Washarika wamkataa Sitta kanisani

Washarika wamkataa Sitta kanisani

Kutokana na habari za kuaminika nilizozipata ni kuwa Sitta ameshindwa kuhudhuria ibada katika usharika wake tangu bunge la katiba la ccm limalizike. Hata hivyo, kutokana na chanzo changu cha habari ni kuwa, washarika wamemtuma mchungaji ampelekee ujumbe Sitta kuwa kutokana na vitendo vyake vya kudharau viongozi wa kanisa, Sitta hatakiwi aonekane hapo kanisani

Nimeongea na mchungaji wa ushirika anasema SIO KWELI NI PROPAGANDA ZA KISIASA HIZO. Kanisa haliwezi kuzuia mkristo kusali.
 
Unanikumbusha viboko vilivyotembezwa pale msikitini korogwe ili kuwaondoa mamuruki. Sijui ilikuwaje Mungu akaruhusu bakora kuingia msikitini!

Mkuu unadhani wengine wanajua wanachochangia......jibu murua kabisa lazima aiende kunywa kahawa na kashata afikirie jinsi ya kuja upya.
 
huyu sitta hafai kabisa labda aanzishe kanisa lake na mke wake labda

Mkuu hata aanzishe lakwake lazima awasaliti waumini hasa akiona bakuli la sadaka lime nona!
 
Wakihongwa kiasi kinachozidi kidogo tu ile posho ya wajumbe wa bunge la sisiem, watamkubali
Mkuu, tena hawezi honga waamini wote, atakachofanya ni kumhonga huyo waliyemtuma tu basi mambo yakaisha kwani kwenye BMK si walikuwemo wa aina hiyo?
 
Propaganda za kitoto za kikundi cha UKAWA zinafurahisha sana.

Kama ndivyo hivyo, basi hilo litakuwa siyo Kanisa la Mwenyezi Mungu bali ni club tu kama vilabu vya mambo ya kidunia.

Msingi mkuu wa kanisa la Mungu umesimama katika sababu za ujio wa Kristo Yesu kama ilivyoandikwa ndani ya Biblia. Maneno hayo yanasema,

Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi (1 Timothy 1:15)
Kama kanisa halitaki mwenye dhambi basi hilo litakuwa siyo kanisa la Mwenyezi Mungu.
 
Kumkataa pekeee haitoshi ilifaa afukuzwe na kutengwa kabisa, inawezekanaje ashiriki na wapuuzi nayeye akijifanya sio mpuuzi. Aaachane na wapuuzi na aendelee na welevu wake hukohuko dodoma.

kanisa ni kwaajili ya wenye dhambi siyo watakatifu kama sits anadhambi ndio wakati muafaka wa kurudi kwa mungu na kutubu madhambi take.
 
Kutokana na habari za kuaminika nilizozipata ni kuwa Sitta ameshindwa kuhudhuria ibada katika usharika wake tangu bunge la katiba la ccm limalizike. Hata hivyo, kutokana na chanzo changu cha habari ni kuwa, washarika wamemtuma mchungaji ampelekee ujumbe Sitta kuwa kutokana na vitendo vyake vya kudharau viongozi wa kanisa, Sitta hatakiwi aonekane hapo kanisani
anasali wapi siku hizi? au amebadili dini?
 
Propaganda za kitoto za kikundi cha UKAWA zinafurahisha sana.

Kama ndivyo hivyo, basi hilo litakuwa siyo Kanisa la Mwenyezi Mungu bali ni club tu kama vilabu vya mambo ya kidunia.

Msingi mkuu wa kanisa la Mungu umesimama katika sababu za ujio wa Kristo Yesu kama ilivyoandikwa ndani ya Biblia. Maneno hayo yanasema,

Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi (1 Timothy 1:15)
Kama kanisa halitaki mwenye dhambi basi hilo litakuwa siyo kanisa la Mwenyezi Mungu.
sasa basi mwambie mume wenyu SIX ahudhurie kanisani ili aongee na maaskofu wake wapuuzi na atubie
 
Tunaongelea mambo ya chizi S. Sita, washirika anawaita wapuuzi, si atafute washirika wake anaoona sio wapuuzi. huyo ni kirusi katika kanisa la mungu na nigugu katika ngano yafaa angólewe na kuchomwa moto
hao sio wafuasi wa Mungu tunayemwabudu bali wamegeuza kanisa kama mali binafsi.Mungu anasema anayehukumu naye atahukumiwa kwa kipimo kile kile siku ya mwisho, so jinsi unavyomwombea mabaya yule uliyemuhukumu tayari ndivyo Mungu anavyozidisha hasira zake juu yako.alituasa kuwa kazi ya kutenga magugu na ngano safi itakuwa yake siku ya mwisho na ndio maana wengine huwa mnaenda kanisani kusali mkiwa mmetoka kuzini au hata kuua.au unadhani kuwa dhambi yako umetenda sirini basi wewe una haki kuliko yule aliyetenda kadamnasini???waambie hao washarika kuwa kama kweli wameshafanya hivyo basi ni dhahiri kuwa wameshamkaribisha shetani ndani ya hekalu ya Mungu na atawatumikisha apendavyo hadi umauti wao akiwasubiria katika makazi yake ya mateso ya milele.Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kama wafuasi wa Yesu tunatakiwa kumwombea na kuacha Mungu atende iliyo haki.
 
Ana wake kila kona halafu anasema ni mkristo , kama sio unafiki ni kitu gani? Mfukuzeni kabisa akija kanisani anakuja kutia nuksi!!

Ebu nenda taratibu mbona padri fukuzwa Slaa ana wanawake kibao hamjataka afukuzwe kanisani? Vipi na mwenyekiti wa Chadema Freeman mbowe na mukya mlishawafukuza kanisani? Wao ni watakatifu?
 
kutokana na habari za kuaminika nilizozipata ni kuwa sitta ameshindwa kuhudhuria ibada katika usharika wake tangu bunge la katiba la ccm limalizike. Hata hivyo, kutokana na chanzo changu cha habari ni kuwa, washarika wamemtuma mchungaji ampelekee ujumbe sitta kuwa kutokana na vitendo vyake vya kudharau viongozi wa kanisa, sitta hatakiwi aonekane hapo kanisani

yaelekea usharika uliyumba kwa kukosa sadaka yake
 
Kwani hilo kanisa ni la washarika au la mwenyezi Mungu? Mimi nilifikiri ni kama misikiti ambayo inakuwa ni ya mwenyezi Mungu ambamo kila mwislamu aweza sali.Wagalatia mna mambo.

Sitta ni muumini wa dhehebu la kiLutheri, na taratibu za waLutheri ni kuwa..unakuwa 'msharika' wa usharika Fulani. Kutokuwa msharika hakukuzuii kwenda kuabudu katika usharika husika. Kuna privileges unapata toka usharikani kwako kwa kuwa msharika, na unapokuwa msharika..kuna wajibu pia unakuwa nao kwa usharika wako, hasa maendeleo ya usharika wako na vitongoji vinavyosimamiwa na usharika wako. Kuna taratibu za kumvua msharika 'usharika' wake. Kwa hili la Sitta sijui kama kuna hoja ya kuweza mvua usharika...ila kama washarika wenzako wanakuona wewe si mwenzao, ni udhahifu kwa mtu mwenye hadhi ya Sitta. Kanisa ni la Mungu..si la washarika, lakini usharika ni wa washarika.
 
Back
Top Bottom