Wasifu (CV) wa Freeman Mbowe huu hapa...

Tuangalie zaidi Performance na cyo umiliki wa makaratasi yanayoitwa CV.NEWTON na ALBERT ENSTEIN Walifanya mambo makubwa sana na ya kukumbukwa vizazi na vizazi ktk Dunia hii japo elimu yao hata degree moja tu hawakuwa nayo, Tz tuna mtu tunayemuita kuwa ni msomi( PROF LIPUMBA) lkn mambo anayoyafanya ni ya kishenzi kiasi kwamba hata mtu wa darasa la saba hawezi kuyafanya.
Ndugu zangu haya makaratasi yanayoitwa Certificates tuwe nayo tu kadri kila mtu atakavyoona inafaa ila performance ya mtu katika Kazi yake ndo kitu cha muhimu zaidi.
SHIVIJI, LIPUMBA,MAGEMBE na KAPUYA Wote hawa ni ma Professor lkn performance zao zinatofautiana kwa kiasi kikubwa mno.
Uelewa wa mambo wa shivji uko juu mno ukilinganisha na ule wa LIPUMBA.
Kwa hiyo jamani tusipotoshwe na haya makaratasi.
Katika history ya Tanzania, kwa wenyeviti wa vyama vya siasa walioongoza vyama vyao kwa mafanikio makubwa ni NYERERE na MBOWE tu.Wenye timamu zao watakuwa wameelewa ila wale washabiki kamwe hawatakaa waelewe.
 
Ndugu magoiga umefanya vyema sana kutaka kujua elimu ya Freeman mbowe maana ulivyosema kuwa elimu ya mtu huwa ni sehemu ya historia yake. Nilidhani wewe ungekuja na majibu mujarabu ya kutufumbulia fumbo hili la elimu ya ndg mbowe freeman. Wewe umesema "Kama kuna kitu ambacho hakuna mtanzania anayekifahamu bayana ni elimu ya Freeman. Hakuna mtu yeyote ajuaye Freeman alisoma wapi elimu ya msingi, elimu ya sekondari wala chuo. Hakuna mtu hata mmoja ndani ya chama chake anayeweza kusema bayana kuwa anaifahamu historia ya kielimu ya kiongozi wao" unaendelea kusema "Ndugu yangu mmoja amenitaarifu kuwa Freeman alisoma elimu ya kidato cha sita (Form Six) pale IHUNGO sekondari". Sasa ndg huoni contradiction kwenye nukuu hizo , unasema hakuna anayejua mbowe alisoma wapi at the same time unasema ndg yako alikuambia alisema IHUNGO kwanini hujamuuliza alikuwa anatumia majina gani na ni miaka ipi?. ''Na ni kwanini hakuna mtu yeyote anayejitokeza kusema kuwa alisoma na Freeman'', kaka umefanya kuuliza watu wangapi nchi nzima ukakosa? kwahiyo kama hakuna aliyejitokeza kusema kasoma na mbowe tafsiri yake ni kwamba hajasoma?. mimi sijawahi kusikia mtu akisema kasoma na baba yangu shule ila ninachojua mzee wangu ana masters, sijasikia kwasababu kwa wengine kusoma na baba yangu ni immaterial.

Ili kuondoa ukakasi ungetuambia MTEI alikuwa gavana miaka ipi na mbowe alifanya kazi huko miaka ipi na alimuoa mtoto wa mtei mwaka gani, hii inaweza kutupa ukweli kama alipewa kazi baada ya kuoa au kabla.Halafu mtu kutumia majina mawili shule mara zote si kununua majina ya watu, mimi nilisoma darasa la kwanza hadi la 4 kwa jina tofauti na nililomaliza nalo la saba. kisha form one hadi two nikatumia jina lingine na form three hadi chuo nimetumia jina lingine, nilipoenda kuomba kazi wakanidai chedi cha la saba wakaona jina ni tofauti na vyeti vya form four ,six na chuo nikaenda mahakani kuapa kuwa majina yote ni ya kwangu, primary waliniandikisha jina sikulipenda nilipopata uhamisho shule nyingine nikabadili jina la nne, kisha hilo jina pia nikalibadili form 3 na kujibatiza jina langu linatumika kwenye mambo ya shule hadi leo na kwa taarifa yako mimi sijawahi kufeli wala kurudia shule. Elimu ya mtu kutokuwa wazi haimaanishi hajasoma maana huenda alisoma nje ya nchi. Lakini pia elimu bila mafanikio ni ujinga na joho bila kazi ni dera ni bora tukawaiga watu kama AMIDU, LA CAIRO, ZAKARIA wenye elimu ndogo huku wakiwa na mafaniko makubwa na si propaganda za kijinga.
 
Ngoja nikueleze Freeman hakusoma kabisa lakini anaongoza vzr chama ...uongozi wake na mafanikio yake kuijenga chadema kutoka wabunge watano mwaka 2000 mpaka ilio nao leo....ni kitu ya kupigiwa mfano....tunampa ile alopewa kiwete inaitwa sijui nini ile ya heshima....endeleeni kujijambia anakuja na kata funua...mtoa mada angalia asikufunue
NAWAKILISHA
 
hahaha tunahoji kutokana na utendaji wake kazi una walakini za kutosha kuuliza kama ako na elimu alnayosema anayo
 
.

Labda turudi nyuma kidogo, alipogombea urais sheria ya kuwa mgombea lazima awe na degree haikuwepo? Kama ilikuwepo aliruhusiwaje kugombea kama ni kweli hakuna historia ya elimu yake?

Katiba ya JMT ya 1977 haijawahi kuwa na kipengele cha elimu kwa mgombea urais wala mbunge na hata diwani.

Ukisoma kifumgu cha 39(1)d kinataka mgombea urais awe na sifa za kuwa mbunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi maanake awe anajua KUSOMA NA KUANDIKA tu.

Mambo ya degree yalikuwa kwenye rasimu ya Katiba mwaka jana.
 
Kwa wenye elimu ya siasa na wanaofanya siasa, hangaikeni kujibu hili, maana hii ni siasa katika uhalisia wake. Ukitoa neno siasa kwenye hili basi linageuka kuwa umbea, udhaifu, ulimbukeni na kupoteza muda. Unakuwa huna tofauti na mtu ambaye anafuatilia nyendo na historia za jirani yake kwa kiwango kikubwa mpaka anajiaibisha mbele ya halaiki. Kama unaamini falsafa ya 'hapa kazi tu' basi chapa kazi uendeleze chama chako acha umbea, unajengaje chama kwa kuchunguza historia za wapinzani wako badala ya kufikiria vitu vipya vya kuongeza idadi ya wanachama katika level yako. kuwa mbunifu acha uvivu. Hizi ni mbinu za kivivu, badala ya kujenga kikubwa zaidi ya alichojenga mpinzani wako, unataka kuvizia ubomoe alichojenga yeye.
 
Amewazidi nguvu?
 
Nini lengo lako hasa? Je elimu yake inasaidia nini katika maisha ya leo?
Don't be defensive. Huyu ni kiongozi mkubwa hapa nchini. Ni mwenyekiti wa chama Kikuu cha Upinzani. Siku moja anaweza kuwa rais. Hivyo tuna haki ya kumjua kindakindaki.
 
Hoja ya kufanya kazi BOT bila kututajia kazi aliyokuwa akiifanya ni uzumbukuku sababu BOT kulikuwa hadi na wafagizi na madereva ambao pengine ni illiterates.

Mambo ya "Baba kanituma" hayajaanza leo nchi hii.
 
Muulize kinana aliuonaje mziki wake?Nasikia mnasema STANDADI FOO YA MKOLONI ..Kwa wazungu hata vyeti hawataki.Kwa ccm kamasi linawatoka bado wanadai vyeti badala ya kuangalia nanmna ya kujinasua ktk huu mziki.
 
Wanasahau pia kuwa familia ya Mwalimu na ya Mzee Aikaeli walikuwa na ukaribu sana.
 
Don't be defensive. Huyu ni kiongozi mkubwa hapa nchini. Ni mwenyekiti wa chama Kikuu cha Upinzani. Siku moja anaweza kuwa rais. Hivyo tuna haki ya kumjua kindakindaki.
Haha..Vipi mmeambia ndie kaifilisi serikali yenu? Kasome profile ya ROSTAM kuhusu sehemu ya elimu. Kwani Office ya Bunge haijui?Kwani Serikali ya CCM haina KUMBUKUMBU ZA WATANZANIA WALIOSOME CHINI YA UTAWALA WAKE? What a shame?
 
BAVICHA njooni mjibu swali!!!
zaidi ya miaka 50, ccm na usalama wao wa taifa baado wanauliza mitaani elimu na vyeti vya watu muhimu ktk nchi na serikali what a shame?Kwa vile mna ZIKa mnaona mmegundua sana kitu cha kuwatoa kimasomaso Lumumba ,nanyi mpewe vyeo vya rusuku.
 
Elimu yako imekusaidia nn..nyie Ndy wazee wa kusoma kwa KUKARIRI tu

OVA
Leo ndiyo unajua kuwa elimu ya mtu haisadiii ...Hovyo kabisa mlivyokuwa mnahangaika na elimu ya Mwenye nchi mlitaka uwasaidie nini ..
 
hapana hakuajiriwa na serikali ya CCM, aliajiriwa na mkwewe Mtei.

Kama hauna uhakika uliza upewe uhakika kabla hujaaanza kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.
Mtei alistep down BOT miaka ya 70 mwishoni.. Mbowe miaka ya 70 mwishoni alikuwa hajafikisha hata miaka 20.. Sasa sijui aliajiriwaje huko BOT na Mtei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…