Wasanii wa siku hizi hawapo jukwaani

Wasanii wa siku hizi hawapo jukwaani

Swet-R

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
5,623
Reaction score
8,141
Siku hizi mziki vijana kama hawafaidi kabisa. Tofauti na zamani miaka ya 2000's tunaenda disco, mnaburudika mwanzo, mwisho. Mnacheza kweli unarudi home umeburudika vya kutosha. Naangalia fiesta Yaani msanii yuko jukwaani inatakiwa aimbe.

Lakini ajabu unapigwa wimbo wake kidogo, msanii utasikia anawaambia watu, wote mikono juu, mara mikono hivi kama mkasi, twende twende twende. Ruka ruka ruka. Sema yeyaaaa, sema wawawwaaaa, sema Wii. Piga miruzi ya kutosha, tuko vizuri. Haya weka mikono hivi, twende, tuko vizuri. Mikono juu wooteeee. Mpaka anatoka jukwaani mtindo ni huo tu.

Anakuja msanii mwingine mambo ni hayo hayo mtindo ni huo huo. Sasa nauliza mashabiki wanaufurahia uimbaji wa msanii au kufurahia kucheza mziki saa ngapi? Mpaka shabiki anaondoka eneo alitoa kiingilio mikono ndio iliyochoka kwa kuipaisha juu, kama anavyotakiwa afanye na msanii. Wasanii wetu wana-FAIL wapi? Kwa nini asipande jukwaani akagonga nyimbo zake sawa sawa, mwanzo mwisho, watu waondoke pale wamesuuzika kabisa moyoni kwa burudani ya jukwaani ya kutosha?

Naona bora uende disco sasa
 
Ni kweli boss hata leo nimeangalia shoo ya Konde youtube ile aliyopiga bure mbagala muda wote ndo hivyo sema yeah yeah,nikisema john sema maguli magufuli mara mikono juu sema konde boy konde boy sa yeah yeah khaaaa nikasema kwakuwa ni shoo ya bure sawa lakini ilikua kupoteza muda[
 
Ni kweli boss hata leo nimeangalia shoo ya Konde youtube ile aliyopiga bure mbagala muda wote ndo hivyo sema yeah yeah,nikisema john sema maguli magufuli mara mikono juu sema konde boy konde boy sa yeah yeah khaaaa nikasema kwakuwa ni shoo ya bure sawa lakini ilikua kupoteza muda
Umeona? Mpaka naona aibu mimi ninaeangalia
 
Yaani,,
Unatoka fiesta jasho mwili mzima
shingo inauma kwa kurukiana kwenye vichwa
Hapo na kiingilio umetoa,,,burudani gani sasa hiyo,
 
Ifike mahali na sie mashabiki tusiwe wajinga,tukiambiwa mikono juu hakuna kupandisha mikono,wakisema cjui everybody say yeah,tunanyamaza kimya,DJ akikata kipande cha mziki ili mashabiki waitikie,tunaitikia kimoyo moyo bila kutoa sauti,..mbona wataimba tu pumbavu zao,,pesa tulipe halaf tukaimbishwe mwanzo mwisho
Umeona? Mpaka naona aibu mimi ninaeangalia
 
Yaani,,
Unatoka fiesta jasho mwili mzima
shingo inauma kwa kurukiana kwenye vichwa
Hapo na kiingilio umetoa,,,burudani gani sasa hiyo,
Yaani naona bora uende disc unafurahia kucheza moyoni unaburudika
 
Ifike mahali na sie mashabiki tusiwe wajinga,tukiambiwa mikono juu hakuna kupandisha mikono,wakisema cjui everybody say yeah,tunanyamaza kimya,DJ akikata kipande cha mziki ili mashabiki waitikie,tunaitikia kimoyo moyo bila kutoa sauti,..mbona wataimba tu pumbavu zao,,pesa tulipe halaf tukaimbishwe mwanzo mwisho
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]... kabisa wangenyooka. Yaani ni mateso I see. Hakuna burudani hapo mkui
 
Yani hao ma-DJ sijui wamekariri wapi kukata kata muziki kila sekunde. Pia tuna safari ndefu sana (thousand light years) kwenye sound engineering.
Ile tuite nini sijui? Maana sio burudani tena
 
Mimi nilidhani wenye tatizo hilo ni wasanii wa kibongo peke yao. Leo nilikuwa naangalia show moja ya Wizkid nikaona swaga ni zile zile.
 
Back
Top Bottom