Wasabato huyu mama ni tapeli ni nani alimleta kwenye mikutano yenu?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,296
3,967
Kuna mama mmoja aliwahi kuwa mkutano wa Dodoma. Nilipata fursa ya kusikiliza baadhi ya vipindi.

Alizungumza mengi mojawapo likiwa madai tena kwa kujiamini kuwa ana dawa ya kuondoa mvi.Kutokana na alivyokuwa anajiamini na mimi kudhani hawezi kusema uongo katika madhabahu, nilitumia fursa kununua kwa ajili ya biashara.

Siwezi kusahau kilichonikuta
Nilipata dawa ambayo ni mafuta ya nazi yaliyochanganywa na maji yaliyotoa harufu mbaya sana.Mteja wangu alipaka hivyo hivyo lakini hakuona matokeo.

Hivi sasa kuna clip yake moja inasambaa kwenye mitandao akisema hamkubali mwanaume anayekula wali. Kwamba wali unaathiri nguvu za kiume.

Mimi nasema huyu mwanamke ni tapeli mkubwa. Wali, ugali, ngano, viazi vyote, muhogo na ndizi vyote ni wanga. Ni kujaribu kudanganya watu kuwa muhogo ni bora kuliko mahindi ama mtama.

Naomba huyu mwanamke achukuliwe kwa tahadhari kwani ni tapeli mkubwa.

Ninawatahadharisha kuwa hizi ni nyakati za mwisho na kuweni makini kusikiliza mafundisho ya mashetani.
Kuna vitu vingi vinaathiri afya ya mwanaume siku hizi ambavyo ni vigumu kuepukika.
 
Kana una akili nzuri utatafuta ku solve changamoto zilizo kwenye jamii na mazingira ulipo.Pesa zitakufuata zenyewe
 
Wasabato hawavumi lakini wamo.....
:D
1694793983539.jpeg
 
Hii kazi yenu maskini endeleeni kutafuta hela huenda mtazipata siku moja.

Kuna watu pesa zinatutafuta

Hakuna mtu anayefuatwa na Pesa pumbavu wewe. Taja tajiri mkubwa unayemjua duniani then njtakuonyesha kwamba hela hazimfuati.
 
Asee kwanza kwanini ukatae mvi kama hutaki mvi nyoa kipara.. Halafu asikudanganye mtu punje zinaongeza ashiki hatari sana mchele, mtama na vingine ni hatari sana
 
Ila hapo kapuyanga...yani walii kabisa?? Wali huu huu? Au kuna wali mwengine....wali una madhara kama mtu ni mgonjwa tayari hasa wa sukari kwa sbb wanasema ni bora kwa mgonjwa kula ugali wa dona kuliko wali...ila otherwise atupe tafiti yake alofanya
 
Ila hapo kapuyanga...yani walii kabisa?? Wali huu huu? Au kuna wali mwengine....wali una madhara kama mtu ni mgonjwa tayari hasa wa sukari kwa sbb wanasema ni bora kwa mgonjwa kula ugali wa dona kuliko wali...ila otherwise atupe tafiti yake alofanya
Wali is not good kabisa, huu huu ubwabwa tunaokula kila siku sio mzuri kwa afya. Hata Prof Janabi alishasema sana kuhusu hili.
 
Huyo Janabi naye ni walewale mara bia mbaya inaleta matatizo ya moyo na blabla kibao.

Huyo mama wa Kisabato wache awapigie wajinga.

Inakuwaje Mungu aliumba vipindi mbalimbali kwa mwanadamu kuanzia mimba na kuendelea sasa umri umefika wa kuota mvi wewe hutaki kwa sababu gani unataka bado uendelee kuitwa bebi unyandue madenti kwa kasi ya 5G?

Wali is not good kabisa, huu huu ubwabwa tunaokula kila siku sio mzuri kwa afya. Hata Prof Janabi alishasema sana kuhusu hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom