Wasichana Dar wauzwa Kongo

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
683
124
Wasichana Dar wauzwa Kongo

*Wachukuliwa mikoani kama wafanyakazi wa ndani
*Wafikia kwenye majumba Masaki, Kunduchi, Z'bar

Na Rashid Mkwinda, Tunduma

BIASHARA haramu ya kuuza binadamu nchi za nje imezuka sehemu mbalimbali mpakani mwa Tanzania na nchi jirani, kwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 13 na 14. Wasichana hao wamekuwa wakikusanywa na kusafirishwa katika nchi hizo ambako hulazimishwa kupigwa picha za uchi na kufanya biashara ya ngono.

Kwa mujibu wa taarifa za siri zilizotolewa na wasichana watatu waliozungumza na gazeti hili mjini hapa juzi, walichukuliwa nchini na kusafirishwa hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mji wa Lubumbashi ambako awali waliambiwa wanakwenda kufanya kazi za ndani. Wasichana hao, Paulina Samwel (14), Happiness Jonathan (14) na Zuhura Majige (15), walidai kuwa walichukuliwa Mbeya Agosti 29 mwaka huu na mwanamke waliyemtaja kwa jina (linahifadhiwa) ambaye alidai anahitaji watu wa kufanya kazi za nyumbani kwake, Dar es Salaam.

Waliendelea kudai kuwa walichukuliwa na mwanamke huyo hadi nyumba moja Mbezi Beach ambako waliwakuta wasichana wa rika lao wasiopungua 55 kutoka mikoa mbalimbali ya Bara wakiwa wamefungiwa ndani na kupewa mahitaji yote muhimu ikiwa ni pamoja na chakula kizuri, mafuta mazuri ya kulainisha ngozi na nguo za kubadilisha.

"Walikuwa wakituhamisha kutoka jumba moja hadi jingine…kuna majumba matano sehemu za Mbagala, Mikocheni B, karibu na Kanisa la Assemblies of God, Masaki, Kunduchi, Mbezi Beach na Unguja karibu na soko la samaki," alidai Paulina. Walidai kuwa pamoja nao walikuwapo wanawake wenye umri mkubwa sawa na mama zao, ambao walikuwa wakiwafundisha mambo ya ngono, huku wakitumia muda mrefu kuangalia picha za ngono kupitia mikanda ya Video na kwamba usiku walichukuliwa baadhi ya wasichana na kurejeshwa alfajiri.

"Huko tunakutanishwa na wanaume ambao tunafanya nao vitendo vya ngono kwa malipo, ambayo huchukuliwa na wanawake hao na siku nyingine huchukuliwa wasichana wengine kwa ajili ya kupelekwa katika majumba ya starehe na kurejeshwa alfajiri na gari maalumu lenye vioo vya giza," alidai Happiness. Waliendelea kudai kuwa wasichana wengi wanatoka Mbeya, Kigoma, Morogoro, Shinyanga na wilaya za Kisii na Kakamega, Kenya na kwamba Oktoba 12 mwaka huu, wasichana 17 wakiwamo wao, walichukuliwa na kusafirishwa kwa njia ya magari makubwa hadi DRC.

Walidai kuwa siku moja kabla ya kuanza safari, waliletewa hati za kusafiria zikiwa na picha ambazo walipigwa siku waliyofika na kwamba kila mmoja anapofika katika jumba hilo, hupigwa picha nne za pasipoti kwa kutumia kamera ndogo ya 'Digital'.

"Tulichukuliwa ndani ya malori yanayosafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam na kila lori tulipanda wasichana watatu…yalikuwa malori yapatayo sita. Kiongozi wetu ambaye alikuwa ni mama wa makamo, alipanda lori la mbele," alidai Zuhura. Aliongeza kusema walipitia katika njia ya mpaka wa Tunduma na kwa siku nne waliingia Lubumbashi na kupelekwa moja kwa moja katika jumba la kifahari ambako waliwakuta wasichana wenye umri kama wao kutoka sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki, wakiwamo wa kitanzania, ambao walifahamiana kutokana na Kiswahili.

Wakiwa katika jumba hilo, walidai walishangaa kuona makundi ya watu kutoka mataifa mbalimbali ambao wakidaiwa kutoka Paris, Ufaransa na Arabuni ambao walifanya mazungumzo na wenyeji wao na baadaye kuchaguliwa baadhi yao na kisha kuondoka nao.

Walidai kuwa utaratibu huo ni wa kila wiki na kila siku makundi ya wasichana walikuwa wanaletwa katika jumba hilo. "Hali hii ilianza kututia hofu mimi na wenzangu, tukatafuta mbinu za kutoroka…tukaondoka alfajiri ndani ya jumba hilo na kufika katika mtaa mmoja, tukakutana na mama akiwa anatoka msikitini, tukamwomba atusaidie baada ya kumweleza matatizo yetu," alidai Zuhura.

Aliongeza kuwa mama huyo aliyemtaja kwa jina (linahifadhiwa) aliwachukua hadi nyumbani kwake na kuwauliza jinsi walivyofika humo na kuwatahadharisha, kuwa watu wale hufanya biashara za kuuza wasichana Ulaya na Arabuni, hivyo walikuwa wamejiingiza katika matatizo.

Alidai kuwa mama huyo aliwatafutia usafiri wa kurudi nchini kupitia magari makubwa yanayofika Tanzania na kuingia kupitia mpaka wa Tanzania na Zambia kitongoji cha Tunduma Novemba 15 mwaka huu. Walipoulizwa sababu za kudanganyika hadi kufika huko, wasichana hao walidai kuwa wao wanatoka katika familia duni na kwamba mara baada ya kumaliza shule ya msingi na kushindwa kuendelea na masomo, waliamua kutafuta kazi yoyote ya kufanya na kwamba kazi pekee waliyoiona ni kufanya kazi za uyaya.

"Mimi naishi na bibi yangu Mbozi, mama yangu alifariki dunia siku nyingi, niliposikia kuna mtu anatafuta msichana wa kazi, nilifurahi na hasa niliposikia kuwa ninakwenda Dar es Salaam, kwani sikuwahi kufika hata siku moja nikajiona mwenye bahati kufika Dar es Salaam, lakini yaliyonikuta siwezi hata kusimulia," alisema Paulina kwa uchungu.

Mmoja wa watoa taarifa hizi ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini alidai kuwa biashara hiyo ni maarufu nchini katika sehemu za mipaka ya nchi za Kasumulu mpakani mwa Malawi, Kigoma, Holili na bandari ya Isaka Kahama na kueleza (bila kufafanua) kwamba biashara hiyo inahusisha watu wakubwaDuuh wazee hii sio issue ndogo jamani ni soo.
 
This is rediculous, Kikwete open your eyes and ears.Ministry of Women and children should also do something about this. We can't keep quiet and let this happen to the young generation,its too dangerous!!!
 
Kwa kweli kwa mtindo huu tunarudi tulikotoka, yaani enzi ya biashara ya utumwa. yote hayo ni matokeo ya hali ngumu ya maisha mtu mzima anabuni biashara haramu kiasi hicho, wizara husika watafuteni watoto hawa waliotoa taarifa hizi kisha fuatilieni. Usalama wa Taifa mpo?????????
 
Kwa kweli kwa mtindo huu tunarudi tulikotoka, yaani enzi ya biashara ya utumwa. yote hayo ni matokeo ya hali ngumu ya maisha mtu mzima anabuni biashara haramu kiasi hicho, wizara husika watafuteni watoto hawa waliotoa taarifa hizi kisha fuatilieni. Usalama wa Taifa mpo?????????

Mkuu hii ni hatari sana na nadhani wakubwa nao wanasoma haya magazeti lakini hamna hatua itakayochukuliwa kwa hawa wakina mama. Hii ni mbaya sana wazee.
 
Kwa wanaolipwa na system kuchunguza kinachoendelea JF pelekeni hili basi kwa mabosi wenu na muwambie tunasisitiza hatua za haraka zichukuliwe, labda hata magazeti hawasomi, hii ni hatari sana. msiwe mnatoa macho kwenye siasa tu huku tunapoteza kizazi hiki.Nachoshangaa ministries kibao sijui kazi yao ni ipi, utaona wametulia kama hawaoni wala kusikia, hii mbaya sana na inatia uchungu.
 
Kweli hapa utumwa umerudi. Mbaya zaidi ni pale utakuta viongozi wanahusika katika biashara hii haramu. Hapo ni nani atawanusu hawa watoto wasio na hatia?
 
..nimekumbuka ule msemo wa watu weupe wa ulaya..."the dark continent!"

..sehemu yeyote yenye dhiki mambo kama haya huwa kawaida!eastern europe,asia na africa ndio inapamba moto sasa!

..moral decay nayo huchangia!laana tupu!

..tatizo ni kama hao watoto si wako!...unawasahau mara baada ya kufunika gazeti!
 
..nimekumbuka ule msemo wa watu weupe wa ulaya..."the dark continent!"

..sehemu yeyote yenye dhiki mambo kama haya huwa kawaida!eastern europe,asia na africa ndio inapamba moto sasa!

..moral decay nayo huchangia!laana tupu!

..tatizo ni kama hao watoto si wako!...unawasahau mara baada ya kufunika gazeti!MKUU,Hapo nimeguswa.
Lakini nauliza hivi,mbona mambo yasiyo ya msingi yanafatiliwa mno!?Hili je
Tafadhali wahusika je hili HALIFAI KUUNDIWA TUME?
 
[/B][/COLOR]


MKUU,Hapo nimeguswa.
Lakini nauliza hivi,mbona mambo yasiyo ya msingi yanafatiliwa mno!?Hili je
Tafadhali wahusika je hili HALIFAI KUUNDIWA TUME?

Mkuu unajua huwa issue ambazo haziko serious ndio zinafuatiliwa lakini issue serious kama hizi watu wanapiga kimya. Jamaa hapo juu amenigusa sana na kusema MTOTO KAMA SIO WAKO UKISOMA GAZETI UKIMALIZA UMESAHAU. Hii inauma sana, zamani mtoto alikuwa ni wa jamii nzima lakini siku hizi sio tena. Utu wa watu umekwisha kabisa.
 
Nimesoma taarifa kwa kina. nimesoma maoni kwa mapana. wananchi wote ni macho ya serikali. ingawa serikali ya Vasco da Gama ina mawaziri lukiki bado hawaoni na sijui kama wanawajibika ipasavyo. we need to kick their bacside. Kwanzan taarifa hizi ni kutisha and I believe kuwa zipo. sasa basi haitoshi kuandika magazetini tu. Thats why vyombo vya habari Tanzania havina mwelekeo. habari kama hizo pamoja na kuchapisha still waltakiwa kupeleka full details Police na waandike jina ofisa aliyepokea taarifa hizo na wampe Ultimatum kuwa watarudi kumuona awape taarifa kamili. Si suala la usalam wa Taifa tu. Hapo ni kamanda mwema na vijana wake. RPCs wanashughulika na nini? Je hao mabinti walishauriwa kwenda Police? Je Mipkani Uhamiaji wapoona hali kama hiyo wot are they doing? Je passport walipate bila kuchukuliwa alama za vidole? Au walisafiri bila pasi? na kama ni hivyo je Uhamiaji Tunduma wana details za majina ya mabinti wa umri mdogo kupita mpakani hapo? tuanzie hapo, Customes wana details za magari yanayopita kila siku kuingia ama kutoka. na as I know hawa mabinti je hawaandiki usafiri wanaotumia? maana kuanzia hapo police Itawabana madereva wapi waliwashusha hao mabinti. Hapa Huhitaji skiills za Interpol kuweza kubaini ukweli na njia chafu za hao mafisadi wa uhai wa binadamu.

Salaam kwa Vasco da Gama hiyo ndiyo kasi mpya na ari mpya ya watu kuwa na kasi mpya ya umaskini mpaka kurubuniwa kuingia katika biashara haramu?

second part ni kuhakikisha kuwa kuna sheria na utaratibu unaofuatwa kuwaajiri mayaya. wizara husika inabidi kuandaa utaratibu mahsussi kwa wajiri na wajairiwa. Kila anayeishi na mfanyakazi wa ndani inabidi taarifa ziwe katika vyombo husika ili kuweza kuwaprotect hawa kwani it easy kuwa abused. si mnakumbuka kesi ya Kamanda Mahita? there are thousands of hidden Mahitas. Also waajiri watakuwa aprotected na mayaya wwezi pale wanapoamua kutimka na vitu vya mwajiri. Sheria na taratibu zikianzia hapo nadhani hata kuuzwa hao mabinti kutapungua. All in all its a responsibility of government kuwalinda wananchi. wanauza mashirika, ardhi na vito vyake sasa wana wa nchi nao wanauzwa! Hatari.
 
Mnajua wateja wa hii biashara ni akina nani?

Tulia kisha tafakari......

Mkuu FD, Nimejaribu kutulia na kutafakari, lakini sipati jibu. au kwamba wateja ni vigogo wetu? maana kuna mahali inaelezwa kwamba walipokuwa Dsm walikuwa wakichukuliwa usiku kwenda kufanya vitendo vya ngono na malipo walipewa watekaji. lakini na huko Kongo Je?

Tumedharauliwa kiasi cha kutosha na kunyanyaswa kiasi cha kutosha kwenye ardhi yetu, kwenye mashamba yetu, kwenye madini yetu, kwenye mabenki yetu, kwenye viwanda vyetu na sasa mpaka kwenye miili yetu wenyewe. "Umasikini na ndege inayopaa"
 
These people should be investigated and if possible criminal charges should be laid against them.
 
nimesoma taarifa hii kwa masikitiko makubwa sana.

hali duni ya maisha na tamaa ya kuwa na maisha bora mara nyingi hupelekea kufikia hali hii.


hili si suala ambalo ni Tanzania pekee inakumbana nalo ni karibu nchi nyingi maskini au jamii maskini wanakumbana nalo, huko ulya kuna majumba wako watu wa n chi zote wahindi, warusi, waafrika, waarabu wakifanyishwa hizo kazi za ngono.


na wengi wao walipelekwa huko wakiwa na umri mdogo,

vita, migogoro ya kisiasa ambayo hupelekea uvunjifu wa amani pia ni sehemu ya sababu hizo.

mtandao huu ni mpana na watendaji au wanaofanya kazi ya kuwarubuni hawa watoto umetapakaa dunia nzima na nguvu zake unafanana na wa madawa ya kulevya.

hapa tumeonesha kukerwa na ngono tu, watoto huibiwa na kulaghaiwa na kufanyishwa kazi nyingi tu za htari, ikiwemo kwenye madawa ya kulevya, kwenye migodi, mabaa, vitani na sehemu nyingi za hatari.


ushauri wangu ss Tanzania kama taifa ambalo linapenda watu wake, tunapaswa kuchukua hatua na kufuatilia kwa makini hii taarifa, nnasema Tanzania nikimaanisha sote, sipendi kusema hili ni suala la serikali peke yake.

serikali itekeleze kilichomo mikononi mwake mfano kuhakikisha mipakani kuko makini , passport hazipatikani kizembe kwa wenye nia mbaya, usalama wa taifa kushuglikia vilivyo hii taarifa na kuwaganda watuhumiwa kujua ukweli.

waandishi kufichua zaidi taarifa hizi, kuielewesha jamii ubaya wa hii biashara na yanayoendelea.

wananchi kujitahidi kuelimishna na kusaidiana kupata miongozo sahihi ya kazi gani tunayotaka kuifanya na kuhabarishana juu ya dhamira za atu hao.

wazee kulea watoto wetu vyema n kuwafatilia na kuwatunza na kutowaruhusu kuwatoa kwa watu tusiowafahamu vyema. imekuwa rahisi ukitaka mfanyakazi wa ndani kwenda bara na kupewa na mzee wala hajui mtoto wake yuko wapi na anaishi vipi, hii aibu kwa wazee.

kule kwetu zanzibar tunao wengi hawa bahati nzuri wengi hufanya kazi za ndani, utamuona mtoto mdogo maskini ana miaka 12 au kumi nanne unaletewa tena si na mzzi wake na atfanya kazi hapo muda wote bila ya wazee wake kuja kumtembelea au kumuulizia inatilisha huruma.

hii ndio wengine hupelekea kumuonea na kumdhalilisha maana tayari nyie wenyewe humumtaki.

nnazungumza kwa uchungu maana hili tatizo linaniuma kama mzazi na hili lipo hta humu humu ndani kabla ya hata kuangalia nje sote tujithidini kutekeleza ubinaadamu wetu kwa binaadamu wenzetu.
 
Ndugu Maarifa, nakushuruku sana kwa mchango wako, lakini kabla ya kuzungumzia masuala ya mikapa nakuomba uelewe nchi zetu hasa Tanzania,Kenya,Uganda,Kongo, Zambia na zingine ambazo sikuzitaja hazina utaratibu mzuri katika kuthibiti mipaka.maana unaweza kushuka kwenye gari na kwenda upande wa pili kama makazi wa eneo hilo bila polisi wala uhamiaji kukuuuliza kitu. Hivyo hata kama utafuatilia ofisi za uhamiaji zilizopo Tunduma hutapata taarifa zozote zinazo uhusiana wa wasichana hao.nina kueleza haya kwasababu nilikuwa ofisa mkubwa wa idara moja kwenye mpka wetu na kenya, kutokana na ujirani mwema watu toka pande hizi mbili tulikuwa tuna kwenda bila hata kuulizwa hati yeyote.Ukijaribu kuuuliza kwanini hakuna umakini kwenye mipaka yetu utaelezwa tunazingatia ujirani mwema lakini siku zijazo tutakuja kupata msiba mkubwa kutokana na serikali kutoweka watu makini kwenye mipaka yetu kwa ujumla.
 
Duh! Yaani nasikia uchungu wa hali ya juu! Kuna mafisadi wana majumba ya gharama kubwa huko Masaki, Mbezi Beach na kwingineko kumbe kazi yao ni kuuza Watanzania wenzetu nchi za nje. Natamani kulia :(
 
Mkuu FD, Nimejaribu kutulia na kutafakari, lakini sipati jibu. au kwamba wateja ni vigogo wetu? maana kuna mahali inaelezwa kwamba walipokuwa Dsm walikuwa wakichukuliwa usiku kwenda kufanya vitendo vya ngono na malipo walipewa watekaji. lakini na huko Kongo Je?

Tumedharauliwa kiasi cha kutosha na kunyanyaswa kiasi cha kutosha kwenye ardhi yetu, kwenye mashamba yetu, kwenye madini yetu, kwenye mabenki yetu, kwenye viwanda vyetu na sasa mpaka kwenye miili yetu wenyewe. "Umasikini na ndege inayopaa"

Good Guess!, Sasa unaweka kuzuia bidhaa "hadimu" unayoipenda?
 
This is very sad and disturbing story. Actual jana nilikuwa naongea na binti mmoja yuko Tanzania, nae akaniambia ana house gal wa miaka 14. Nikauliza 14 years old nadhani anastaili kuwa form I, akanijibu kwamba ndio, tena huyu wangu kafaulu, lakini shule akienda mwisho wake atapata mimba na kupoteza pesa za wazazi, bora aje hapa afanye kazi kisha atapata mtaji. Kusema kweli jibu hili lilinikata maini, hasa ikizingatiwa limetolewa na mwanamke.

Serikali can't help kama wananchi individual hawata simama na kupinga swala hili, magazeti ya Tanzania yanapaswa kuacha huu ushenzi wa kuwaficha hawa wahaini kwa kutokuwaandika majina yao bayana. Hii ni new slave trade, na inafanyika kwa wingi sana nchi za asia, madhara yake ni UKIMWI, kuwa na taifa linlodhalilisha wanawake, madhara ya kisaikologia, na mengineyo mengi. Ni lini Watanzania tutasema enough is enough?

Inajulikana bayana kabisa serikali yetu ni jina, na imeshakufa tangu mwanzoni mwa miaka ya 90. Ni jukumu la kila mwananchi kupambana na haya maswala ya udhalilishaji wa wanawake, ni jukumu la kila mwananchi kuelimisha jamii ni nini umuhimu wa kupata elimu kwa usawa.

Naamini kabisa, one person can make changes, Stop ajira kwa watoto, elimisha jamii kuhusu umuhimu wa Mwanamke. Kina baba na kina kaka tuache kuabuse wanawake na kuwafanya second citizen.
 
.....Kusema kweli jibu hili lilinikata maini, hasa ikizingatiwa limetolewa na mwanamke.

Inajulikana bayana kabisa serikali yetu ni jina, na imeshakufa tangu mwanzoni mwa miaka ya 90. Ni jukumu la kila mwananchi kupambana na haya maswala ya udhalilishaji wa wanawake, ni jukumu la kila mwananchi kuelimisha jamii ni nini umuhimu wa kupata elimu kwa usawa.

Naamini kabisa, one person can make changes, Stop ajira kwa watoto, elimisha jamii kuhusu umuhimu wa Mwanamke. Kina baba na kina kaka tuache kua-buse wanawake na kuwafanya second citizen.

Mtanganyika,

Nakuunga mkono katika maandishi yako yote isipokuwa mstari wa Bluu. Serikali ipo hai tena iko makini. Labda kama maana ya Serikali imebadilika!

Watanzania tulipigie kelele suala hili. Nakumbuka wakati nimempata binti mmoja wa kazi nikamwuliza ana elimu gani akasema kaishia Form II nikaamua kumpeleka shule na kumwachisha kazi nilionekana chizi sana. Huyu hakupenda kuwa alivyokuwa isipokuwa mambo yalikwama ajili ya karo. Nilimwitaji afanye kazi lakini kwa kuona umuhimu wa kusoma nilimpeleka shule. Kibao kiligeuzwa kwangu na mwanamke mwenzie akisema "Huyu utakuwa unamtaka ndiyo maana ukampeleka shule ili uweze kumpata kirahisi".

Watu wana fikra mbaya mbaya tu. Mtoto wa kike anatakiwa kuelimishwa jama!
 
Na huyo Waziri wao yuko wapi. Kwani yeye hajui hili? au ndio Buzwagi yake. There are very few women who think sex business is a problem. After all most of them do it for money. To them it is a commmon thing. Mwekeni dume hapo ,angalau atajali kidogo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom