Watahiniwa 106,955 kuanza mitihani ya Kitaifa ya Kidato cha 6 leo Mei 2 hadi Mei 22, 2023

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Baraza la Mitihani (NECTA) limesema kuwa leo Mei 2, 2023 Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita utaanza huku likitoa namba maalum ya kupokea taarifa za udanganyifu wa aina yoyote utakaofanyika katika vituo vya mitihani ambayo wadau wanapaswa kuitumia

Katibu Mtendaji wa Baraza, Dk. Said Ally Mohamed, alitangaza hilo jana mkoani Dar es Salaam na kuitaja namba hiyo kuwa ni 0759 360 000.

Kiongozi huyo alisema mtihani huo utaanza kesho hadi Mei 22 mwaka huu. Watahiniwa 106,955 wamesajiliwa kuufanya ambapo kati yao, wa shule ni 96,914 na wa kujitegemea ni 10,041.

Alisema kati ya watahiniwa wa shule waliosajiliwa, wanaume ni 53,324 sawa na asilimia 55 na wanawake ni 43,590 sawa na asilimia 45.

"Watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 181. Kati yao, 114 ni wenye uoni hafifu, 14 ni wasioona, 28 wenye ulemavu wa viungo vya mwili na mmoja ni mwenye mtindio wa akili," alifafanua.

Alisema kuwa kati ya watahiniwa wa kujitegemea 10,041 waliosajiliwa, wanaume ni 6,248 sawa na asilimia 62 na wanawake ni 3,793 sawa na asilimia 38. Mmoja ana uoni hafifu.

Pia alisema kutafanyika mitihani ya ualimu ambayo itakayomalizika Mei 16 mwaka huu, ikihusisha watahiniwa 8,906. Kati yao, 2,344 ni wa ngazi ya stashahada na 6,562 ni wa ngazi ya cheti.

"Ngazi ya stashahada wanaume ni 1,438 sawa na asilimia 61 na wanawake ni 906 sawa na asilimia 39. Watahiniwa ngazi ya cheti, wanaume ni 2,885 sawa na asilimia 44 na wanawake ni 3,677 sawa na asilimia 56. Wenye uoni hafifu wapo watatu kwa ngazi ya stashahada na wanne ngazi ya cheti. Tuna mtahiniwa mmoja asiyeoona," alisema.

Dk. Mohamed alisema kuanzia kesho hadi Mei 15 mwaka huu, kutafanyika mtihani wa marudio wa kidato cha nne ukihusisha wanafunzi 337 ambao matokeo yao yalifutwa mwaka 2022 kutokana na udanganyifu.

"Uamuzi wa watahiniwa kurudia mitihani umezingatia kuwa zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa waliofanya udanganyifu huo, chanzo kilitokana na mipango iliyofanywa na kuratibiwa na vituo husika kwa kushirikiana na wamiliki wa shule, wakuu wa shule, walimu na wasimamizi wa mitihani
 
Mwaka huu vyuo vitaneemeka maana wanafunzi 40,000 wataendelea na chuo
 
Kila la heri watahiniwa wote. Kumbe kidato Cha sita watahiniwa ni wachache hivyo? Less than 7% of the birth cohort!
 
Back
Top Bottom