Warithi wa Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli

Warithi wa Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli

Umeandika hoja nzuri ndugu,
Ila je, tutumie mfumo gani kama nchi ili tuweze kupata viongozi wazuri katika nchi hapo badae?
Je kuna mfumo wa siri wa kupata viongozi ambao raia wa kawaida hatuufahamu?
au tusubiri kupata viongozi kutoka kwa watoto, wajukuu na ndugu wa Mwinyi, Karume, Mkapa, Shein, Kikwete, Magufuli n.k?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nchi yetu ipo nyuma sana katika talent management, huko mashuleni na mitaani watu charismatic wapo ila hakuna mfumo wa kuwapata na kuwakuza mkuu...

Mbaya zaidi mfumo mzima unalazimisha watu wawe na vyama na kuingia katika cheap politics. Big brains na wanaojiweza hawawezi kuingia huku

Kuna chances kama ukurugenzi na ukuu wa wilaya ambazo ni ngazi nzuri za watu kuandaliwa na kuibuliwa kiuwezo lakini bado zinapewa kwa wafuasi wa vyama

Naona uchama utoke na hilo ni la muhimu
 
Tatizo kubwa ni Inteligence system yetu. Marais hawana haja ya kuandaliwa bali wanasiasa wanatakiwa kuachiwa uwanja huru na nafasi sawa wajinadi wawezavyo, ili mwisho wa siku system za nchi zifanye upembuzi yakinifu.

Shida yetu kubwa ni kuwa tuna inteligence system mbovu ambayo haina uwezo wa kuwafanyia vetting wagombea kujua yupi ni mamluki na yupi si mamluki.

Unforgetable
Pia tulitakiwa tuwe na DNA center kuepuka kuongozwa na wakimbizi wakatuletea tabia zisizo za kitanzania Tiss iko bize kulinda cccm kuliko utaifa.
 
Mambo ya vetting. Nikizidisha zaidi ya nilichoandika, nitaharibu, hivyo nawasilisha.
 
Tatizo kubwa ni Inteligence system yetu. Marais hawana haja ya kuandaliwa bali wanasiasa wanatakiwa kuachiwa uwanja huru na nafasi sawa wajinadi wawezavyo, ili mwisho wa siku system za nchi zifanye upembuzi yakinifu.

Shida yetu kubwa ni kuwa tuna inteligence system mbovu ambayo haina uwezo wa kuwafanyia vetting wagombea kujua yupi ni mamluki na yupi si mamluki.

Unforgetable

..mimi naomba kwa heshima kabisa nitofautiane na wewe kuhusu ushiriki wa "intelligence system" ktk masuala ya siasa.

..unapopendekeza intelligence system ifanye vetting ya wanasiasa, Je nani anawa-vet watu wa intelligence system?

..Ushauri wangu ni kuwa tuboreshe mfumo wetu wa ELIMU. watoto wetu wafundishwe uadilifu, utu, na kuipenda nchi yao tangu wakiwa mashuleni.

..Vilevile tuweke mfumo na taratibu zinazozuia fedha na rushwa kuwa kikwazo cha wenye nia kuingia ktk siasa na uongozi.

..lingine ni kuweka sheria za maadili ya viongozi na kuvipa nguvu vyombo vyetu ku-enforce sheria hizo. Viongozi lazima waogope kuvunja sheria na wawe na uhakika kwamba hakuna aliye juu ya sheria.

..Mwisho, wananchi tunatakiwa tuwe na mwamko wa kuchagua viongozi wenye maadili na wanaozingati sheria na utawala bora.
 
Kikubwa hapo mkuu mitindo huru ni watawala wawape freedom of expression, damu changa zishiriki kwenye vikao na ngazi kuu za maamuzi kuanzia ndani ya vyama na serikalini.
Kiujumla watawala wabadilike wawe na mitazamo ya kizalendo zaidi ili damu changa iige na kurithi yaliyo mema.
Bunge liwe huru ili wananchi waanze kuwamulika mapema viongozi wanaochipukia.
Vyama vya siasa vipewe uhuru wa mikutano na pia viongozi wa vyama wawape nafasi vijana wenye talanta ya uongozi na wawalee vyema waje kuwa watawala wazuri.
Mawazo mazuri kabisa haya,
Lakini Nyerere alifanikiwa kuandaa vijana wengi kwenye uongozi na baadhi tumelishaona matunda yao,
Kikwete aliruhusu siasa ifanyike kwa upana lakini bado hatukufanikiwa kupata vijana wengi kwenye uongozi na matokeo yake ni kuzalisha vijana wenye ufisadi, rushwa, jeuri n.k

Kuna vitu inatubidi tuendelee kutafakari ili tuweze kupata vijana wazuri kwenye uongozi kwa ajili ya Taifa baadae


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unahisi kwamba kuna uwezekano wa kupatikana kwa kiongozi mkubwa wa nchi ,kwa ngazi ya mkuu wa nchi alafu akawa mamluki?
Ndiyo inawezekana,
Marekani walishawai pandikiza raisi mamluki Urusi, raisi huyo ndiyo aliyesababisha kuanguka kwa USSR kipindi hicho kwa kuanzisha sera zilizokua tofauti na misingi ya USSR kipindi hicho.
Hivyo ni muhimu tukaendelea kutafakari misingi mizuri ya kutumia ili kuandaa viongozi wa badae katika nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi yetu ipo nyuma sana katika talent management, huko mashuleni na mitaani watu charismatic wapo ila hakuna mfumo wa kuwapata na kuwakuza mkuu...

Mbaya zaidi mfumo mzima unalazimisha watu wawe na vyama na kuingia katika cheap politics. Big brains na wanaojiweza hawawezi kuingia huku

Kuna chances kama ukurugenzi na ukuu wa wilaya ambazo ni ngazi nzuri za watu kuandaliwa na kuibuliwa kiuwezo lakini bado zinapewa kwa wafuasi wa vyama

Naona uchama utoke na hilo ni la muhimu
Umeongea point kubwa sana ndugu,
Nafikiri viongozi wa sasa wa siasa na vyama mbalimbali, hasa Raisi Magufuli aanzishe mifumo mizuri ya kuandaa viongozi watiifu na wazalendo kwa badae ili kuendelea kulinda misingi ya Taifa na nchi kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mambo yamebadilika sana! vijana walioandaliwa kipindi cha Kikwete ilikuwa ni kubebana na kujuana. Wengi hawakuwa na uzalendo ndani yake na mbaya zaidi rushwa ilitamalaki kuanzia ngazi ya juu kabisa ya utawala. Vijana waandaliwa walipikwa kuwa wanamtandao na hatimae wakajifunza ubinafsi na uroho wa kujilimbikizia mali make watawala waliwakumbatia.

Ukiachana na hilo wapo vijana wachache sana ambao kwamtazamo wangu wangekuja kuwa vingozi wazuri tu mathalani akina Francis Mawazo, Ben Sanane, Mtatiro, Zitto, Mnyika n.k baadhi yao harakati zao zilivurugwa na au kuuawa kutokana na udharimu wa watawala wa nchi ama ndani ya vyama vyao.

Usitegemee kiongozi kama Mbowe akuache ung'ale na akupe support ili baadae uje kuwa kiongozi mkubwa katika jamii pasipo kumsujudia.
Matokeo yake vijana wamegeuka kuwa wachumia tumbo na wapiga zumari wa watawala.
Umemsahau Deo Filikunjombe nae aliuawa na wanaCCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea point kubwa sana ndugu,
Nafikiri viongozi wa sasa wa siasa na vyama mbalimbali, hasa Raisi Magufuli aanzishe mifumo mizuri ya kuandaa viongozi watiifu na wazalendo kwa badae ili kuendelea kulinda misingi ya Taifa na nchi kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna mtu YOYOTE mchama ataleta mabadiliko. Only watu wasiopendezwa au kulinda ukubwa wa vyama vyao ndio wanaoweza kuweka national interest mbele
 
Habari wadau,
Kuna hili jambo nalifikiria

Mwalimu Nyerere aliweza kuandaa vijana wengi kuwa viongozi wa badae nchini Tanzania na hata nchi jirani na alifanikiwa kwa asilimia kubwa

aliandaa viongozi wengi ambao watakuja kuongoza nchi katika nafasi mbalimbali za uongozi katika Taifa, nafasi kama Rais n.k

alifanya kazi hii kubwa ya kuandaa vijana kuwa viongozi wa badae tangu akiwa Mwenyekiti wa TANU na hata badae ilipoanzishwa CCM.

Lengo la Mwalimu Nyerere lilikuwa kuandaa viongozi watiifu, wazalendo na wawajibikaji kwa Taifa na wananchi pia Mwalimu Nyerere aliwaandaa vijana kuwa viongozi wa badae ili waendane na falsafa na kanuni za Mwalimu Nyerere mwenyewe binafsi na pia vijana waendane na falsafa za chama kuanzia TANU hadi CCM.

Wengi wa vijana walioandaliwa na Mwalimu Nyerere walifanikiwa kufikia malengo ya Mwalim Nyerere na Chama kwa kuwa viongozi kabla hawajachafuka na mambo mbalimbali kama ufisadi, rushwa n.k

Mfano wa vijana waliondaliwa na Mwalimu Nyerere pamoja na Chama ni pamoja na Mkapa, Kikwete Sr, Sita Sr, Makamba Sr, Warioba n.k pia inasemekana aliwaandaa viongozi wa nchi jirani kama Uganda, Rwanda na Burundi.

Hoja hapa ni kwamba kwanini viongozi wengine wameshindwa kuandaa vijana wa badae mfano tulikuwa tunajua Rais anaekuja baada ya Mkapa kutokana na Nyerere.

Mfano Mzee Mwinyi ajaandaa vijana wengi kama alivyoaandaa Mwalimu Nyerere kipindi cha uongozi wake bali tunamuona Hussein Mwinyi tu ambaye ni mtoto wake.

Kuhusu mzee Mkapa sina uhakika kama alimuandaa Raisi Magufuli au imetokea kama bahati tu, wengi wa vijana aliowaandaa wameishia kuchafuka kwa ufisadi na rushwa kabla hawajafikia malengo.

Pia Mzee Kikwete nae kaishia kumuandaa mtoto wake Ridhiwan, ila vijana wengi aliowaandaa wameishia kwenye ufisadi, rushwa, jeuri n.k mfano ni Nape, Makamba Jr, Makonda, Jerry Slaa n.k

Swali ni kwanini viongozi kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete wameshindwa kuandaa viongozi wa uhakika wa badae kama alivyofanya Mwalimu Nyerere sababu naona wengi wa vijana walioandaliwa wameishia kukengeuka na ufisadi, rushwa, kutowajibika, jeuri n.k

hoja hapa ni kwamba Tanzania hatujui hatma yetu ya uongozi wa nchi kwa badae sababu hakuna viongozi wazalendo wanaonekana kuandaliwa kuja kuongoza nchi.

Binafsi naona hili ni tatizo sababu ni rahisi kupata viongozi mamluki wa nchi jirani.

Hapa sizungumzii CCM pekee bali na vyama vyote ikiwemo UDP, ACT, Chadema, CUF, TLP je wanautaratibu gani wa kuandaa vijana wazalendo wanaoweza kuongoza Taifa hili hapo badae?

Sent using Jamii Forums mobile app
MADA NZURI SANA MKUU TENA SANA, LAKINI JE, HAYA MAWAZO WENDA HATA YAKAPOTEA BILA JAMII KUYAONA, INAUMA SANA JAMII FORUM KUNA MAWAZO MENGI MAZURI YA KUJENGA TAIFA BORA, YANI KAMA SERIKALI INGEKUA INATIA JICHO LAKE HUKU KUSIKILIZA WANANCHI TUNGEFIKA MBALI, MIMI BINAFSI NIKITAKA HABARI ZENYE UHALISIA MAJIBU YOTE HUWA NAYAPATA JAMII FORUM.
YANI NAIAMINI JAMII FORUM KULIKO TBC, CLAUSE NA MAGAZETI. SAFI SANA MKUU, NIMEKUELEWA HOJA YAKO KWAMBA VIJANA WA TANZANIA WANATAKIWA KUANDALIWA.
HAYA MAMBO YA KUANDAA VIONGOZI YANA HISTORIA NA YANAPLAY PART KUBWA KATIKA KUENDELEZA UONGOZI BORA. MFANO KINA ALEXANDER THE GREAT HUKO ROMAN BC. ALEXANDER ALIANDALIWA NA ARISTOTLE THE GREAT PHILOSOPHER, NA AKAJA KUWA THE GREAT NI KWA SABABU ALIPEWA BUSARA YA KUTOSHA.
TUNAHITAJI VIONGOZI SMART ENOUGH TO FIT INTO COMPLEX MODERN WORLD
 
DNA center ni kituo cha kuhifadhi vinasaba vya nchi wazawa wa nchi husika kuepuka kupata Viongozi wasio RAIA wakatumika kwa maslai ya mataifa yao.Mungai aliuwa elimu yetu akiwa waziri alibadili mitaala iliyopelekea kupata vilaza wengi
Hii ni taarifa mpya kwangu, je inawezekana vinasaba vya Tanzania vikawa tofauti kabisa na Rwanda, Burundi, Kenya, Malawi, Uganda, Zambia n.k?
Sababu naona kuna mfanano wa vinasaba kati ya watu wa Kagera na nchi ya Rwanda na Burundi, pia naona kuna mfanano wa masai wa Tanzania na Kenya kule Arusha n.k
Naomba fafanua vizuri kama ikiwezekana kuhusu hii DNA centre hasa ukilinganisha na mazingira yetu ya Tanzania?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MADA NZURI SANA MKUU TENA SANA, LAKINI JE, HAYA MAWAZO WENDA HATA YAKAPOTEA BILA JAMII KUYAONA, INAUMA SANA JAMII FORUM KUNA MAWAZO MENGI MAZURI YA KUJENGA TAIFA BORA, YANI KAMA SERIKALI INGEKUA INATIA JICHO LAKE HUKU KUSIKILIZA WANANCHI TUNGEFIKA MBALI, MIMI BINAFSI NIKITAKA HABARI ZENYE UHALISIA MAJIBU YOTE HUWA NAYAPATA JAMII FORUM.
YANI NAIAMINI JAMII FORUM KULIKO TBC, CLAUSE NA MAGAZETI. SAFI SANA MKUU, NIMEKUELEWA HOJA YAKO KWAMBA VIJANA WA TANZANIA WANATAKIWA KUANDALIWA.
HAYA MAMBO YA KUANDAA VIONGOZI YANA HISTORIA NA YANAPLAY PART KUBWA KATIKA KUENDELEZA UONGOZI BORA. MFANO KINA ALEXANDER THE GREAT HUKO ROMAN BC. ALEXANDER ALIANDALIWA NA ARISTOTLE THE GREAT PHILOSOPHER, NA AKAJA KUWA THE GREAT NI KWA SABABU ALIPEWA BUSARA YA KUTOSHA.
TUNAHITAJI VIONGOZI SMART ENOUGH TO FIT INTO COMPLEX MODERN WORLD
Asante ndugu,
Kuna mda mtu unakaa na kutafakari future ya hii nchi ndio haya mawazo yanakuja.
Pia sababu nyingine ni kwamba watu wanaona uongozi ni kama jambo linalotokea bahati mbaya ndio mana mambo ya Rushwa, Ufisadi, ujeuri hauishi kwa viongozi wengi sasa.

Jambo lingine nilikuwa nafikiri nchi iwe na manifesto (sera) ya kufanya mambo kwa vipindi mfano miaka 50 hadi 200 ili kuepukana kufanya mambo hovyo kwa viongozi wakubwa wa nchi kwa maslahi yao binafsi kisiasa na sehemu walizotoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom