Msonjo
JF-Expert Member
- Oct 13, 2019
- 1,378
- 2,395
Wakuu salaam
Unajua nimekuwa nikijiuliza hivi ni nani aliyesema msanii ni kioo cha jamii? au kuna maana gani unaposema msanii ni kioo cha jamii? au ni wakati gani msanii anakuwa ni kioo cha jamii?
Kwa ninavyofahamu unapojiangalia kwenye kioo unatakiwa ujione mapungufu yako. Na ndio kazi ya kioo, kama unavaa tai huku ukijiangalia kwenye kioo unaangalia ni sehemu gani haijakaa sawa ili uirekebishe. Na kama unaajiangalia usoni unaangalia ni sehamu gani kuna chunusi au kipele ili ukitumbue.
Sasa hawa wanaoitwa wasanii huwa huo ukioo wao upo wapi? maana si kwa nyimbo wanazoimba (hadi nyingine kufungiwa na BASATA), wala kwa maigizo wanayoigiza,wala kwa mavazi ya ajabu ajabu wanayovaa na mienendo yao kwa ujumla.Ni skendo tu za ajabu ajabu.
Usiseme eti wanaelimisha jamii,elimu gani hasa? na kama ni kuelimisha mbona walimu wanaelimisha lakini hawaitwi vioo.
Na kuelimisha tu haitoshelezi kuitwa vioo,maana wana mapungufu mengi.
Labda wawe ni burudani tu kwa jamii,na hapo ni kwa atakayetaka kuburudika. Lakini kwa vioo vya jamii hapana.