Warning, Disturbing Images: Je umeshawahi kutoa mimba?

Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
8,316
17,455
Watu wengi huwa wanajaribu kuunga mkono suala la kutoa mimba pale ambapo wahusika hawakupanga kupata mtoto. Wengine hutetea kitendo hicho eti kama msichana akibakwa basi anahaki ya kutoa. Kuna wanaosema mwanamke anahaki ya kufanya chochote kwasababu huo ni mwili wake. Je hii ni sawa?

Kunabaadhi wanapinga kutoa mimba miezi ya mwisho (baada ya wiki ya ishirini) lakini wanakubali kutoa wakati wa wiki za mwanzoni eti sababu hawaui binadamu bali vijiseli. Jee hii ni kweli?

Dedicated to all babies who were murdered, Amen

Last edited by a moderator:
Hii ni dhambi ambayo inaandama watu wengi tuliopitia madarasa kadhaa

Dhambi zote kwani si zinauzito sawa kwa mujibu wa maandiko?

Sasa dhambi hiyo ya kuuwa kichanga na kuzini si ni sawa au? (sawa na ya kusema uongo, kudokoa vitu vya watu, n.k?)

Ufafanuzi tafadhali

Dhambi zote kwani si zinauzito sawa kwa mujibu wa maandiko?

Sasa dhambi hiyo ya kuuwa kichanga na kuzini si ni sawa au? (sawa na ya kusema uongo, kudokoa vitu vya watu, n.k?)

Ufafanuzi tafadhali

Ndio Dhambi zote sawa, tatizo kuna dhambi zinazaa nyingine na nyingine: Mf mtu aliye ua tukio lile litachukua muda sana kutoka akilini au lisitoke kbs, tofauti na aliye tukana nk

Ndio Dhambi zote sawa, tatizo kuna dhambi zinazaa nyingine na nyingine: Mf mtu aliye ua tukio lile litachukua muda sana kutoka akilini au lisitoke kbs, tofauti na aliye tukana nk

As long as dhambi zote ni sawa, hapo ndipo panapokuja urahisi kwa watu kutoa mimba. Kama zote ni sawa, na aliweza kuzini repeatedly mpaka akapata hiyo mimba, hana sababu ya kutotoa mimba hiyo.

Hiyo athari ya kutotoka akili tu, kwake yeye haimkeri.

Mwalimu kwani mtazamo wako kwenye utoaji mimba ni nini?

Naamini kuna occasions-rarely I admit- zinazolazimisha mimba kutolewa ambazo afya ya mama inakuwa hatarini.

Mimba iruhusiwe kutolewa kwenye situations kama hizo na kila ikiwa changa ni bora zaidi.

wanawake wachache sana ambao hawajawahi kutoa mimba. Hasa kipindi chao cha utoaji mimba ni kuanzia sekondari na chuo

Gaijin, vipi kwenye macho ya sheria za nchi, haya makosa yana adhabu kali zaidi, hiyo haikufanyi uone kuwa hayalingani?

Gaijin, vipi kwenye macho ya sheria za nchi, haya makosa yana adhabu kali zaidi, hiyo haikufanyi uone kuwa hayalingani?

Kuna mtu anajali sheria ya nchi Tanzania sasa? Watu wanakwapua mabilioni ya umma, mtu anaona mwili wake mwenyewe, potelea mbalini.

Disclaimer

Siungi mkono utoaji mimba, tunajadili tupate kujua tu vichocheo vinavyowapeleka kutoa mimba.

Disclaimer ndo mpango sio....lol!

G uko sawa kwenye utii wa sheria! Ni kama tumekuwa lawless state tu sasa....kila mtu anafanya apendalo.

Wakukwiba haya, wakuua haya, alimradi fujo tupu.

mi navofahamu sababu halali ya kutoa mimba ni pamoja na pale inapohatarisha uhai wa mama, na hilo lithibitishwe na mganga.

Hivi ukibakwa na ukabeba mimba je, is it a legitimate reason to abort?

Disclaimer ndo mpango mzima.....lol

Hii ya kubakwa na kubeba mimba inategemea unataka kuitizama kiupande gani.

Sheria za Mungu

kuna madhehebu mengine yanasema uruhusiwe kutoa iwapo unahisi hutaweza kuishi na huyo mtoto kwa kumchukia, au labda jamii haitokuelewa kuwa na mtoto bila ya mume (unaruhusiwa kutoa kwa ajili ya psychological relief)

Kuna madhehebu yanayosema sheria ni msumeno, hairuhusiwi kutolewa wakati wote. Na wapo ambao hawataki watolewe mimba hata maisha ya mama yakiwa hatarini.

Sheria za Tanzania

Haziruhusu utoaji mimba kwa sababu ya mtu kubakwa (I stand to be corrected). Inaruhusu iwapo maisha ya mama yako hatarini, na daktari akaidhinisha kutolewa kwa mimba hiyo tu.

Sheria nchi za zilizoendelea.

Wengine wanaruhusu utoaji bila hata ya sababu ya msingi kama hiyo.

Wanawake wengi wanatoa mimba, kuna kituo kimoja maarufu kipo jirani na soko la mahakama ya ndizi pale jirani na kona ya mabibo kuelekea NIT.
Kuna madaktari ambao wako full time kwa kazi hizo.
Ni hatari sana kwa afya za wenye ujauzito hata kama zoezi litakuwa successfully. Kwa sababu mazingira ni ya kificho,mambo ya usafi yanakuwa hayazingatiwi sana. Sharing of abortion tools is not an optional!!!
Suala la ku legalise abortion kama ilivyo prostitution ni gumu sana kulitolea maamuzi. Japo kuna baadhi ya activists wanapigania hii kitu iwe legalised.

Naamini kuna occasions-rarely I admit- zinazolazimisha mimba kutolewa ambazo afya ya mama inakuwa hatarini.

Mimba iruhusiwe kutolewa kwenye situations kama hizo na kila ikiwa changa ni bora zaidi.

Ni kweli kabisa kama mtu anapata tubuar pregancy hapa ni lazima wa-ternimate kwa ajili ya afya ya mama ila kuna mtu naye mfahamu ambaye alikuwa na tubular pregnancy na walimpa uchaguzi wa ku-plant kwenye tumbo la uzazi au kutupa viseli. Yeye alichagua kuplant, katoto kake sasa ni ka six grader.

G bado kidogo na ww ungechelewa kuiweka hiyo dislaimer....bahati yako!

Sasa hapo kwenye kutoa mimba ili upate psychological relief hapo....kitendo chenyewe cha kutoa mimba si tayari kinaweza kumpa mtu tatizo la kisaikolojia?

Au tatizo hilo linakuwa si long lasting kama vile kumzaa mtoto na kuwa nae for the rest of your life?

Sio sawa hata kidogo..labda kwa sababu za kiafya pekee.

Kama mtu aliweza kufurahia starehe yake bila kufikiria nini kinaweza kutokea bila yeye kua mwangalifu basi inabidi apokee na kukubali jukumu la kuzaa iwapo litajitokeza. After all...kila mwenye akili timamu anajua kabisa nini kinaweza kutokea akifanya mapenzi bila kinga...kwahiyo kama kweli hana nia wala mawazo ya kuitwa mama karibuni ni vizuri akawa mwangalifu au asifanye mapenzi kabisa.

Sio starehe apatr mwingine na adhabu apate mwingine.

Back
Top Bottom