe binadamu wote hatujakamilika... kila mtu apambane na hali yake kwanini tuanze kunyosheana vidole fulani hafai mara atubu
 
Kumbe binadamu wote hatujakamilika... kila mtu apambane na hali yake kwanini tuanze kunyosheana vidole fulani hafai mara atubu
Yesu katika biblia aliwahi kusema kwamba ,ndugu yako akikosea mwambie!akikusikia umempata huyo la akikataa mwambie mtu mwingine awe kama shahidi na kisha mumfuate tena.lakini pia biblia hiyohiyo inasema,ukiona kosa kwa mwenzako mwambie na yeye akiona kwako pia akwambie.siyo hivyo unasema wewe,hatunyoosheani vidole,bali tunasaidiana.
 
Mkuu umesema vema,kukosea ni sehemu ya uanadamu ni sifa inayomtenganisha na sifa za muumba wake.Tatizo si kukosea tatizo ni kushupaza shingo na kukataa kutubu bila shaka ni kukana uwezo wa muumba.Dhambi ya Adam haikuwa tu kukataa kuishi mpango wa Mungu tu,bali alipopewa nafasi ya kutubu hakuitumia(unaweza kujiuliza wapi alipewa nafasi?Ni kupitia mahojiano ya ana kwa ana na Mungu pale bustanini).Hivyo kukosea si janga janga ni kukataa kwamba unafanya makosa na kujiingiza kwenye dhambi mbaya zaidi KIBURI hii hukupeleka kwenye mama wa dhambi zote UBINAFSI baada ya hiyo nafasi ya toba inakuwa finyu sana kwani mwanadamu hujiona sawa tu na Mungu.Mkumbukeni shetani na dhambi yake ilitokana na haya hata KUASI kukamfanya afukuzwe mbinguni.Tutubu tuache visingizio sisi ni viumbe tu tena vyenye udhaifu mwingi.Kutubu hakushushi hadhi yetu badala yake kunatujenga
 
Yesu katika biblia aliwahi kusema kwamba ,ndugu yako akikosea mwambie!akikusikia umempata huyo la akikataa mwambie mtu mwingine awe kama shahidi na kisha mumfuate tena.lakini pia biblia hiyohiyo inasema,ukiona kosa kwa mwenzako mwambie na yeye akiona kwako pia akwambie.siyo hivyo unasema wewe,hatunyoosheani vidole,bali tunasaidiana.
Ni ngumu sana kumkosoa mtu anayedhani anaonewa.Ukikosolewa usikaze shingo kwa kibri utapatwa na degedege la ukubwani.
 
Back
Top Bottom