Wasanii Aunti Ezekiel na Vincent Kigosi kutoka UKAWA wajiunga na kampeni za CCM

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Zikiwa zimebaki takribani siku 39 kuelekea siku ya Kupiga kura. Wasanii wawili wa tasnia ya Maigizo waliokuwa katika Kampeni za Mh Edward Lowassa wa CHADEMA ghafla wameamia kwenye Kampeni za Mh John P. Magufuli wa CCM.

Hii imethibitishwa na mmoja wa wasanii hao, yaani Anti Ezekiel kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter. ( Auntezeofficial)

Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza kuchukua headlines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzi.

Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao sasa ripota wa millardayo.com amezungumza na Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na Mwanao…’Ndugu zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt Ezekiel walitoroka wamerudi CCM kabla hawajatangaza lakini watatangaza wamerudi kwa kishindo kikubwa wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere

‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania kuwa hao watu wamerudi katika chama cha mapinduzi na wala msidanganywe pilika pilika za huku na kule hawa watu ni wanachama wa CCM hai walitoroka na sifa ya kutoroka ni kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao tuna watoto , mtoto akitoroka unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi afahamu njia ya sahihi na njia sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho kina Dkt John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu’ – Steve Nyerere

"Nimeamua kuondoka Chadema na vuguvugu la Ukawa kwa sababu mbalimbali:

Moja ni ubovu wa kimfumo katika uongozi, uratibu na misimamo.

Fujo: Wafuasi wengi Ukawa bado wana muhemko kwenye kufanya mambo. Naamini uongozi wa nchi unahitaji busara kuhimili kazi. Tumefeli hilo.

Kwa siku 39 zilizobaki nitaongea na mamilioni ya mashabiki wangu kuhusu msimamo wangu. Naondoka Chadema, nitamuunga mkono Magufuli". Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika Aunt Ezekiel
 
Msanii ni mwananchi wa kawaida kama wewe na mimi, wanayo haki ya kupenda na kuchagua yeyote wanayeona kwao ni

bora ka maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Ndio maana leo hii wapo wasanii wanaopenda Chadema na wapo wengine

wanaopenda CCM, kwa hiyo mi nadhani tusipoteze muda kumjadili mtu mmoja mmoja wakati tuko na jukumu kubwa la

kufanya Oct 25.
 
Kumbe wale watu wote waliokuwa wanakusanyika kwenye mikutano huwa wanawafuata wao!?
Nasikitika sana kuwa nchi ya Tanzania tuna tatizo lingine ambalo ni kubwa zaidi na waote tumerelax na kuchekea tu.
Hebu fikiri Mzee Warioba anaposimama jukwaani mchana kweupee na kusema kuwa 'UKAWA wanataka kuvujna muungano', kisa kwa sababu wanaamini katika rasimu aliyoitengeneza kutokana na maoni ya wananchi!
 
Msanii ni mwananchi wa kawaida kama wewe na mimi, wanayo haki ya kupenda na kuchagua yeyote wanayeona kwao ni

bora ka maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Ndio maana leo hii wapo wasanii wanaopenda Chadema na wapo wengine

wanaopenda CCM, kwa hiyo mi nadhani tusipoteze muda kumjadili mtu mmoja mmoja wakati tuko na jukumu kubwa la

kufanya Oct 25.

Uko sahihi, ila tujiulize kwanini urubuniwe kwanza ndio uhame?...maana yake sio utashi wako ila umelazimishwa kwenda huko. Hizo milioni hamsini si wangejenga hata choo cha shule tu.
NDIO HAPA BADO TUNASEMA CCM NI TATIZO.
 
Lakini mheshimiwa labda nikuulize swali dogo tu, una ushahidi wowote labda wa makabidhiano ya hizo fedha tajwa?
 
Hakuna anayeweza badili fikra zangu kuhusu mabadiliko hata wazazi wangu awawezi hilo sasa hao wasanii awasumbui hakili zangu ata kidogo waende ata wapi slaa ndio aliniumiza sana kwenye mabadiliko kwa sababu nilimwamini na kumpa kura yangu mwaka 2010
 
Sikio la kufa halisikii dawa! Good riddance

Zikiwa zimebaki takribani siku 39 kuelekea siku ya Kupiga kura. Wasanii wawili wa tasnia ya Maigizo waliokuwa katika Kampeni za Mh Edward Lowassa wa CHADEMA ghafla wameamia kwenye Kampeni za Mh John P. Magufuli wa CCM.

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/09/UKAWAAA2.jpg?zoom=4&resize=337,352

Hii imethibitishwa na mmoja wa wasanii hao, yaani Anti Ezekiel kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter. ( Auntezeofficial)

.http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/09/UKAWAAAAAAAAAA.jpg?zoom=4&resize=337,286

Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza kuchukua headlines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzi.

Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao sasa ripota wa millardayo.com amezungumza na Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na Mwanao…'Ndugu zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt Ezekiel walitoroka wamerudi CCM kabla hawajatangaza lakini watatangaza wamerudi kwa kishindo kikubwa wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere

.

‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania kuwa hao watu wamerudi katika chama cha mapinduzi na wala msidanganywe pilika pilika za huku na kule hawa watu ni wanachama wa CCM hai walitoroka na sifa ya kutoroka ni kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao tuna watoto , mtoto akitoroka unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi afahamu njia ya sahihi na njia sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho kina Dkt John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu' – Steve Nyerere
 
Back
Top Bottom