Warning kuhusu simu za Galaxy S4, S3, Note 2 za kichina

Warning kuhusu simu za Galaxy S4, S3, Note 2 za kichina

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,068
Reaction score
43,510
Umeona wapi Galaxy S4 ikauzwa chini ya milioni 1? Nilishangaa sana nilipoona hizi galaxies zikiuzwa cheap sana mwanzo nilifikiri wanaiba ila sasa nimekuja kugundua kumbe ni za kichina ila mchina huu ni balaa kwa macho ya kawaida huwezi kugundua hadi ufikirishe kichwa sana.

sgs4-fake

hio picha hapo juu ni ya galaxy s4 fake ya kichina
hebu tuangalie specificatio za galaxy s4 ya kichina na original.

specification za galaxy s4 origial
Processor: Quadcore snapdragon 600 1.9 ghz
RAM: 2gb
Kioo: inch 5
OS version: Android jelly bean 4.22
na benchmark za antutu zipo hivi

Samsung-Galaxy-S4-AnTuTu-3.3.jpg

Specification za galaxy s4 ya kichina
Processor: mediatek 1ghz quadcore
RAM: 1gb
Kioo: 5inch
OS version: Android jellybean 4.22

Kwa macho ya kawaida huwezi tofautisha perfomance even nilirun antutu kwenye galaxy s4 ya kichina ilifika 22,000

So nawatahadharisha wabongo kuwa makini na simu za bei rahisi na kujiona wamepata simu kali kwa bei rahisi.vitu vifuatavyo ufanye kuitambua simu hizi za kichina.

1. Camera Quality: Hata ikija na camera 13mp simu ya kichina itatoa picha vibaya hakikisha unapiga picha mbili tatu kujua quality
2. Download application yoyote ya benchmark, antutu ni nzuri pima score za simu yako kwenye proccessor, gpu na jinsi inavyo-render graphic kujua kama itascore kama galaxy original. score original zipo kibao online.
3. Charger yake usb na earphone hazina quality ya flagship

Je, zinafaa kununa hizo za kichina?
Sio mbaya kununua hizi clone za kichina lakini hazi-deserve kuuzwa hela nyingi. Simu kama hii yenye quadcore 1ghz ina-deserve around 300,000 hadi 400,000!
update
Sishauri mtu kununua simu ya clone, sasa hv unapata simu original kwa bei reasonable

So, muwe makini wana JMF!
 
Chief-mkwawa, vipi kuhusu iphones

zipo nyingi tu feki sema zinagundulika kirahisi
1. ukitype hairespond vizuri kila saa unakosea au ukitouch namba haifany kitu
2. zinatumia line kubwa badala ya ndogo
3. hazina playstore ya kudownload apps
4. zina java apps wakati iphone haina java
5. ukiclick browser ya safari inakuletea uc browser
6. nyengine zina memory card wakati iphone haitumii memory card
7. zina usb cable universal ya kawaida kama nokia, samsung wakati iphone cable yake ni unique
8. mandishi mandishi ya kichina unayakuta baadhi ya maeneo wakati kwengine ni kingereza
 
Mkwawa hizo simu ziko nyingi sana Dubai,na bei yake kama hizo s4 wanauza dirham 450 kama laki 2,ndugu yangu inataka uwe mzoefu wa simu tena sana ndio utazigundua lakini vinginevyo huwezi,nyuma zimeandikwa made in Korea,zipo s3 s4 na iPhone 5 jamaa kwa copy mara hii wmaefaulu,
Kama mtu akiwa hajawahi kutumia simu Kati ya hizo hawezi kujua kama feki,

Kuna rfk yng aliniagiza s3 tatu nashkuru maduka ya wenzetu hawakuzii kitu mpaka wakufahamishe kilivyo,ilibidi niende maduka ninayo yaamini ndio nikanunua s3 hizo,
 
Na je, inaweza kuwa ni iphone feki na wakati huohuo ikawa na SIRI?
 
Na je, inaweza kuwa ni iphone feki na wakati huohuo ikawa na SIRI?

nop feki haina siri ila wachina wanaweza kueka voice feature then wakajifanya ni siri hebu jaribu kuitumia uone kama inarespond
 
Mkwawa hizo simu ziko nyingi sana Dubai,na bei yake kama hizo s4 wanauza dirham 450 kama laki 2,ndugu yangu inataka uwe mzoefu wa simu tena sana ndio utazigundua lakini vinginevyo huwezi,nyuma zimeandikwa made in Korea,zipo s3 s4 na iPhone 5 jamaa kwa copy mara hii wmaefaulu,
Kama mtu akiwa hajawahi kutumia simu Kati ya hizo hawezi kujua kama feki,

Kuna rfk yng aliniagiza s3 tatu nashkuru maduka ya wenzetu hawakuzii kitu mpaka wakufahamishe kilivyo,ilibidi niende maduka ninayo yaamini ndio nikanunua s3 hizo,

mkuu kwa laki mbili ni bei nzuri sana. vp na mi nkitaka naweza kupata?
 
Ni pm chief mkawa ntakupa adress zangu,utapata ziko nyingi sana hapa Dragon Mart Dubai,kwa sababu naishi karibu na hapa
 
GONGO iite KONYAGI feki.
kinachofanya gongo iwe be poa ni gharama nafuu za utengenazaji.
kinachofanya konyagi iuzwe bei mbaya zaidi ya gongo ni gharama za logo ya TBS. Athari zake kwenye ubongo, maini, na figo ni zilezile.

mkuu ninachoongea hapa ni kua mtu ametoa buku kanunua kiroba kumbe ndani ya kiroba cha konyagi wajanja wamejaza gongo ambayo angeipata kwa sh 200
 
Je zinatumia android jelly bean kweli au hata os ni fake
Na kama inatumia os original inabeba apps za android bila shida?
 
afadhali mi uwa nasubiri kwanza hata mwaka upite ndo nichukue, mimi now galaxy s2
 
Hahaha. Sasa OS hujui, simu yako unatumia kubip na kutuma sms ama? Usipotee sana shemeji.
Mi hayo mambo ya OS sijui atuntu siyajui..nilinununua galaxy S4 dukani kwa samsung dealer, ni made in China...warranty ya miaka 2 inacover mpaka physical damage.
.
 
Back
Top Bottom