Wasichana wanavyojidanganya wakiwa 20's

Wasichana wanavyojidanganya wakiwa 20's

PARADIGM

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2014
Posts
2,774
Reaction score
1,830
Tumezoea kusikia matamko kutoka kwa mabinti kama vike
kazi ndiyo mume wangu,
mume si lazima ninaweza kuzaa nikalea mwenyewe,
kuolewa siyo lazima,
kuishi single ndo maisha niliyoamua, n.k

Mi nafikiri wasichana wengi hudanganywa na umri kwamba walivyo wataendelea kuwa on demand ya wanaume na hivyo wakihitaji mume watampata. Ya nini kuwa chini ya mtu mwingine.Kumbe hawajui umri unavyosogea waliokuwa wakikupapatikia nao wanaendelea kupungua.

Wengine wameamua kuzaa aidha kwa bahati mbaya au kwa sababu nilizoeleza hapo awali. Lakini kauli ya "mwanaume nini bwana" imekuwa ikisikika sana vinywani mwao. Sasa sijui hutoa kauli za namna hiyo kwasababu ya kukosa, kuumizwa au kiukweli kutoka rohoni. Na wakishazalishwa watoto pengine zaidi ya mmoja utasikia wanatafuta mwanaume aliye BORA wakililia upweke.

Kilichonifanya niandike huu uzi ni case ya Snura ambayo iko kwenye gazeti la jana la Risasi. Nimeimbatanisha na uzi huu. Hili tatizo ni la Snura lakini naamini kwamba mawazo yake yanawakilisha wanawake walio wengi ambao wako kweny hali aliyo nayo. Swali ni je wanawake huwa wanajua kwamba haya matamko ni ya ujana? Je wanajua consequnces ya kuwa single mother pamoja na kwamba utakuwa unajiweza kiuchumi? Nimeleta hii labda inaweza kubadili mitizamo ya mabinti wengi wanaodanganywa na wakati bila kuona mbele wanapokwenda.

Unaweza kuwa na mawazo ya kutoolewa. Swali je hutakuwa na mwanaume wa kukutimizia haja zako? Kama unamhitaji utapandwa na wangapi? Maana itafika wakati kila mwanaume anayetaka anakuja kwako kama kipozeo.

Nimeiweka humu kwa maoni yenu wana jf ili isaide kupanua mawazo jinsi mahusiano tunavyoyachukulia.karibuni.
1480243274256.jpg
 
ujumbe mzuri shida iyo ya Snura haisomeki ungekopi tu ukaandika hapa maandishi madogo mno ukizum ndio hayasomeki kabisa
 
ujumbe mzuri shida iyo ya Snura haisomeki ungekopi tu ukaandika hapa maandishi madogo mno ukizum ndio hayasomeki kabisa
Tatizo niliipiga picha. Iko kwenye gazeti. Labda nitaongeza mwanga ili ionekane vizuri.
 
Wewe umejuaje kama wanajidanganya?

Kuna ubaya mtu akichagua kuishi maisha fulani kwa wakati fulani?
Nimeshuhudia wengi wakisema hawataolewa lakini baade huja kugundua walidanganywa na umri. Sasa unataka kuolewa una watoto wawili tayari unafikiri ni wanaume wangapi wanakubali hilo?
 
ujumbe mzuri shida iyo ya Snura haisomeki ungekopi tu ukaandika hapa maandishi madogo mno ukizum ndio hayasomeki kabisa
Snura anasema anatafuta mume hana muda wa kuongeza mtt tena watt wawili alionao wanatosha....upweke unamsumbua
 
Wanawake wanafikiria Kwa asilimia kubwa kutokana na hca zao za mda ,mazingira na nyakat huchelewa kujua usahihi wa maisha mapema
 
Nimeshuhudia wengi wakisema hawataolewa lakini baade huja kugundua walidanganywa na umri. Sasa unataka kuolewa una watoto wawili tayari unafikiri ni wanaume wangapi wanakubali hilo?
Kuna ubaya gani leo mtu akawa hataki kuolewa na kesho akataka kuolewa? Wewe huwa hubadilishi misimamo na mitazamo katika maisha yako?

Na hao wadada unaodai 'umeshuhudia' walikufata wakakwambia walidanganyika na umri?

Halafu usiwasemee wanaume wengine, jisemee wewe.
 
Nimewaona wakihangaika kutafuta wanaume, kama Snura huoni anasema mwenyewe. Samahani kama na wewe ni mhanga wa hii hali maana inaweza isikupendeze. Wanaume wengi hawapendi wakuooe tayari una watoto wawili. Siyo mimi tu. Uliza humu ndani utapata jibu kama unafikiri ni mawazo yangu tu.
 
Kuna ubaya gani leo mtu akawa hataki kuolewa na kesho akataka kuolewa? Wewe huwa hubadilishi misimamo na mitazamo katika maisha yako?

Na hao wadada unaodai 'umeshuhudia' walikufata wakakwambia walidanganyika na umri?

Halafu usiwasemee wanaume wengine, jisemee wewe.
wewe unapenda uolewe?
 
Back
Top Bottom