Wasanii ambao mziki ulisababisha wapoteze majina yao ya asili

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
Imekuwa ni kawaida kwa kampuni, taasisi na mashirika makubwa duniani kote kubadili majina kutokana na sababu za kibiashara, kubadilishwa kwa lengo la uanzishwaji wake au kuuzwa kwa mmiliki mwingine.

Hilo pia hujitokeza kwa wasanii wa muziki, filamu na mitindo kwa lengo la kuimarisha chapa zao ili kuvutia mashabiki ambao ndio wanunuzi wa bidhaa wanayoizalisha. Je, kwenye Bongofleva hali ipo vipi? Makala haya yanaenda kuangazia wasanii 10 wa muziki huo ambao wamewahi kubadili majina.

1. SARAH - SHAA
Jina la kuzaliwa ni Sarah Kaisi, alipoanza muziki alikuwa akijiita Sarah pekee, jina la Shaa lilitokana na jina la kundi la Wakilisha ambalo liliundwa na wasanii watatu ambao ni Witness, Marehemu Langa Kileo na Shaa mwenyewe, hivyo aliongeza herufi A mwishoni.

Hata hivyo sio Shaa aliyeunda jina hilo bali ni rapa Albert Mangwea aliyefariki mwaka 2013. Shaa sio msanii wa kwanza kupewa jina, kuna wasanii wengine kama Young Dee aliyepewa jina hilo na Dully Sykes.
1622451341190.png

2. RAPCHA - JOH MAKINI
Rapa huyo kutoka kundi la Weusi kabla ya kusikika akiwa chini ya River Camp Soldiers alikuwa anatumia jina la Rapcha kama anavyokumbushia kwenye wimbo wake uitwao ‘Bye Bye’ aliomshirikisha G Nako.

Jina Joh Makini ni chimbuko la jina lake la kuzaliwa, John Mseke, hata hivyo jina alilolitupa (Rapcha) limeokotwa tena. Pale Bongo Records kuna Rapa mwingine anaitwa Rapcha ambaye kwa sasa anafanya vizuri.
1622451452140.png

3. LIL K - YOUNG KILLER
Kabla ya kuanza kutumia jina la Young Killer mwanzoni alikuwa akijita Lil K, hii ni kufuatia umaarufu wa Rapa wa Marekani, Lil Wayne aliokuwa nao wakati ndoto ya Young Killer kimuziki ikiwa imeiva.

Wakati Young Killer akitumia jina Lil K alitoa wimbo uitwao ‘Winner’ ambao alimshirikisha Barakah The Prince ambaye kipindi hicho alitambulika kama Dogo Baraka. Wimbo huo ulitengenezwa na watayarishaji wawili ambao ni Duke Tachez na Deey Classic ndani ya studio za Rock Town Records.
1622451571619.png

4. NIGGA JAY - PROFESSA JAY
Rapa huyu aliyetoka na kundi la Hard Blasters Crew (HBC) waliofunika zaidi mwaka 2000 na albamu yao iitwayo ‘Funga Kazi’, mwanzoni alikuwa anajiita Nigga Jay, lakini baadaye akaja na Professa Jay.

Hata jina la Professa Jay sio yeye aliyeliunda, bali alipewa, yupo nalo hadi sasa ingawa limekuwa likipambwa na a.k.a kama Wamitulinga, Mbunge Nje ya Bunge na mengineyo.
1622451675680.png

5. DOGO BARAKA- BARAKA DA PRINCE
Huyu ni miongoni mwa wasanii waliofanya sana marekebisho kwenye majina yao, alianza kujiita Dogo Baraka. Wakati anatoka kimuziki alijulikana kama Baraka Da Prince na sasa kaliboresha kidogo na kuwa Barakah The Prince.

Wakati akitumia jina la Dogo Baraka alisababisha video ya wimbo ‘Winner’ wa Young Killer (Lil K) kutofanyika kwa kuwa siku ya kushuti video alikwenda akiwa amepaka rangi kwenye nywele zake.
1622451832918.png

6. DOGO HAMIDU - NYANDU TOZZY
Ni miongoni mwa wasanii walioanza muziki wakiwa na umri mdogo sana, wakati akiwa na Dar Skendo chini ya Dudu Baya alijulikana kama Dogo Hamidu.

Rapa huyu kutokea ‘26 Life’, kadiri muda ulivyozidi kwenda na kuwa mtu mzima akaamua kuachana na jina hilo, ndipo likaibuka na la Nyandu Tozzy ambalo analitumia hadi sasa.
1622451976764.png

7. NIKKI MAKINI - NIKKI WA PILI
Kutokana na kaka yake Joh Makini kuwa tayari ameshatoka kimuziki, Nikki alishawishika kutembelea gia hiyo kama alivyofanya Abdukiba baada ya kaka yake, Alikiba kutoka kimuziki.

Hata alipokuja kujiita Nikki wa Pili kitu hicho kilikosolowa na Nikki Mbishi kupitia wimbo ‘Puch Line’ aliomshirikisha Grace Matata. Mbishi alisema; “Kivipi Nikki wa Pili na wa kwanza hajulikani, Wakili unakosa dili kwa stanza hatulingani”.
1622452059568.png

8. LIL SAMA - MR. BLUE
Mwanzoni alikuwa anajiita Lil Sama, baada ya kutoa wimbo ‘Blue’ na kufanya vizuri sana, ndipo watu wakaanza kumuita Mr. Blue na yeye hakutaka kubadilisha hadi leo.

Hii ni sawa na Rapa One The Incredible, wakati anaanza muziki alitambulika kama One lakini alipotoa wimbo uitwao Incredible na kufanya vizuri, ndipo likazaliwa jina la One The Incredible.
1622452277555.png

9. 2PROUD - SUGU
Rafiki yake mzungu ambaye alikuwa akimkubali kimuziki ndiye aliyempa jina hilo, ni kufuatia kauli zake za kila mara ‘Am too proud of you’ (najivunia wewe), katika kufupisha, yule mzungu ndio akaja na jina hilo, 2Proud, kisha likafuata Mr. Two.

Mbeleni kabisa miaka ya 2000 baada ya kutoa albamu kadhaa na misimamo yake katika muziki katika kudai maslahi yake na kwa wasanii wote kwa ujumla ambayo yalikuwa akiporwa na wauzaji wa albamu (kanda) ndipo likaibuka jina la Sugu.
1622452361951.png

10. NEY - NAY WA MITEGO
Rapa huyo kutokea Free Nation kabla ya mwaka 2005 alikuwa hatumii jina hilo, bali alikuwa anaitwa ‘Ney’ jina alilopewa na mpenzi wake ambaye ndiye aliyemlipia fedha ya kurekodi wimbo wake wa kwanza ndani ya Bongo Records.

Mwaka 2005 alitoa wimbo uitwao ‘Wamitego’ ambao ulifanya vizuri kwa kiasi chake, ndipo mashabiki wengi wakampa jina la Nay wa Mitego ambalo Nikki Mbishi aliwahi kuliponda kupitia wimbo wake (diss track) uitwao Ney wa Mitego.
1622452736122.png


Pia kuna wasanii waliofanya marekebisho madogo kwenye majina yao, nao ni;
Raymond - Rayvanny
Nikki Ray - Nikki Mbishi
Maromboso - Mbosso
Darasa - Darassa
Q Chief - Q Chillar na wengineo.



©MwanaSpoti
 
Sijaelewa hasa mantiki ya hii thread Ni Kama vile tumepewa making mawili wawili ya wasanii..nimetoka kapa
 
Kuna msanii mmoja anaitwa Hongera. Yeye ilo jina ndio alikua lake kabisa, nimelisahau jina lake la kisanii, ila kulikua na tamasha sasa mtu mmoja alienda jiandikisha kwa jina la Hongera. Ikafika zamu yake wanaita Hongera apande stejini hakuna mtu, jamaa akajiripua akapanda. Hafu akachana fresh tu.

Ana wimbo unaimba:

Mashabiki bwana "Shukaaa Shukaaa",
Ata sijaanza kuchana "Shukaaa Shukaaa"...
 
Back
Top Bottom