Mimi sio muangaliaji wa TV hiyo,kuna siku nilienda kwa jamaa yangu nikakuta wanaangalia Wasafi TV,tena kipindi hiko hiko cha Story book na walikuwa wanaongelea kuhusu WORMHOLE....sasa cha kusikitisha huyo host ambaye anajiita profesa alikuwa na ubao na chaki,katika uchambuzi wake wa hilo jambo akachukua chaki akaandika ubaoni WORMHALL..nikasema huyu anafafanua kuhusu wormhole kwenye TV lakini yeye mwenyewe hajui inaandikwaje,pili kipindi kina timu kubwa sana ya maandalizi,mpaka kinaruka hewani hakuna hata mtu mmoja aliyegundua profesa wao kakosea kuandika neno wormhole.