Wasifu wa Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
MAISHA YAKE

Mhe. Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja. Ameolewa na Bw. Hafidh Ameir na wamejaaliwa watoto wanne, watatu wa kiume na mmoja wa kike.

ELIMU NA MAFUNZO

Mhe. Samia Suluhu Hassan alipata elimu ya msingi katika shule mbalimbali, zikiwemo Shule ya Msingi Chwaka iliyoko Unguja kuanzia 1966 hadi 1968, Shule ya Msingi Ziwani mwaka 1970 na Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972. Baada ya hapo, alijiunga na Shule ya Sekondari ya Ng’ambo kwa ajili ya masomo ya Kidato cha Kwanza hadi cha tatu, na Shule ya Sekondari Lumumba kwa ajili ya Kidato cha Nne kati ya mwaka 1973 hadi 1976.

Mwaka 1983, alipata Astashada katika Mafunzo ya Takwimu kutoka Chuo cha Uchumi, Zanzibar. Baada ya kufanya kazi kwa kipindi kifupi kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo, mwaka 1983 hadi 1986, alijiunga na Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) kwa ajili ya masomo ya juu katika Utawala wa Umma. Aidha, alipata mafunzo mbalimbali katika Taasisi ya Chuo cha Utawala wa Umma Lahore, Pakistan 1987, Taasisi ya Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) 1991, na Taasisi ya Uongozi ya Hyderabad India 1998 kwa ajili ya Astashahada ya Utawala. Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Manchester kilichopo Uingereza kwa ajili ya masomo ya Juu ya Uchumi. Vilevile, alipata Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii kupitia programu ya pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire, Marekani.

UZOEFU NDANI YA SERIKALI

Mhe. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliapishwa Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ndugu Samia ni mwanamke wa kwanza nchini kushika nafasi za Makamu wa Rais na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyadhifa nyingine alizoshika ndani ya Serikali ni; Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mambo ya Muungano 2010/2015; Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2005/2010 na Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira, Maendeleo ya Wanawake, na Watoto, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 2000/2005. Mwaka 2014, alihudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Bunge lililojadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuandaa rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania. Mwaka 1987 hadi 1988, alikuwa Afisa Mipango Rasilimali Watu na Mwaka 1977 hadi 1983, Karani Masijala.

UZOEFU NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mhe. Samia Suluhu Hassan aliingia katika siasa kama mwanachama wa CCM tarehe 10 Juni, 1987. Aliingia katika siasa za uchaguzi mwaka 2000 katika nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar kama Mwakilishi wa Viti Maalum vya Wanawake hadi mwaka 2010. Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, aligombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Makunduchi, Zanzibar.

Mwaka 2002, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, na vile vile, kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi; nyadhifa ambazo ameendelea kuzifanyia kazi hadi leo. Ndugu Samia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja; na alikuwa Mjumbe wa Kamati za Siasa Mkoa na Wilaya ya Kusini Unguja.

Kwa upande wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi, Ndugu Samia ni mwanachama wa Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT) kuanzia mwaka 1996 hadi leo. Aidha, ameshiriki katika kuandika Ilani ya Chama cha Mapinduzi mara nne mfululizo kuanzia 2005/2010, 2010/2015, 2015/2020 na 2020/2025.

UZOEFU KATIKA TAASISI NYINGINE

Mwaka 2016, Mhe. Samia aliteuliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki Moon, kuwa Mjumbe wa Jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi, akiwakilisha Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kati ya mwaka 2016 na 2017. Katika kipindi cha ujumbe wake, aliwasilisha mambo 27 kwenye Jopo hilo, ambayo Serikali ya Tanzania ilibainisha kama hatua za kimkakati kwa ajili ya kuweka mfumo endelevu wa kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Miongoni mwa matokeo ya kazi zake ni kusimamia uanzishwaji wa majukwaa ya uchumi ya wanawake nchini kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wafanyabiashara wadogo na wakati kwenye masoko, hasa wanawake wanaoishi mipakani, kuwaunganisha na mikopo nafuu na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali; na kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuanzisha kampeni ya kuongeza uwajibikaji katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto, maarufu kama “Jiongeze Tuwavushe Salama”.

Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme) mwaka 1988 hadi 1997. Vile vile, amefanya kazi katika Kamati, Bodi na Taasisi mbalimbali kama vile; Mjumbe wa Kamati ya Msamaha wa Wafungwa (Parole Committee) ya Zanzibar (2001- 2010), Mlezi wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar (1997-2000), Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote – EOTF (1996-2000), Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Taasisi zisizo za Kiserikali Zanzibar (ANGOZA) 1995-2000, Mwanachama wa Lions Club Zanzibar (1991-1998), Mjumbe wa Kamati ya Uundaji wa Sera ya Elimu Zanzibar (1996) na Mwanachama Mwanzilishi wa Taasisi ya Kuchochea Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (1991-1994).

MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ngoja niihifadhi hii
 
Hana wasifu mrefu hivyo. Umeandika uongo
 
Shule na msingi na sekondari alisoma kwa kuhama hama sana kulikuwa ni kwa sababu gani. Sio mbaya iko vizuri tu
 
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN​

Wataalam wa taaluma tuelimisheni inachoonyesha na kusema CV hii 'kali' kuliko ya marais wote walioiwahi kuongoza Bongolalaland.

CHANZO: TOVUTI YA IKULU Ikulu | Wasifu
 
Unajua maana ya kujitosheleza au ni njaa, uchawa, uzwazwa na kujikomba vinasumbua? Wakati mwingine, elimu chafu na finyu ya madrassa ni taabu tupu.
Sawa mkuu, lkn angalia wasifu wake huo kwani ulikuwa haumtoshi kuwa na uwezo mkbwa zaidi. ? Read between lines katia comments zangu sio unakurupuka tu kuonesha namna gani uwezo wako ni mdogo.
 
Mhe. Samia Suluhu Hassan alipata elimu ya msingi katika shule mbalimbali, zikiwemo Shule ya Msingi Chwaka iliyoko Unguja kuanzia 1966 hadi 1968, Shule ya Msingi Ziwani mwaka 1970 na Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972. Baada ya hapo, alijiunga na Shule ya Sekondari ya Ng’ambo kwa ajili ya masomo ya Kidato cha Kwanza hadi cha tatu, na Shule ya Sekondari Lumumba kwa ajili ya Kidato cha Nne kati ya mwaka 1973 hadi 1976.
Yeye kazaliwa tu Kizimkazi bila ya kuwa na wazazi?

Ni sababu zipi zilizo mfanya asome shule za primai nyingi kiasi hicho; ni sababu zipi zilifanya ahame sekondari.

Hata hivyo, elimu ya huko chini unahangaika nayo kiasi hiki kwa sababu zipi hasa?
 
Watu ni mahodari wa kuungaunga.
Hongo, mkuu. Bila shaka hongo imetembea sana wakati wote huo!

Inaonyesha huyu hajawahi kuwa na maisha tulivu hata siku moja. Ni mihangaiko hangaiko tuuu kila sehemu
Ukifuatilia vizuri, hata miaka ilipo tajwa imeingiliana; sasa haijulikani hivyo vikozi vilikuwa ni vya muda gani!

Huyu alikuwa 'busy' sana kwa hongo kwenye maeneo yote hayo alikopitia.

EEEeeeeh! Ukitumia msemo wake maarufu: "alikula kwa urefu wa kamba yake".
 
Gundua kuwa wengi waliofoji miaka ya kuzaliwa huanzia na mwezi January, huyu naye ni hivyo hivyo!.

Angalizo: Mtu amezaliwa mwaka 1960 anadai ameanza darasa la kwanza mwaka 1966? ... Wakati huo mtoto bila kuwa na miaka saba kamili huruhusiwi kuanza darasa la kwanza.
 
Kweli huyu Samia ni mwongo,me nimeanza darasa la kwanza nikiwa na miaka kimi,kuanzia miaka ya 70-90 kuanza shule lazima uwe na miaka kuanzia 10 na hapo usiwe mfupi, Maana kipimo ilikuwa kupitisha mkono wa kulia kichwa na kushika sikio la kushoto,kitu ambacho watoto wafupi walishindwa na kurudishwa nyumbani labda kwa huruma za mwalimu mkuu.Samia huyu kaforge vyeti,kasoma helimu ya watu wazima,henzi hizo haiwezekani kuanza shule na miaka 6.
 
Huo wasifu bora wangeuficha tu, kuuweka hadharani hivi ni dharau ya wazi kwa watanzania hasa kwa mtu asiyekuwa na vigezo kuongoza watu million 60+

Mimi nilikataliwa kuanza darasa la kwanza 1965 pamoja na dada nikiwa na miaka pungufu ya sana, kipimo cha kushika sikio kilinitoa kwenye kinyang'anyiro mpaka nilipotimiza miaka saba nikaandikishwa darasa la kwanza....

Enzi hizo Tanganyika ndio ilikuwa na shule nyingi za Serikali zilizorithiwa kutoka madhehebu ya kidini, hasa Catholic na Anglican tofauti na Zanzibar... Nina wasi wasi kama kweli kilichoandikwa kina ukweli maana hakuna uhalisia.... 😲
 
IMG_20250418_152128.jpg

Hivi kwa mfano tunatoka Dar kwenda Arusha kwenye basi. Halafu ghafla tulipofika mitaa ya korogwe tukiwa katikati ya safari,dereva wa basi letu anapatwa na homa kali na kuumwa sana kiasi akashindwa kuendelea na safari.

Then akaja dereva mwingine na kushika nafasi yake safari ikaendelea.

Swali langu, je baada ya dereva mpya kushika usukani,hiyo itamaanisha kuwa safari nayo itakuwa ni safari mpya au safari ile ile ila dereva ni mpya?

Okay,with the same logic. Hadi mwaka 2020 wakati wa uchaguzi na Magufuri alikuwa raisi wa jamuhuri ya muungano huku makamo wake akiwa ni Samia.

Baada ya kifo cha Utata cha magufuri, Samia akawa ndie mrithi wa nafasi ya uraisi wa jamuhuri ya muungano na akatakiwa kupewa makamo wake kumsaidia.

Ila hakuna uchaguzi ulifanyika wala haikuwa process ya kawaida ya kupata raisi wa awamu mpya bali ni process ya nadra na bahati mbaya kutokea chanzo kikiwa ni msiba.

Sasa swali la kujiuliza,why inaitwa awamu mpya au awamu ya sita badala ya tano?🤔

Nadhani kuna muda kama raia tuwe makini sana na nani anazungumza kipi na kinakwenda kuhifadhiwa vipi katika kumbukumbu za kudumu za kitaifa.

Samia anaingia katika kumbukumbu za jamii yetu kama raisi wa kwanza wa kike wa jamuhuri ya muungano ila sio raisi wa awamu ya sita.

Uchaguzi huu alitakiwa sasa kusema inatafutwa awamu ya sita ila si kweli kuwa kuna awamu ya sita bali kwasasa tuna awamu ya tano ile ile ikimalizia muda wake kisheria na kikatiba. Awamu ya kwanza Nyerere,ya Pili ni Mwinyi,ya tatu ya mkapa,ya nne kikwete,ya tano magufuri,sita bado uchaguzi wake ni 2025.

Acheni kupotosha.
 
Back
Top Bottom