Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
That is very true.Tuko nyuma yako Mzee Waryoba. Katu hatutakubali mawazo yetu kuchakachuliwa.
Hata hivyo upo ushahidi beyond reasonable doubt, unaotuthibitishia kuwa toka awali CCM hawakuwa na nia ya dhati kwa nchi yetu tupate katiba mpya.
Kwa wenye kumbukumbu, baada ya kutoka kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na shinikizo lilipokuwa kubwa kutoka kwa vyama vya siasa vya upinzani na kutoka kwa wanaharakati mbalimbali la kutaka katiba mpya, si mnakumbuka kauli zilizokuwa zikitolewa na aliyekuwa waziri wa sheria na katiba Celina Kombani na AG Werema, kuwa nchi yetu haihitaji kuwa na katiba mpya, bali inapaswa kuendelea na katiba yetu ya mwaka 1977 na tuendelee pale inapobidi, kuiwekea viraka visivyo na mwisho?!
Hivi kwa yeyote alifuatilia katiba hiyo iliyopendekezwa na wabunge wa CCM, ikisomwa na Andrew Chenge, hivi unaweza kweli kusema kuwa hiyo ni katiba mpya yenye maoni ya wananchi yaliyowasilishwa kwa Tume ya Warioba, au ni katiba yetu ya mwaka 1977, iliyojazwa viraka kibao?
Jibu unalo wewe unayefuatilia mwenendo wa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.