Wasafi hawaponi sakata la dawa za kulevya- Afande Sele

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
Afande Sele amefunguka na kusema kama jambo hili litafanywa kwa haki na umakini basi huenda hata wale wasafi wakaonekana ni wachafu.

Afande Sele ameonyesha wasiwasi juu ya sakata hili la madawa ya kulevya ila amesisitiza kuwa kama kweli litafanyikwa kazi kwa umakini mkubwa basi kuna kundi kubwa la watu ambao wanaonekana ni wasafi kuchafuka kutokana na sakata hili.

"Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya unga kama kweli braza Paul yupo 'serious' na sio 'Matango Pori'kama tulivyoona katika masakata mengine, huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu...kila la kheri Mr Paul....RiP dada Amina...wacha party ianzeee" aliandika Afande Sele

Kauli hii ya Afande Sele imekuwa ni kauli tata na imeibuka mjadala kwa baadhi ya mashabiki katika kuitafsiri wengine wakisema Afande Sele amezungumzia wasanii ambao wapo chini ya label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz huku wengine wakisema amezungumzia watu ambao wanaonekana ni wema katika jamiii kumbe si wema bali ni wachafu kwa matendo yao kwa kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.
Wasafi hawaponi sakata la dawa za kulevya- Afande | East Africa Television
 
Watatajana tu,twende mpaka wiki ijayo siku kama hii tutasikia mengi!!kwani huo unga mtamu kama maziwa jamani mbona wanang'ang'aniaa?? Wagonge milk kama mm basi mororooooooo!!
 
Watoto wa watu wanakaza kwenye game watu wanaleta majungu wakati wao kutwa wanashinda wanakula bange... Hivi afande sele ni wa kuwasema wasafi kweli? Au katumwa
 
Tusimbeze Afande, ndege wanaofanana huruka pamoja, labda anaruka nao ila wao wanaruka juu zaidi. Ukimuweka pembeni atakwambia idadi ya ndege na jinsi wanavyoruka.
 
Hii ndio shida ya hii nchi! Kila wakati kumuandama mwenye mafanikio ....
Tangu walipoanza kusema Diamond anauza unga angekuwa ameshakamatwa!
Wenzao kila siku wanakaza kwenye muziki wao yamebaki majungu tu
 
Hii ndio shida ya hii nchi! Kila wakati kumuandama mwenye mafanikio ....
Tangu walipoanza kusema Diamond anauza unga angekuwa ameshakamatwa!
Wenzao kila siku wanakaza kwenye muziki wao yamebaki majungu tu
Ukweli utajulikana muda ukifika
 
Watoto wa watu wanakaza kwenye game watu wanaleta majungu wakati wao kutwa wanashinda wanakula bange... Hivi afande sele ni wa kuwasema wasafi kweli? Au katumwa
Kwani afande si anakula majani ? Majani yana shida gani mkuu ?
 
Afande sele hajui kama Bange ni madawa ya kulevya pia! Ajiandae tu.. Ukiona mwenzio ananyolewa nywele ngumu zinauma wewe tia maji
 
Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya unga kama kweli braza Paul yupo 'serious' na sio 'Matango Pori'kama tulivyoona katika masakata mengine, huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu...kila la kheri Mr Paul....RiP dada Amina...wacha party ianzeee" aliandika Afande Sele
Inawezekana ni kweli tusubiri uchunguzi
 
Watu walishapotea wanatafuta jinsi ya kurudi hawajui sisi tuko busy na HAMO RAPA!!! Wakwendreee
 
Serikali inawafahamu wanao uza hayo madawa ya kulevya lakini haiwachukulii hatua


Kuna wabunge kama ridhiwani na watoto wa vigogo wengine humo ndiyo maana Kikwete alipokabishiwa ile list aliogopa kuona kuna viongozi humo ndani na wajanja wa mjini. WCB kwa kweli inahusika sana pamoja na Clouds Media. Tusubiri tu.
 
Back
Top Bottom