Warioba na Tume yake wajiunga na Upinzani

Warioba na Tume yake wajiunga na Upinzani

Mzee Wrioba Mungu akujalie na wajume wote pasiwepo na mauaji tena kama ya mvungi ili muweze kuzunguka na kuhabarisha wananchi jinsi BMK ya Sitta na Kikwete walivyozika rasmu ya wananchi
 
"Siku moja akatokea kiongozi wa Taifa letu, akatuambia huko nje kuna hela nyingi kuliko hapa nyumbani, mwambieni wewe ni mpumbavu" Mwalimu J.K. Nyerere.

"Kama kuna mtu ambaye anaamini nchi hii inaweza kuendelea kwa kusaidiwa, anajidanganya, Narudiia tena, Katika nchi hii kama kuna kiongozi anaamini nchi inaweza kuendelea kwa kupewa misaada, anajidanganya" Benjamin Mkapa.

"Unapoenda kuomba siyo kwamba wewe unapenda tu kuomba. Huko nje kuna mataifa yenye hela nyingi tu, unachotakiwa ni kujieleza, wakikuelewa, watakupa" Jakaya Kikwete.
 
Maandishi ya kijinga kabisa!
G Sam, achana na wapuuzi kama Happy Feet, safari hii kitaeleweka tu Tanzania. Wezi na wajinga wameichezea hili taifa kwa muda wa kutosha, wakiitafuna kama vile nchi haina wenyewe. Fallout is on the horizon, kuna walafi watatamani watapike waliyokuwa wakiyabugia kama walevi. Eti leo fisadi kama Chenge ndiye anapewa hadhi ya kuwasilisha rasimu ya Katiba, my God!
 
Last edited by a moderator:
sikumbuki katika nchi hii kuwepo tume yoyote ya serikali ya kupata maoni ya wananchi kushinikiza serikali kukubali maoni yake. sikuamini masikio yangu baada ya kumsikia mzee warioba akisema yeye na tume yake wataenda kwa wananchi kupinga bmk. hatua kama hiyo ni kinyume na maadili na inaelekea huyu mzee hakua na nia njema. bmk liko kisheria na hata mahakama imethibitisha. hatua ya warioba kwanza inaweza kua ni uvunjaji wa sheria na inaweza kwa kiasi kikubwa kushusha hadhi yake.

Kumbuka kuwa Warioba pamoja na wajumbe wengine wa tume ile aliyeiongoza walikuwa na bado ni Watanzania. Hivyo basi walikuwa ni Watanzania kwanza hata kabla ya kuteuliwa kuwa wajumbe au sio?. Hivyo basi wana haki zao za kimsingi kabisa katika kupinga hiyo rasimu ya mwisho kama Watanzania wengine wowote tu.

Kumbuka pia utumishi wao kama wajumbe wa Tume ya kusaka maoni ulishakoma toka siku ile Rasimu ilipowasilishwa bungeni. Hivyo ni sasa ni Watanzania hutu na hawawajibiki kwa taasisi yeyote wala kufungwa na kifungo cha aina yeyote ile iwe ni katika kutoa maoni yao au kuonyesha hisia zao kama watanzania wengine wafanyavyo. Ni haki zao za msingi na kikatiba. Unaona demokrasia ilivyo hapo?

Nii hayo tu na ni katika kuelemishana tu.
 
Ulivyo huna hoja wp nimesema warioba kaandika katiba? Ngoja nikuulize jaji warioba haya maoni ya kuchangia katiba alikuwa peke yake unavyo mkosoa? Walicho kikosea wakakataa kukitolea ufafanuzi ni kipi au ni kitu gani haswa kinacho wanyima watanzania wawe tofauti na tume ya warioba?
Wewe una lako jambo na wananchi wa tanzania.
Leave alone of some impracticalities on the draft, the law was clear on the role of the parliament, and where the draft committee ceases. Kilichobaki ni kuamua tu kuleta ubishi na malalamiko ya kujitungia, sasa mtu anaejitungia mchana kweupe sijui unamsaidiaje.

Nikukuuliza ni kipi hasa kinampa legitimate Jaji Warioba kupinga maamuzi ya bunge la katiba katika mwongozo uliowekwa wakupata katiba (sheria ya mabadiliko ya katiba) maana si kujiamulia tu wakati kuna utaratibu uliompa yeye nafasi na ni wapi bunge limekosea again kwa mwongozo huo huo.

Ni vyema tukajifunza kueshimu taratibu za kuendeshwa kwa nchi, si kila kitu kitatupendezea wote regardless rules are rules and so are duties, mbona akulazimishwa yeye kutoa frame work itakayo wafurahisha wengine, kwanini akatae kazi ya wengine iliyowekwa kisheria tena inayoenda amuliwa na wananchi; na amna mtu aliewaambia UKAWA wasiingie bungeni. Kwa hivyo leo ataka kama kuna mengine ayatufurahishi lazima tueshimu rules of the game ambazo halali kisheria.
 
G Sam, achana na wapuuzi kama Happy Feet, safari hii kitaeleweka tu Tanzania. Wezi na wajinga wameichezea hili taifa kwa muda wa kutosha, wakiitafuna kama vile nchi haina wenyewe. Fallout is on the horizon, kuna walafi watatamani watapike waliyokuwa wakiyabugia kama walevi. Eti leo fisadi kama Chenge ndiye anapewa hadhi ya kuwasilisha rasimu ya Katiba, my God!
Ingekuwa vizuri kama ungekosoa mfumo wa usimamizi uliopendekezwa na mianya ya ufisadi itakayo jitokeza. Lakini sioni mchakato wa katiba unahusiana vipi na concerns zako za hii post.
 
Swala la msingi hapa ni kujiuliza hii rasimu iliyoandikwa na BMK ni halali kisheria? Kama ni halali kisheria tume ya jaji Warioba imefanya kazi ambayo haitambuliki na kulindwa kisheria? Kama hivyo ndivyo BMK wangeandika rasimu wao.
Maswala mengine mpaka najiuliza hivi kama hawa viongozi wetu ni wa namna hii unategemea kuwa na mabadiko yoyote??
Siamini mpaka sasa jinsi rasimu ya jaji Warioba ambayo ndio hasa maoni ya wananchi yanavyodhalilishwa kupindukia na mamlaka husika kuona ni jambo la kawaida..... Truely fed up....
 
Warioba ni CCM damu damu, mwenyekiti wenu wa CCM hakumwona mtu bora wa kuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba isipokuwa Warioba…Warioba hakuchaguliwa na UKAWA…vinara wengi waliokuwa katika kamati ya kupata maoni kalibu asimia kubwa walikuwa ni CCM na wana CCM wote mliwashangilia na kumpa pongezi mwenyekiti wenu kwa uchaguzi wa busara…Mchakato wa kwanza na wa pili baada ya kumkabidhi mwenyekiti wenu wote mliusifia..sasa mwenyekiti wenu alipogeuka ktk ufunguzi wa Bunge la katiba na ninyi wote mi inarahamwe mkageuka…Kesho Mwenyekiti wenu akibadili msimamo mtamuunga tena mkono….Hivi akili yenu kwa nini mnampa mtu mmoja awafikilie nyinyi wote???
Anachofanya Warioba na baadhi ya wana CCM ni uzalendo yaani nchi mbele na chama baadae…ninyi mnaotoka povu mnaweka mbele chama na mnaliangamiza taifa….safari hii imekula kwenu
 

Attachments

  • 1411776906549.jpg
    1411776906549.jpg
    27.9 KB · Views: 141
CCM sijui katiba hiyo wanamtungia nani.

Yaaani wanadhani Watanzania ni wapuuuz wa kuweza kuwaamulia kila walitakalo wao??

Tutakutana 2015 panapo majaliwa.

Hata muibe kura safari hii ni bye bye tu.
 
mbowe akamatwe kwakauli yake aloitoa itv kuwa ataingia msituni

karibu mbowe huko msituni utatukuta huko tumetangulia tuna hamu sana na wewe tuanze pamoja maisha huko uje na familia yako lakini
 
Sikubali mawazo yangu yangu yakazimwa na watu wachache wenye uchu wa madaraka na ndio wenye ukoo wa kifalme hapa Tanzania.Mwisho wa ukoo wa kifalme umefika.
 
Namjua mpaka mama muuza anayemuuzia Warioba ile kitu iliyohalalishwa na chadema.
Ndege wafananao huruka pamoja. Na wapenda gongo wana akili na mitazamo inayofanana.
Kwa ujumla mimi namdharaaaaaaaaaauuuuuuu

Unamuathiri nini kwa kumdharau? Heshima yake kwa jamii inazidi kupanda upende usipende.
 
Ungeeleza ni sheria ipi Jaji ameivuja, kabla hujauacha wazi uroro wako.

Unajua tatizo ni kuwa humu jf na haswa jukwaa hili la great thinkers tumo mashabiki wengi wa vyama vya siasa na pia wamo wasio na uelewa wa masuala ya siasa za nchi. Wao huchangia tu hata kama michango yao haina tija na haina malipo jf. Kudai kuwa hujaona m/kiti wa kamati kushinikiza mapendekezo ya kamati yashughulikiwe haina mashiko. Kila tume itakayoundwa inagharimu fedha za wananchi hivyo m/kiti wake kama ni mzalendo kama Warioba hawezi kukubali maoni ya tume ambayo ni ya wananchi yafungiwe makabatini au yachezewe kwa faida na maslahi ya kikundi kidogo katika jamii.Uelewe tume ya jaji Warioba ilitumia shs. bilioni 60 za kodi ya wananchi. Hivyo asingeweza kukaa kimya anapoona bunge maalumu likiyaacha baadhi ya mambo muhimu waliyoyataka wananchi kuingizwa katika katiba yao. Mnaposema Warioba kajiunga na ukawa ni kukosa tu uelewa. Jaji Warioba ameungana na wananchi waliotoa maoni kama ukawa nao wanavyoungana na wananchi kwa maoni yao waliyoyatoa kwenye tume ya maoni.Sasa wao wjumbe wa bunge maalumu wanaungana na wananchi gani wakati hawajadili na kuweka katika katiba maoni yote ya wananchi ila baadhi tu.Umeisoma tafsiri ya sheria iliyotolewa na mahakama kuu kuhusu mamlaka ya bunge hilo kama ilivyoombwa na Saidi Kubenea? Tatizo la viongozi wa nchi hii ni kuchakachua kila kitu na suala linapopelekwa mahakamani na kutolewa tafsiri wanapigwa chini. Umesikia hukumu ya uchaguzi wa wabunge wa bunge la A.Mashariki kama ilivyoombwa na Komu wa Chadema? Hapo tena serikali imepigwa chini. Komu akikomaa na mahakama za nchini hapa wabunge wetu kwenye bunge la A.Mashariki wanaweza kipigwa chini. Kama ulifuatilia matokeo ya kipima joto kilichoendeshwa na Itv kuhusu rasimu ya katiba kukidhi matarajio ya wananchi asilimia 86 walisema haikidhi. Jee ikipelekwa kwa wananchi hata kama rushwa itatumika itapita kwa theluthi mbili zinazotakiwa kisheria? Kwa kumalizia naona na wengi wanaona ni vizuri jaji Warioba akaenda kwa wananchi mkono mmoja ukiwa na maoni waliopendekeza wananchi na mwingine ukiwa na rasimu ya bunge maalum wananchi waamue ni kipi walichopendekeza.Wote wanaodiriki kumwita mwasisi na nguli huyu wa siasa za nchi hii eti kaehuka, ana laana, eti hanq haki ya kuyazungumzia tena haya kwa kuwa alishakabidhi rasimu naona wao wanasumbuliwa na upofu,njaa,uelewa mdogo na ushabiki tu. Lazima awepo wa kuwatetea wananchi na kukemea.
 
Huwa nikikaa Na kufikiria, naona hakuna kazi mbaya na ya kinafiki kama siasa. Nakumbuka mwaka 2011 wakati kamati ya bunge ya katika,sheria na utawala inakusanya maoni ya sheria ya mabadiliko ya katiba pale Karimjee hall, Lissu alikusanya wanafunzi wa vyuo kuja kumzomea Waryoba. Na walimzomea mzee wa watu mpaka ikawa aibu kwelikweli. Leo ninapoambiwa hao watu wawili wanasafiri mtumbwi mmoja,sielewi. Surely, politics is a dirty game.
 
Huwa nikikaa Na kufikiria, naona hakuna kazi mbaya na ya kinafiki kama siasa. Nakumbuka mwaka 2011 wakati kamati ya bunge ya katika,sheria na utawala inakusanya maoni ya sheria ya mabadiliko ya katiba pale Karimjee hall, Lissu alikusanya wanafunzi wa vyuo kuja kumzomea Waryoba. Na walimzomea mzee wa watu mpaka ikawa aibu kwelikweli. Leo ninapoambiwa hao watu wawili wanasafiri mtumbwi mmoja,sielewi. Surely, politics is a dirty game.

WARIOBA alikua hajajitambua na sasa ameshajitambua na ameiona KWELI kwahiyo usishangae wameelewana
 
G Sam, achana na wapuuzi kama Happy Feet, safari hii kitaeleweka tu Tanzania. Wezi na wajinga wameichezea hili taifa kwa muda wa kutosha, wakiitafuna kama vile nchi haina wenyewe. Fallout is on the horizon, kuna walafi watatamani watapike waliyokuwa wakiyabugia kama walevi. Eti leo fisadi kama Chenge ndiye anapewa hadhi ya kuwasilisha rasimu ya Katiba, my God!

umemsahau na yule mwali KIZEE KIBOGOYO Baba KINJE
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom