Tuache uwanja wa kampeni uwe huru kwa watu wote wanaopenda kupigia kampeni upande fulani. Wasanii ni watu wanaohudumia jamii sawa na viongozi wa dini, wasanii wana utashi, wafuasi na wapenzi wao sawa na viongozi wa dini. Wasanii wanashawishi wapenzi wao na viongozi wa dini wanashawishi wafuasi wao, lakini mwisho wa siku watu nao huwa wana akili na matakwa yao, wataamua nani watampigia kura.
Haiwezi kuwa sawa wasanii waruhusiwe kufanyia mtu kampeni lakini viongozi wa dini wanyimwe. Kwani shida ni nini hasa Mh. Lubuva?, ruhusu wote au kataza wote (all or none) utaeleweka sana.
Ila wengi wa wasanii no pro-CCM! Donge la Kampeni lilishatengwa na wamekumbukwa!!
Taasisi yoyote hata iwe ya kishetani iko sawa kama itapigia kampeni upande fulani, lakini haiko sawa kama itapigia kampeni upande wa pili. Tumeona baadhi ya vyombo vya habari, taasisi, na makampuni yakilalamikiwa na mengine yakinyamiziwa kimya yanapoegemea upande.Naomba mifano mitano ya nchi ambazo zimeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya wasanii kushabikia upande fulani wa kisiasa.
Taasisi yoyote hata iwe ya kishetani iko sawa kama itapigia kampeni upande fulani, lakini haiko sawa kama itapigia kampeni upande wa pili. Tumeona baadhi ya vyombo vya habari, taasisi, na makampuni yakilalamikiwa na mengine yakinyamiziwa kimya yanapoegemea upande.
Dk Magufuli ni chaguo la wazalendo...Ccm mpya, Tanzania Mpya! 2015!
Kitu kilichoanzishwa mwaka 1977hakiwez kuwa kipya mwaka 2015 ongea kwa mntiki mkuu...kwa kikwete mlisema hivi hivi matokeo yake tupo hapa
Kwahiyo unasema Lowassa na ile taasisi aliyotokanayo ccm ndo inatuhakikishia mabadiliko? Jitambue bwa'mdogo
Magufuli ameamua kutumia makahaba kwa kampeni?
Ni aibu kwa ccm, hapo usikute anafanya hivyo ili baadae apate uteuzi serikalini, na unaweza kushangaa kumsikia anapewa uongozi kweli.
Kwahiyo unasema Lowassa na ile taasisi aliyotokanayo ccm ndo inatuhakikishia mabadiliko? Jitambue bwa'mdogo
Watakujibu wasomaji wengine wa jf hilo swali lako linalotaka kuhalalisha kutumika vibaya kwa wasanii kubeba mgongoni mafisadi kwenda Ikulu. Baada ya uchaguzi kwisha kazi za wasanii hao zitadoda kwa hasira za walioshindwa, na mifano hai tunayo ya wasanii walioanguka kwasababi za kushabikia vyama.Mkuu, nimeongea lugha nyepesi tu ya Kiswahili. Nimetumia maneno rahisi kuwa "Naomba mifano mitano ya nchi ambazo zimeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya wasanii kushabikia upande fulani wa kisiasa." Naona unanipa hadithi badala ya kujibu swahi langu. Kama hakuna mifano sema hakuna, kama ipo basi itaje hapa. Sihitaji hayo maelezo uliyonipa, nahitaji mifano tu.
Ni kweli ila tatizo la wasanii wa bongo ni NJAA, CCM iliwaahidi mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwajengea studio ya kisasa na pia kulishuhulikia tatizo la haki miliki(copyright) ya kazi zao. ILA HAKUNA LILILOFANYWA NA CCM,zaidi ya kuwatumia kipindi cha kampeni ili kupata watu wengi kwenye mikutano yao.
Watakujibu wasomaji wengine wa jf hilo swali lako linalotaka kuhalalisha kutumika vibaya kwa wasanii kubeba mgongoni mafisadi kwenda Ikulu. Baada ya uchaguzi kwisha kazi za wasanii hao zitadoda kwa hasira za walioshindwa, na mifano hai tunayo ya wasanii walioanguka kwasababi za kushabikia vyama.