Jmushi.. najua wewe mwenyewe ni kijana wa kizazi kipya... na hii fani unaiweza sasa onesha mfano. Nikutengenezee beat ya uhakika?
Niliwahi kuanzisha thread hapa kuhusu Mageuzi yaliyotokea nchini Kenya. Nilielezea jinsi kikundi ya Redykyulas ambavyo kiliweza kuwaelimisha wananchi wa Kenya jinsi viongozi waliokuwa madarakani walivyokuwa wakiwasaliti. Na vilevile kuwaelimisha jinsi ya kuweza kuwaajibisha, naamini sisi wenyeywe tulishuhudia ni mawaziri wangapi na wabunge walivyoweza kupoteza nafasi zao. Naamini tukijifunza yale kwa makini na kuingizwa katika usanii, watu watavutiwa na kujifunza zaidi.
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=11172
Si wakati wa kuwaelezea namna ya kuwaelimisha bali ni wakati wa kuwaelimisha.
Utawaeleweshaje husipowapa namna ya kuelewa?? Kuna namna ya ufundishaji Mushi, hata huko shule kindergaten ya Kibongo tulikuwa tuhahesabu vizibo ya soda au vijiti. Hiyo ilikuwa ni namna ya kuelewa hesabu za kujumlisha au kutoa. Namna ya uelewa iko tofauti tofauti inategemea na mwalimu mhusika ndio maana hata katika sanaa kuna nyimbo, ngonjera/ugani, maigizo n.k Njia zote hizo zinaweza kumuelewesha mtu madhui ya ujumbe hata kama ujumbe utakuwa uleule.
Nadhani kama mtu ana nia ni vizuri tukaacha blah blah tukawasaidia hao wasanii
Tuwasaidie nini maana hata kusaidika hawa saidiki.Mpe mashairi then ataboronga tuu.Madj watamfanyia hujuma,wanasiasa wataweka mikono yao humo mwishowe itakuwa comedy show.
Mmhhh, kweli JF ni ya WOTE.
Umeambiwa wanataka mashairi? na hayo wanayoimba ni nini?
Kaazi kweli kweli.
Ndio watanzania sisi.
Jmushi,
Wagosi wa kaya wametoa wimbo mkali sana wa POLE, wamezungumzia yote yanayotokea na hata wamempa POLE JK kwa uchumi Unaokua POLEPOLE (MANENO NDANI YA WIMBO). Wimbo ni mzuri sana na mashairi yametulia sana, unapigwa ila sio sana si unajua redio zetu na madj? lazima wapewe Ma dj kitu kidogo ndio upigwe au uufanyie kampeni ya nguvu.
Huo wimbo unazungumzia ufisadi wote uliotokea majuzi hapa nchini yaani una hot issues zote.
Wasiliana na Fred Mkoloni kwenye +255 71 623 8590. Uweze kuwasaidia usikike zaidi na uweze kuwasaidia wa shoot VIDEO.
FairPlayer
tehetehetehe!Mkuu hiyo ni mojawapo ya njia niliyo suggest ya kuwasaidia hawa wasanii wetu.Kuna watu wanaweza kutunga mashairi ila hawawezi kuimba na labda hawana muda wa kuimba Kama MwanaKjj anavyosema lakini kama akiwapa mashairi yake kwani ujumbe haufiki?Kaka/dada read and understand usikurupuke tuuuuuuu!
Ni sawa na wewe uliyempa JMushi no.ya simu ya mkoloni walikuambia wanataka msaada wa Video Shoot?
Kweli JF ni ya wote na siyo ya wachache wenye fikra duni kama weweSoma tena post yangu nimesema, tatizo sio WIMBO, nyimbo zipo. Na sikusema asaidie Video tu, nimesema a promote wimbo kusikika hewani ikiwa video ni njia mojawapo. UJUMBE HAUFIKI KWASABABU WIMBO KUTUNGA NI RAHISI ILA KUSIKIKA REDIONI NA KWENYE TV (Ujumbe kuwafikia walengwa) NDO ISSUE.
Aisee ngoja nijiondokee. Tofauti ya Mwizi na aliyekuwa anaoga akaibiwa nguo zake haitaonekana.
Umeshinda. OVER and OUT for GOOD on this!