Sikulaumu mwenzangu
Ila ni kipaji changu
Amenijalia mungu
Ndio nikakukosoa
Kama mimi mshairi
Jina langu ni Twahiri
Ni muelewa hodari
Daima najitungia
Unapotunga sanaa
Punguza yako fazaa
Sema kitu cha kufaa
Hazira inufaike
Sio wote waelewa
Kile kilokusudiwa
Yafaa kuzingatiwa
Nao wapate elimu
Uwache utandawanzi
Urudiye yetu enzi
Kutunga ni kubwa kazi
Mababu walitwambia
Sanaa inapotea
Nyinyi mnachekelea
Wakati mnatambua
Wapi tunaelekea
Sanaa ni ya zamani
Ukisema jukwaani
Hadhira pia fanani
Wote wanakuelewa
Maneno hayajanisha
Nachelea kukuchosha
Ama nikakuchekesha
Na jibu nalingojea
Na mimi nahitaji tiba..
nije?
^^
Hayo mawazo ulotoa
Ndio msingi wa mapokeo,kuamini kuwa ushairi ni kipaji toka kwa Mungu kwa watu maalum tu,,
Rejea Kanuni za Ushairi za Amri Abeid (1967) na Mashairi ya Shaaban Robert.
Wao husisitiza sanaa zaidi kuliko ujumbe.
Rejea mgogoro wa ushairi wa 1970 juu ya maana,asili,chanzo,n.k kuliko leta MASIVINA,MAVUE au Mashairi ya kisasa
^^
Hata hivyo Lengo langu ni wasifu wa wana MMU na si sanaa ya ushairi,,ningekuwa na nia ya kujenga sanaa ningeenda katika JUKWAA LA LUGHA.
Pia asante kwa changamoto ya kimapokeo.
Hoja zako zinajibiwa ktk ushairi wa Euphrase Kezilahabi-KARIBU NDANI
^^
halafu wee una pacha humu ndani, unalijua hilo? Nenda kule kwa wale new comer utamkuta.
Shukrani Himidini.
Btw kiplagati26 yuko Kusini mwa China.
Hvo nafasi yake ame-cover mpenzi wangu Ben Saanane na Remote.
Nitam fire very soon
kuna boss mmoja tu humu
wengine pretenders
wewe hujanijibu unajua?
plz come to my office!
elekeza your office ilipo..
angalia PM usipoelewa muombe Himidini akulete
ole wako nisiikuute pm ....lol
du aiseee umemjibu vizuri sana. atakuwa ni mfuasi wa mashairi ya kimapokeo. mashairi ya kisasa ni mashairi pia anapaswa kufahamu hilo.^^
Hayo mawazo ulotoa
Ndio msingi wa mapokeo,kuamini kuwa ushairi ni kipaji toka kwa Mungu kwa watu maalum tu,,
Rejea Kanuni za Ushairi za Amri Abeid (1967) na Mashairi ya Shaaban Robert.
Wao husisitiza sanaa zaidi kuliko ujumbe.
Rejea mgogoro wa ushairi wa 1970 juu ya maana,asili,chanzo,n.k kuliko leta MASIVINA,MAVUE au Mashairi ya kisasa
^^
Hata hivyo Lengo langu ni wasifu wa wana MMU na si sanaa ya ushairi,,ningekuwa na nia ya kujenga sanaa ningeenda katika JUKWAA LA LUGHA.
Pia asante kwa changamoto ya kimapokeo.
Hoja zako zinajibiwa ktk ushairi wa Euphrase Kezilahabi-KARIBU NDANI
^^
hahahaaa usipoikuta ujue imesomwa na mwingine then ikadeletiwa
Nisipoiona ndo ntajua we ni doctor for real
au Dr Manyaunyau
hahahaaaaa! Husinifananishe na huyo bhana...! Nimeku PM Kama tano kwa hasira