Wasanii wa Bongo na Live Band

Handsome Rob

Senior Member
Jan 12, 2017
156
522
Jana nlipata wasaa wa kuangalia mashindano ya Bongo Star Search (BSS). Nmeangalia perfomance ya wale washindani pamoja na ile band yao, aisee napenda kukiri wale jamaa wa band wanajua vibaya mno. Kinachonishangaza ni haya matamasha yetu yanayoendelea kwanini hawatumii live band kama BSS..??

Nilishawah kuhudhuria Fiesta miaka kadhaa iliyopita kiukweli nliapa kutokuja kuhudhuria tamasha la muziki loloto apa bongo kwani ni bora nikae nyumbani nisikilize CD tu kuliko zile kelele.

Kwann wasanii wa bongo hawatumii live band kama ile ya BSS.??, wale jamaa wanajua sana wanafanya usichoke kuangalia.

Haya matamasha inatakiwa wajifunze kutumia live band..
 
Mkuu unataka bongo fleva ifee? Maana live band ni timu kamili sasa vijana wakufokafoka hawawezi
Mi nadhani ndo tutaweza kufikia level za juu sana, kuna kipindi Mwana FA alishawahi kufanya show na live band, aisee nadhani ndo show bora kuwah kuiona apa bongo.
 
Back
Top Bottom