Sababu kubwa 2 kwanini Miziki wa Tanzania kwa sasa ni Fake, Mgumu na Mbovu

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,617
34,062
Watu wengi sina hakika kama wanaliona hili ila Muziki wa Bongo fleva kwa kifupi umeingiliwa, umechakachuliwa na too bad ni kama unakufa.

Nadhani wanaopenda muziki kama mimi wanapata tabu tu na hawana la kufanya.

Na katika hili Clouds media ( Hususani marehemu Ruge ) hawezi kuepuka lawama.

Sababu:

1. Kwanza Tasnia ya mapromota Tanzania imekufa. Hakuna kabisa independent music promoters.
- Yaani hapa media ( au media related promoters ) ndio promoters kwenye muziki na wanamiliki wasanii.

2. Media ( hususani ambazo zimechagua niche ya burudani ) zimegeuka Record labels, waandaaji wa matamasha na promoters.

UFAFANUZI.

Ukuchagua kuwa mwanamuziki ( hata ukiwa na kipaji kama Michael Jackson ) kwanza bila kuwa katika upande mmoja muziki wako hauwezi kwenda.

- Hapa kuna pande kubwa 4.

1. Clouds media ( Waandaaji wa Fiesta )
2. Wasafi Media ( Waandaaji wa Wasafi festival )

Note: Waandaaji wa Tamasha la Fiesta na Wasafi festival ni kanpuni moja Prime time promotions ya Juhayna Kusaga.

3. Efm ( Waandaaji wa Muziki Mnene - hawa tamasha lao ni bure ).

4. Lastly, ni East Africa TV ( hawa hawana tamasha, ila hutoa tu suppory ).

So, bila kuwa associated na media mojawapo hapo juu maana yake hutapata Show wala promo kupitia media yao mwaka mzima🤣🤣🤣 ( Maana wanatoa promo kwa wasanii ambao finally watawtumia kwenye matamasha yao kwa ujira mdogo. )
Hapa hata wakikwambia ufanye tamasha bure, utafanya kama malipo ya promo na support uliyopewa.

- Pia, ukijinasibisha na media mojawapo tafsiri ni kwamba, hupati support kutoka media nyingine.

Na Kwasababu ya promo kubwa inayofanywa, tayari mashabiki wako brainwashed, wapo wapo tu kama waumini wa Gwajima.

Na hapa ndipo Muziki wa Tanzania ulipofikia, huhitaji kuwa na kipaji kuimba, unahitaji kuwa kwenye kundi mojawapo hapo juu.

Kwahiyo kwa wale wanaooenda muziki mzuri ( siyo wa kulishwa kwa lazima wajue hili )

Je, Tunaelekea wapi ?
 
Pongezi kubwa kwa Diamond platnumz simbaaa, mwamba pekee aliyeweza kusimama mwenyewe na kusimamisha wasanii wake na label yake kuwa moja ya label kubwa hapa Afrika bila pamoja na vita kubwa aliyopigwa na media zote kubwa za burudani nchini ila wameshindwa badala yake wanaanza kuitumia silaha aliyetengeneza mwenyewe.
Anyways,lete ushahidi unaoonyesha prime time promotion ni waandaaji wa wasafi festival.
 
Bongo fleva zenye video za uchi uchi tu, singeli, vogodoro na taarabu(mipasho) zikifungiwa tu ndipo hadhi ya mziki itakapobamba.
 
Hakuna unachoweza kuandika zaidi ya matusi...hongera kwa hilo.. kama busara yenyewe kazi unatoa wapi haki ya kushauru vijana walioamua kuwekeza nguvu, akili na vipaji vyao kwenye muziki.

Unafikiri muziki ni kuandikaandika tu nenda kwa mumeo...wanavuja jasho saana na wanapitia magumu. Sio kila mmoja anauwezo wa kutunga wimbo hata upate kupendwa na familia yake.

Lets appriciate the good work done by these guys. Kama ni rahisi nenda stidio kisha uje hapa.
Mkuu umesoma heading tu ndio ukachangia au umesoma na yaliyomo?

Nafikiri hujaelewa mada na sio mbaya kurudia kusoma mpaka ukaelewa
 
Mkuu umesoma heading tu ndio ukachangia au umesoma na yaliyomo?

Nafikiri hujaelewa mada na sio mbaya kurudia kusoma mpaka ukaelewa
Mkuu usimtegemee lolote la maana kutoka kwa watu takataka kama hao.

Ndio maana mimi nawaita misukule wanakasirika
 
Kwanini unadhani sijasoma mkuu? Kwasababu sijachangia kwa matarajio yako?

Hoja yangu inabaki pale pale...mtoa mada aingie studio aokoe muziki unaokufa.

Ila kama anaweza kuandikaandika tu aendelee.
Hapana mkuu sio kwasababu ya matarajio yangu bali ni umetoa maoni kuhusu hali ya wasanii wakati mleta sredi kaongelea hali ya mziki!
 
Acha maneno wewe....kama unaona kitu fake kafanye orijino.

Kuongea na kuandika andika kila anayejua kuunda maneno anaweza. Ingia sokoni tusikie muziki orijino. Acha poyoyo mingi maana ndicho aslimia kubwa ya wabongo mnachoweza.
Huyu jamaa anajifanya mjuaji alafu ukimzidi kwa hoja anakimbilia matusi na pia Ni mtu mwenye hasira sana
 
Pamoja na yote uliyoandika lakini sasa hivi ndo wanafanikiwa zaidi kuliko zamani.
Mkuu huyajui maisha ya wasanii.

One in million.

Leo Babu Tale au Mutta ni matajiri kuliko Ferooz au Saida Kaloli.
 
Mkuu huyajui maisha ya wasanii.

One in million.

Leo Babu Tale au Mutta ni matajiri kuliko Ferooz au Saida Kaloli.
Hao walikuwa zamani, lakini wewe umejikita na wa sasa.

Najua si wote lakini angalau tofauti na zamani, ingawa muziki wa zamani ulikuwa mzuri sana
 
kufanikiwa kupi huko?

Msanii mwenye mafanikio hapa bongo ni MONDI tu... am not his fan tho
Tho you ain't his fan, but at least unamkuabali.

Sio yeye tu hata genge lake zima la wasafi bila kumsahau konde boy angalau wamepiga hatua.

Zamani walitoa kazi nzuri sana lakini ndo hivyo.
 
Back
Top Bottom