gwahe
Senior Member
- Nov 24, 2014
- 147
- 84
Wanaume tuwe na huruma na wasichana wadogo.Jamaa yangu mmoja amenipatia stori moja, ukweli nimesikitika ingawa inaweza kutufunua macho, kutufundisha na kutubadili tabia.
Jamaa na miaka 34-38 na pia ana mke na watoto watatu. Basi siku moja msichana mmoja alikosea namba ya simu na kumtumia vocha ya 500 tu. Baadaye huyo msichana aliamua kupiga simu na kumwomba jamaa amrudishie hiyo vocha. Jamaa alimwuuliza binti, anafanya nini na mbona pesa kidogo sana anayoomba arudishiwe.
Msichana akasema anasoma form two. Basi jamaa akaamua kumrudishia vocha ya 5000 badala ya 500.
Msichana kuona 5000 kesho yake, chatting zikaanza na baadaye mambo ya kimapenzi yakatawala na msichana akawa anamwita jamaa my uncle. Basi wakakubaliana siku moja kukutana.
Siku ya kukutana jamaa alikwenda anaendesha gari yake aina ya NOAH mpk check point. Msichana alisimama sehemu akimsubiri my uncle. Msichana baada ya kuona uncle na umbile lake huku akimpigia simu. Msichana akaamua kuondoka huku akifikiria mambo mawili. Jamaaa kama Baba yake na pia kwa nini amekuja na gari aina ya NOAH.
Baada ya kuondoka msichana ikambidi amweleze uncle ukweli kwa nini aliamua kuondoka, kumbe jamaa naye alimwona yule binti, akawa anafikiri kama kweli ni ndiye yeye maana alikuwa mdogo sana.
Tafakari.