Washindi wa Kilimanjaro Marathon kuzawadiwa viwanja kutoka Lapex Properties

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Lapex Properties imetangaza kuwazawadia viwanja mshindi wa kiume na wa kike wa mbio za kilometa 42 za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2024.

Zawadi hizi zinatolewa kwa kushirikiana na mdhamini Mkuu wa Mbio za Km 42- Kilimanjaro Premium Lager na waandaaji wa mbio hizi.

Tangazo hili linakuja takriban wiki mbili kabla ya mbio hizo maarufu na ambazo huvutia washiriki zaidi ya 11,000 na idadi kama hiyo ya mashabiki kutoka nchi zadi ya 56 Duniani.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Lapex Properties, Thom Mukondya alisema kama wataalamu na washauri wameamua kutoa zawadi hizo kutokana na ukubwa wa mbio hizo na umaarufu wake ambao utawasaidia kutangaza shughuli zao kwa umma.

“Tunaamini Kilimanjaro Marathon inawavutia vijana wengi kushiriki na tunatamani wamiliki ardhi bila kuingia kwenye migogoro,” alibainisha na kuongeza kuwa vijana wengi wanaingia katika migogoro kwa kushindwa kupata ushauri wa kitaalamu pale wanaponunua viwanja au nyumba.

WhatsApp Image 2024-02-12 at 13.04.54_372e2441.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Lapex Properties, Thom Mukondya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo kuwazawadia viwanja washindi wa Kitanzania wa Kilimanjaro Premium Lager International Marathon km 42. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Lapex Properties, Shakila Hante na Meneja Matukio wa Kilimanjaro Marathon, David Marealle.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, viwanja wanavyotoa ni square mita 500 na vipo Kimbiji, Kigamboni ambapo kila kimoja kina thamani ya milioni 6.

“Viwanja hivi tunatoa kwa mshindi wa mbio za km 42 na tutawakabidhi hati baada ya waandaaji kuthibitisha washindi,” aliweka bayana.

Lapex Properties pia itashiriki katika maonesho maalumu ya siku nne yanayojulikana kama ‘People’s Expo’ yatakayofanyika katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU) kuanzia Februari 22 hadi 25, 2024 ambapo makampuni mbalimbali na mashirika yataonesha huduma na bidhaa zao kabla ya mbio hizo kufanyika Februari 25 Mjini Moshi. “Tutakuwepo kutoa elimu kuhusu taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa kabla ya kununua viwanja, alieleza.

Shughuli nyingine za Lapex Properties ni pamoja na kupima viwanja, ushauri na elimu kuhusu ardhi, kununua na kuuza viwanja na mashamba, uwakala wa kufuatilia masuala ya hati, na uchunguzi wa eneo.

Naye mwakilishi wa waandaaji wa mbio hizo, David Marealle aliipongeza Lapex Properties Kwa hatua hiyo ambayo itsongeza hamasa Kwa watanzania kufanya vizuri zaidi ili wajishindie viwanja.

"Sisi kama waandaaji na Kwa niaba ya mdhamini Mkuu, Kilimanjaro Premium Lager tunawapongeza sana Kwa hatua hii," alisema.
 
Back
Top Bottom