Warioba unageukageuka sana kuna nini unacho kiogopa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba unageukageuka sana kuna nini unacho kiogopa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Dec 9, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jaji Warioba: Hii Ni Hatari


  WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema amekerwa na tabia ya wanasiasa kupakana matope na kuonya kuwa kisingizio cha utawala bora kisitumiwe kutaka kuangusha dola zilizopo madarakani.

  "Tukosoe lakini si kupata maslahi kisiasa… naona ndiyo tabia ya sasa kupakana matope kupata maslahi kisiasa. Tusiache kupambana na rushwa, lakini tusipakane matope kwa maslahi ya siasa," Jaji Warioba aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake Oysterbay, Dar es Salaam jana.

  Sambamba na hilo, mwanasiasa huyo maarufu nchini alisema ameshitushwa na madai ya ufisadi yaliyoelekezwa kwa baadhi ya viongozi wa serikali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa."Mengine yanashitusha. Umoja wa nchi hii unaweza kufika mahali pabaya. Yaani Rais anaitwa fisadi kwa sababu hizi na zile tu.


  Huyu ni mwanadamu kama wengine, lakini ndiyo symbol (alama) ya Taifa, ukishamwita fisadi na unakwenda unazungumzia hivyo hakuna uongozi wa Taifa."Hata Mkapa aliyemtangulia anaitwa fisadi, hivi hivi tu, habari hizi zinaleta picha gani?

  Kwamba alijitajirisha yeye na ndugu zake katika miaka yake 10."Mkapa kama binadamu alikuwa na weakness zake, lakini kwa nchi hii huwezi kufuta historia yake," alisema Jaji Warioba katika mkutano ambao alizungumza kwa makini na kwa busara, huku akitumia mifano mbalimbali kujenga hoja zake mbele ya waandishi waliokuwa kimya wakimsikiliza.

  Alisema ameshangazwa na siasa iliyojitokeza katika miaka ya karibuni ya kupakana matope, ndani ya serikali na katika vyama vya siasa, akionya kuwa hiyo itaipeleka nchi pabaya.Lakini zaidi, akawataka viongozi wa serikali, wapinzani na waandishi wa habari, kujiuliza kama kweli habari hizo na mambo yanayoandikwa, ndivyo vipaumbele vya wananchi.

  "Rushwa imekuwa silaha ya kisiasa, watu wanatumia good governance (utawala bora) kutaka kuangusha utawala uliopo madarakani."Siku hizi wakubwa wakizungumzia utawala bora, ujue wanazungumzia regime change (mabadiliko ya uongozi).

  Nia yao ni kutaka kuondoa utawala ule. Angalia Irak. Sababu ya Marekani ilikuwa kumuondoa Saddam. Simtetei Saddam, lakini nia yao ilikuwa kumuondoa. Leo hii mauaji ni ya kutisha kuliko wakati mwingine wowote."Jana nimemwona Mugabe anazungumza UN.

  Wakubwa Zimbabwe wanazungumzia good governance, suluhisho ni Mugabe ang'oke, ardhi si issue, issue ni Mugabe."Good governance inatumiwa kama silaha ya kisiasa, kubadili utawala. Watu wanaamini ukiondoa utawala, rushwa itakoma, Siamini," alisema Jaji huyo aliyewahi kuwa pia Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Alisema rushwa nchini imekuwa ikiongezeka kiasi kuwa hata wananchi wa kawaida, sasa wanashiriki kwa kiasi kikubwa, lakini hiyo siyo sababu ya kuondoa utawala."Unataka regime change au kuendeleza utawala. Kwa hiyo, mnawaambia wananchi hawa ndiyo wala rushwa, wakiondoka mambo safi, mimi inanipa taabu.

  "Watu wameacha kushughulikia matatizo ya wananchi, mambo ya msingi ya wananchi. Kwa mfano, mwaka jana, tumepata tatizo la chakula na umeme, lakini badala ya kuzungumzia jinsi ya kulikabili mwaka huu, watu wako busy kuzungumzia mambo ya uongozi.

  "Wanazungumzia nani fisadi, kutueleza mambo yao ya uongozi. Vipaumbele vyetu vinaanza kupotoshwa. Maendeleo hayawezi kuletwa na viongozi na serikali.

  Yataletwa na wananchi, serikali inatunga sera tu na kuzisimamia. Yanayokuja sasa ni lawama tu," alisema na kuongeza:"Vyombo vya habari mtusaidie, utawala bora ni kitu muhimu, lakini watu wanahitaji msaada.

  Nimesikiliza Bunge hadi ikafika hoja ya Zitto, watu wanajadili masuala ya uongozi tu. Hoja inazungumzwa mazungumzo hayalengi hoja yenyewe.

  Hii concentration ya kulaumiana sijui inawasaidiaje wananchi."Alisema ameiona orodha inayodaiwa kuwa ya mafisadi wanaoitafuna nchi, lakini akasema haina jipya kwa sababu imeshawahi kuandikwa, lakini akasema ina maswali mengi.

  "Hii si ilitoka katika miezi miwili mitatu iliyopita. Ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa, ikaja nyingine kabla ya hii. Hii ndiyo current (ya sasa) ikipita, sijui itakuja nyingine."Wengine wameisambaza, wanaizungumza wananchi hawana details (maelezo ya kina).

  Siyo kitu kipya, imefanywa issue (hoja). Msingi unawezekana upo, lakini ndivyo mambo yanavyopaswa kufanywa? Unatudanganya, unachotusaidia hakionekani. Ukitazama mahakamani hatashinda, lakini politically, amepata umaarufu," alisema Jaji Warioba.

  Akizungumzia kuhusishwa kwa Rais Kikwete katika orodha hiyo, Jaji Warioba alisema: "Kwa kweli tu Rais alikuwa Waziri hapo kabla, anahusishwa kwa kusaini mikataba wakati huo".

  Kuhusu Rais mstaafu Mkapa, huku akishika tama, Jaji Warioba alisema: "Huyu alikuta mfumko wa bei ukiwa zaidi ya asilimia 30, ameondoka uko chini ya asilimia tano."Amekuta katika huduma ya afya tunategemea vipakiti vya dawa ya misaada kutoka nje, ameondoka hali ya sekta ya afya imeimarika kwa kiwango kikubwa.

  Amezikuta shule na vyuo katika hali mbaya, leo kuna mabadiliko makubwa katika elimu. Katika miundombinu, amejenga madaraja na barabara.

  "Mawasiliano yamekuwa mazuri. Hata vyombo vyenu vya habari vimeongezeka na mawasiliano ya simu leo unaweza kuzungumza hata ukiwa kijijini. Tumeshausahau uongozi wake."Alisema alifikiri kipaumbele cha viongozi wa serikali na wa upinzani na vyombo vya habari, ingekuwa ni kuhimiza suala kama kilimo ambao huu ndiyo msimu wake, badala ya kukazania kulumbana kuhusu uongozi.

  "Jana (juzi) nimemwona Mhita anazungumzia suala la mvua, nilidhani hii ndiyo message (ujumbe) ungesambazwa, lakini wangapi wanamsikiliza. Tukiwaandama viongozi hatupati maendeleo. Jana Karamagi, leo Mgonja, kesho sijui nani anakwenda mahakamani. Tukiendelea hivi sijui…," alisema."Tunavyo-behave sisi inaweza kuwa burudani kwa wananchi, lakini isilete maendeleo. Tuache tabia ya kupakana matope, haitatusukuma mbele.

  Tusiache kupambana na rushwa, lakini tusifanye hivyo kwa maslahi ya siasa," alisema.Alisema maisha ya wanaharakati na viongozi wanaopiga kelele juu ya wananchi ni bora kuliko ya wananchi, na kuonya kuwa kumeanza kujengwa tabaka miongoni mwa wanajamii.

  "Tubadilike, tuwe na vipaumbele vitakavyosaidia wengi, badala ya maslahi ya wakubwa ambayo hali zao ni nzuri," alisema Jaji Warioba na kueleza kuwa mkutano wake huo na waandishi wa habari haukuwa na shikinizo la mtu ye yote."Kawaida yangu najulikana kwa misimamo yangu.
  na serikali wala chama. Nazungumza ninachoamini," alisema Jaji Warioba katika mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yalijikita katika kuzungumzia madai yaliyotolewa na wapinzani hivi karibuni kuhusu viongozi yaliyodai wanaitafuna nchi.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi Waroba simwelewi je kuna mwenye kujua zaidi anisaidie kumwelewa ?
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Basically anakuja na some very old school argument ya kwamba rais ndiye sovereign, and like Louis wa wafaransa, the president is basically the state and can do no wrong.Therefore enough already with the ufisadi anthem for it is a threat to our statehood and some crowd control kama hizo, kashapigiwa simu na washua wanamuona yeye kidogo anaaminika wanamuambia awapigie ndogondogo zao, au anajikomba, au ni plain maji ya serikali "rais can do no wrong" (Nixon apparently believed in the same mantra)

  Watu hawamuulizi ilikuwaje wanyamwezi walimuondoa Nixon?
   
 4. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani warioba anamiaka mingapi ?,isijekuwa uzee unamsumbua lakini uongozi wa mafisadi ndio uliotufikisha hapa,yeye hajui hilo kwani bado anagharamiwa na serikali.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu hawezi kuwa ni mmoja wa mafisadi na sasa anaogopa kwamba he mighyt the next person kufika Kisutu ?Je hawezi kuwa ana anza kutuzuga huyu ?
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  .....Na tutafakari... zilikuwepo fununu kuwa atafikishwa kizimbani... naona tayari wamesham- black mail.......
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ndivyo walivyo. None of our leaders whether currents or pasts are free from "ufisadi genes" Sasa unaposema mwenzako ana makalio mekundu jiulize kwanza je wewe si miongoni mwa jamii hiyohiyo?

  - Always smart monkeys will reason why most of their fellow monkeys have "red natural seating devices"?,

  Am I different?, the answer is no, and if I continue to laugh at them, won't they tell others that I am one of them?

  Won't they expose me to those who are not one of us?, and then chase me out of the group in which we enjoy fruits of our tree ( former PM retirement benefits and my past activities which benefited me and my family)

  "Then let me show them that I am one of them without impairing my status to others that, I am not one of them"

  These are the kind of Wariobas
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Dec 9, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Vipi hii si ni ya zamani sana na tuliwahi kuijadili sana siku za nyuma. Labda mod aitafute aziunganishe. Viongozi wengi wa kisiasa Tanzania ni bomu kabisa; wana kigeu kigeu kulingana na upepo unakwenda wapi.

  Sambamba na Waryoba, Msekwa kabla ya kuukwaa u-makamu mwenyekiti (baada ya kukosa uspika) aliwahi kusikika naye akilalamika kuwa inabidi bunge lidumishe demokrasi na bla bla bla..., vitu ambavyo hakufanya wakati akiwa spika; hata hivyo, baada ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, najua tena mtizamo huo haupo tena, ndiyo maana alitoa vitisho vya matumizi ya nguvu ya dola huko Tarime.

  Nina wasiwasi kuwa pamoja na kumheshimu sana SAS, naye anayo madoa ya namna hiyohiyo. Baada ya kuukosa uraisi, kuna siku moja alitoa mada nzuri sana huko Nairobi kuhusu kuweka level ground kwa wanasiasa wote bila kujali kama wako vyama tawala au vyama vya upinzani. Hata hivyo wakati angali CCM hakuwahi kusikika kukemea jinsi serikali ilivyokuwa inatumia raslimali za serikali ili kuinufaisha CCM against vyama vya upinzani.
   
 9. M

  Mutu JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hahahaaaaaaaaa Warioba namwaminia sana ila inaonekana na yeye kuna kipindi alilambishwa kidogo mgawo fulani ili atulie.Na sasa wamemtuma "sema wewe wananchi watakusikiliza "

  Anachoongea ni sawa kuwa wasipakane matope kwa sababu za kisiasa na pia sisi hapa tunatakiwa tulione hili ndio maana tunataka wote waliohusika na ufisadi wafikishwe mahakamani.
  Kuwa tumekazania kuongelea ufisadi hatuongelei kilimo na kufanya kazi kwa bidii ni kwamba ni kweli la msingi nchi haita enda mbele bila kufanya kazi kwa bidii.Lakini je inatufaidi ni kama tunafanya kazi kwa bidii kisha kodi zetu na mapato yanaenda kwa kina wao wakina Mafisadi ambo unadai tusi concetrate sana.Sijui tone aliyekuwa akiongea nayo kwa hiyo na miss kitu,ila naona pia amesema tusiache kupambana na rushwa/ufisadi ila tusifanye kwa sababu za kisiasa.Maneno mazuri baba ila who cares kama machafuana kisiasa so long as unaufisadi utaenda kunako pilato hao wanao jificha kwa kuwa tu ndio wao wako na madaraka nao tutakuja kushitaki wakimaliza hayo madaraka ahaaaaaaaa.
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kichuguu,

  Hii ndiyo ile ile au Mzee anarudia nyimbo zake over and over again?

  Lunyungu umeitoa wapi? Date?
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii karudia tena maana kaona kadi ya Op sangara si ya kawaida sasa kaamua kupima uzito.Hii ni habari mpya mkuu
   
 12. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Muzee Warioba yuko very right!. Just read between lines, you won't need microscope to scrutinise facts. Mimi siku zote huwa sioni kwani watu wasio na upeo wanamsakama sana mzee Mkapa. I was waiting for someone like him to speak. I knew it would happen soon. It has. Twende sasa.

  Watu wengi wana-base arguments zao kwenye mikataba ya madini. Lakini hawa watu hawa hawa hawajawahi hata ku-take troubers kuangalia mikataba ya madini ya nchi zingine ikoje? Nenda Ghana, South Africa au hata Nigeria kwenye mafuta. Niambie, who gets better, Tanzania au Nigeria? Kwanini basi? Sasa hapo ndipo kwa mwenye akili anatakiwa ajue. Otherwise, hata waheshimiwa wanaishia kupayuka tu hawasemi wenyewe wana ideas gani! This is strange sana kwa njii hii!

  Watu wengi nimeona wanashangilia Yona na Mramba kufikishwa mahakamani. Hata hapa JF. Sina uhakika na kiwango cha kufikiria na kuchekecha cha watu, ila Kwa Mramba na Yona Kikwete n serikali wamekula GALASA. Bonge la loss kuwapeleka mahakamani hawa jamaa. Uwamuzi wa Mramba kusamehe kodi, kwa namna yoyote ile uko ndani ya sheria ya nchi. Wether amesamehe kidogo au sana ama kwa interests zake, nchi hii inampa nafasi kama waziri wa fedha kuamua. Kwa hiyo akiamua kifisadi au kwa interest ya nchi, ni nchi yenyewe imempa huo uwezo. Siyo lazima kila ushauri asikilize kwa kuwa yeye mwenyewe ni mchumi. Yeye ndiyo mwisho kwa ile kanuni inavyosema.

  Sasa mimi nashangaa. Badala ya kuondoa hiyo kanuni, tunamfikisha mahakamani ati katumia madaraka vibaya! Na watu wenye akili timamu hasa, wanashangalia sana! I think njii watu tulilishwa bangi sometimes ago. Hatujui tu. Haiwezi kuwa bure hii

  Baba ya yote. Maamuzi mengi ya mawaziri kama siyo maelekezo ya president basi ni maamuzi ya cabinet. Na hii kanuni za nchi. Nashangaa leo ati Yona kafanya hivi au vile wakati Cabinet ilipitisha akiwemo mweshimiwa! Bado wadanganyika wako,,, yep yep hoyeee kwa kumfikisha Yona mahakamani! Crazy as it is!

  Tuwasahuri wabunge wabadilishe kanuni. Vinginevyo, tutaishia tukishanglia daima na kuishi kwa matumaini kwamba siku za MAFISADI zinahesabika ili hali ndiyo kwanza wanaanza UFISADI

  Let's fight for change of these kanunis and madaraka. Otherwise, nchi itegemee humuliation kubwa kwenye case ya Yona/Mramba.
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Si mpya Mkuu:

   
 14. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #14
  Dec 10, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh! .... I don't think a response is needed.
   
 15. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  unahakika na hili au ndio munkari umekupanda?
   
 16. A

  Atanaye Senior Member

  #16
  Dec 10, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lunyungu

  Hii habari ni ya zamani!

  Warioba hamwogopi mtu.

  Wacha majungu, amegeuka kuwa nini?

  Muulize huyo Mkuu anaogopa nini kuwashughulikia hao mafisadi!

  Hili ni jungu!
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Heshima mkuu
  Nimevutiwa na hoja yako. Sielewi unasema nini unapotuambia kuwa tuangalie Ghana wanafanya nini kuhusu sekta ya madini. Una maana kuwa kitu watakachofanya wenzetu tuige tu hata kama ni kibaya? Una maana Mramba na Yona hawawezi kutumia udhaifu wa sheria zetu kufanya uhalifu wa kujinufaisha na kuliingizia hasara taifa? Una maana gani unaposema serikali imelamba galasa kwa kuwafikisha kina Yona na Mramba kwenye mikono ya sheria. Unaweza kueleza ni vipi mtumishi wa umma anaweza kuwa na mali za zaidi ya shilingi bilioni tano, na mjukuu wake ambaye hata hajafikisha miaka 10 anakuwa na hela za kweza kumbail babu yake, Au hizi ni porojo tu?
  Unajua kuwa issue kubwa inayotukabili sasa ni EPA, kina Mramba wamefikishwa mahakamani kwa kuliingizia hasara taifa kama kuwafumba macho watanzania, na mii naona ni njia ya kuwafanya wakwepe EPA kiujanja, the game being played is fooling international community so as they can keep on pumping money in, not really rooting out graft. Mimi niko pessmistic sana na mwenendo mzima wa EPA naona kama kuna mchezo unachezwa, lakini this does not mean that jamaa hawana la kuwajibika nalo. Hata Ben ana mengi ya kuwajibika nayo, he oversaw the masacre in Zanzibar hiyo ni kesi tosha tu, kuna uhalifu mwingine unafanyiika huku ukiwa covered na sheria, lakini hili halina maana kuwa huo si uhalifu. Sema tatizo letu ni kuwa hatuna uwezo na ubavu wa kumfikisha mahakamani mpaka walio madarakani waamue.
   
 18. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kipunguni ....maneno hayo........KAZI IPO.
  JF where we dare to talk openly.
   
 19. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 20. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  .........I don't thnk you need to read something you don't understang.........
   
Loading...