Wasanii mmepewa mikopo mikubwa, Wekezeni mtoe Ajira kwa Vijana, Kumbukeni mtarudisha ni mikopo

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Hongera sana kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kufanikisha jambo kubwa la kutoa mikopo kwa Wasanii wa Tanzania.

Ni jambo la kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa kiasi cha zaidi ya TZS 1,000,000,000 (zaidi ya bilioni moja) ili mkopeshwe Wasanii.

Lengo la mikopo hii ni mkafanye uwekezaji wa kutosha katika tasnia zenu ili muweze kuajiri Vijana wenzenu wa Kitanzania na hatimaye muweze kushindana na soko la dunia katika tasnia zenu.

Ni mategemeo ya Watanzania wengi mtatoa ajira na mtalipa kodi. Watanzania tulifurahi tulipo ona nyuso zenu zenye Tabasamu wakati mkipokea mfano wa hundi zenye thamani ya mikopo mliyopewa.

Ni fedha nyingi kama zitawekezwa na kutumika kwa lengo lilotolewa, Serikali imewathamini saana, kwa fedha mlizokopeshwa. Lakini ni fedha ndogo kama tutaamua kwenda Dubai.

Lazima mjue, mna jukumu la kuzirejesha fedha hizo ili waje wakopeshwe watu wengine na Serikali isione mpango huo hauna maana, mkirudisha pengine baadaye watakopeshwa Vijana wanaomaliza vyuo ili kuweza kuajiajiri na kuajiri Vijana wengine.

Mhe. Mohamed O. Mchengerwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, ni muwazi, ni mkweli, ana penda haki, ni mpenda Maendeleo, ni Mzalendo, Wasanii mtumieni, ila sio vibaya kuwakumbusha Mchengerwa ni mtu anayeita kijiko ni kijiko na siyo "spedi" hivyo mkumbuke atahakikisha mnalipa ili zikawasaidie wengine.

Hongera saana Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

Mungu ibariki Tanzania

Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom