mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,607
- 1,596
Habari wadau,
Kuna hili jambo nalifikiria
Mwalimu Nyerere aliweza kuandaa vijana wengi kuwa viongozi wa badae nchini Tanzania na hata nchi jirani na alifanikiwa kwa asilimia kubwa
aliandaa viongozi wengi ambao watakuja kuongoza nchi katika nafasi mbalimbali za uongozi katika Taifa, nafasi kama Rais n.k
alifanya kazi hii kubwa ya kuandaa vijana kuwa viongozi wa badae tangu akiwa Mwenyekiti wa TANU na hata badae ilipoanzishwa CCM.
Lengo la Mwalimu Nyerere lilikuwa kuandaa viongozi watiifu, wazalendo na wawajibikaji kwa Taifa na wananchi pia Mwalimu Nyerere aliwaandaa vijana kuwa viongozi wa badae ili waendane na falsafa na kanuni za Mwalimu Nyerere mwenyewe binafsi na pia vijana waendane na falsafa za chama kuanzia TANU hadi CCM.
Wengi wa vijana walioandaliwa na Mwalimu Nyerere walifanikiwa kufikia malengo ya Mwalim Nyerere na Chama kwa kuwa viongozi kabla hawajachafuka na mambo mbalimbali kama ufisadi, rushwa n.k
Mfano wa vijana waliondaliwa na Mwalimu Nyerere pamoja na Chama ni pamoja na Mkapa, Kikwete Sr, Sita Sr, Makamba Sr, Warioba n.k pia inasemekana aliwaandaa viongozi wa nchi jirani kama Uganda, Rwanda na Burundi.
Hoja hapa ni kwamba kwanini viongozi wengine wameshindwa kuandaa vijana wa badae mfano tulikuwa tunajua Rais anaekuja baada ya Mkapa kutokana na Nyerere.
Mfano Mzee Mwinyi ajaandaa vijana wengi kama alivyoaandaa Mwalimu Nyerere kipindi cha uongozi wake bali tunamuona Hussein Mwinyi tu ambaye ni mtoto wake.
Kuhusu mzee Mkapa sina uhakika kama alimuandaa Raisi Magufuli au imetokea kama bahati tu, wengi wa vijana aliowaandaa wameishia kuchafuka kwa ufisadi na rushwa kabla hawajafikia malengo.
Pia Mzee Kikwete nae kaishia kumuandaa mtoto wake Ridhiwan, ila vijana wengi aliowaandaa wameishia kwenye ufisadi, rushwa, jeuri n.k mfano ni Nape, Makamba Jr, Makonda, Jerry Slaa n.k
Swali ni kwanini viongozi kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete wameshindwa kuandaa viongozi wa uhakika wa badae kama alivyofanya Mwalimu Nyerere sababu naona wengi wa vijana walioandaliwa wameishia kukengeuka na ufisadi, rushwa, kutowajibika, jeuri n.k
hoja hapa ni kwamba Tanzania hatujui hatma yetu ya uongozi wa nchi kwa badae sababu hakuna viongozi wazalendo wanaonekana kuandaliwa kuja kuongoza nchi.
Binafsi naona hili ni tatizo sababu ni rahisi kupata viongozi mamluki wa nchi jirani.
Hapa sizungumzii CCM pekee bali na vyama vyote ikiwemo UDP, ACT, Chadema, CUF, TLP je wanautaratibu gani wa kuandaa vijana wazalendo wanaoweza kuongoza Taifa hili hapo badae?
Sent using Jamii Forums mobile app