Wasichana wang'ara matokeo kidato cha 6

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Wasichana wang'ara matokeo kidato cha 6
Saturday, 02 May 2009 09:40
* Kiwango cha kufaulu chapanda
* Kumi na saba wafutiwa matokeo

Na Said Mwishehe

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato Sita uliofanyika Februari mwaka huu, huku shule za wasichana zikingiza .

Katika matokeo hayo, Shule ya Wasichana ya Kibosho ya mkoani Kilimanjaro, imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Sekondari ya Wasichana ya Marian ya mkoani Pwani.

Akitangaza matokeo hayo Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji NECTA, Dkt. Joyce Ndalichako alisema ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha madaraja kuanzia daraja la I hadi III.

Pia alisema shule hizo zimegawanywa katika makundi mawili, kulingana na idadi ya watahiniwa. Kundi la kwanza ni lenye watahiniwa 25 na zaidi na kundi la pili ni lile lenye watahiniwa chini ya 25.

Kutokana na mpangalio huo, Shule ya wasichana Kibosho na Marian zimeshika nafasi ya kwanza.

"Mwaka huu shule za wasichana zimefanya vizuri zaidi, hata katika ufaulu pia wasichana wamewazidi wavulana hali inayoashiria kuwa safari hii wasichana wamewazidi wavulana katika kiwango cha ufaulu matokeo ya kidato cha sita," alisema, Dkt. Ndalichako.

Akizungumzia matokeo ya watahiniwa wote, Dkt. Ndalichako alisema jumla ya watahiniwa 45,716 sawa na asilimia 89.64 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo, wamefaulu.

Wasichana waliofaulu ni 17,152 sawa na asilimia 90.92 ya wasichana waliofanya mtihani. Wavulana waliofaulu ni 28,564 sawa na asilimia 88.89 ya wavulana waliofanya mtihani.

Alifafanua kuwa watahiniwa wa shule waliofaulu ni 36,472 sawa na asilimia 94.37 ya watahiniwa wa shule waliofanya mtihani huo. Mwaka 2008 watahiniwa wa shule waliofanya mtihani ni 29.924 sawa na asilimia 92.72.

Hivyo idadi ya watahiniwa wa shule imeongezeka kwa watahiniwa 6,548 ambayo ni sawa na asilimia 21.9 ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana.

Akizungumzia zaidi ubora wa ufaulu kwa jinsia, Dkt. Ndalichako alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule katika mitihani ya kidato cha sita mwaka huu, umeonesha jumla ya watahiniwa 32,023, sawa na asilimia 82.86 wamefaulu katika madaraja I-III.

Wasichana waliofaulu katika madaraja hayo ni 12,053 , sawa na asilimia 82.84 na wavulana ni 19,970 sawa na asilimia 82.87.

Alitaja shule 10 ambazo zimefanya vizuri katika matokeo hayo zenye watahiniwa zaidi ya 25 kuwa ni Kibosho Girls (Kilimanjaro), Marian Girls (Pwani), Kibaha (Pwani), Mzumbe (Morogoro), Ilboru (Arusha), Malangali (Iringa), Maua Seminari (Kilimanjaro), Uru Seminari (Kilimanjaro), St. Mary Goreti (Kilimanjaro) na Boniconsili Mabamba Girls (Kigoma).

Kwa upande wa shule 10 bora zenye watahiniwa chini ya 25, iliyoshika nafasi ya kwanza ni St. James Seminari (Kilimanjaro) ikifuatiwa na Kisimiri (Arusha), Masama Girls (Kilimanjaro), Katoke Seminari (Kagera), St. Joseph -Kilocha Seminari (Iringa), Usa Seminari (Arusha), St. Peter's Seminari (Morogoro), St. Francis Desales Seminari (Morogoro), Arusha Catholic (Arusha) na Dungunyi Seminari (Singida).

Shule 10 za mwisho katika kundi la shule lenye watahiniwa zaidi ya 25 ya kwanza kutoka mwisho ni Andrew Faza Memorial (Dar es Salaam), Mount Kilimanjaro (Kilimanjaro), Likonde Seminari (Ruvuma), Hekima (Kagera), Mambwe (Rukwa), Dongobeshi (Manyara), Donbosco-Didia (Shinyanga), Adolec (Kagera), Nyuki (Zanzibar) na Rosemerie (Pwani).

Shule 10 za mwisho kwa upande wa shule zenye watahiniwa 25 na zaidi ya kwanza ni Ambassador (Dar es Salaam), Maswa Girls (Shinyanga), Dodoma Central (Dodoma), Fidel Castro (Pemba), Muslim College (Zanzibar), Uweleni (Pemba), Tumekuja (Zanzibar), Popatlals (Tanga), Dr.Olsen (Manyara) na Jaffery (Arusha).

Akizungumzia wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, Dkt. Ndalichako alisema wamepatikana kwa kuangalia wastani wa alama za jumla walizopata pamoja na muunganisho wa masomo (combination).

Mwanafunzi wa kwanza kwa upande wa wasichana ni Sophia Nahoza (PCM) wa Marian Girls (Pwani) , Lilian Ahmed (HKL) wa Boniconsili Mabamba Girls ya Kigoma), Tunu Mangara (PCM) Marian Girls (Pwani) na Naomi Elibariki (HGE) Jangwani (Dar es Salaam).

Wengine ni Agnes Dominick (HKL) Kibosho Girls (Kilimanjaro), Habiba Twaha (HGK) Lumumba (Unguja), Furaha Amos (ECA) Marian Girls (Pwani), Amina Mziray (HKL) Machame Girls (Kilimanjaro), Asimwe Rugunyoisa (HKL) Barbro-Hohansson (Dar) na Upendo Stiven (ECA) Weruweru (Kilimanjaro).

Kwa upande wa wavulana, aliyeshika nafasi ya kwanza ni Auden Kileo (PCM) Kibaha (Pwani), Raymond Aidan (PCM) Kibaha (Pwani),Frank Shega (PCM) Tabora Boys (Tabora), Charles Simkonda (PCM) Ilboru (Arusha), Maclean Mwaijonga (PCM) Fezza Boys (Dar) na Atupele Kilindu (PCM) Mzumbe (Morogoro).

Wengine ni Athuman Juma (PCM) Ilboru (Arusha), Dickson Mutegeki (PCM) Tabora Boys, Michael Andrew (PCM) Ilboru (Arusha) na Fidahussein Premji (PCM) Al-Muntazir Islamic (Dar).

Wanafunzi 10 waliofanya vizuri kwa ujumla kitaifa ni Auden Kileo, Raymond Aidan, Frank Shega, Charles Simkonda, Maclean Mwaijonga, Sophia Nahoza, Atupele Kilindu, Athuman Juma, Dickson Mutegeki na Michael Andrew.

NECTA pia limefuta matokeo ya watahiniwa nane wa shule na watahiniwa 17 wa kujitegemea kwa kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani.

Pia watahiniwa 53 waliofanya mtihani wakiwa na sifa zenye utata, watathibitishiwa uhalali wa matokeo yao baada ya kuwasilisha vielelezo vya kuthibitisha uhalali wao.

Watahiniwa 33 wa Shule ya Sekondari Engusero iliyoko Manyara na Breakthrough ya Pwani hawakupewa matokeo yao kutokana na kutolipa ada ya watahiniwa hadi pale watakapolipa.

Dkt.Ndalichako, alisema Baraza limefuta matokeo ya kidato cha nne kwa wanafunzi wawili kwa kubainika kufanya udanganyifu.

Wanafunzi wengine 50 wa kujitegemea wa kituo cha Shule ya Sekondari Konde matokeo yao yamefutwa kwa kufanya udanganyifu katika mitihani ya kidato cha nne mwaka 2008.
 
Back
Top Bottom