Hizi taasisi zina mamlaka ya kusimamia elimu ya sekondari na vyuo
Elimu ya msingi na sekondari ya bwana Paul Makonda imezua maswali hivi karibuni, taasisi muafaka ya kuondoa shaka,tena kwa kutumia nyaraka halisi na kuziweka wazi ni Baraza la Mitihani Tanzania.
Itueleze kama alisoma pamba secondary ,index namba yake, matokeo yake ya mock,na pia shule ya msingi aliyotoka,na kama alichukua cheti cha mtu aliyesoma BUSWELU sekondari, pia tuambiwe alitokaje pamba sekondari akaenda BUSWELU sekondary
Kuhusu suala la kusoma DIPLOMA chuo cha uvuvi Mbegani,NACTE watoe ufafanuzi iwapo mtu huyu alisoma diploma mbegani,kwa jina gani,na aliingia kwa maksi zipi,na alisoma form six wapi(hii ya form six haisemwi alisoma wapi)
Tunajua huwezi kusoma diploma bila kupitia "A" level,ni nani alimpa admission
Kuhusu elimu ya juu,TCU itoe ufafanuzi.
Ikishindikana basi wizara ya elimu iingilie kati
Pia msajili wa hati (DEED POLL) wizara ya ardhi kwa mzee lukuvi,atuambie kama ana rekodi zozote za huyu bwana kubadili jina na zilisajiliwa lini na lini zilitangazwa kwenye gazeti la serikali (Government Gazette),