Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani

Ni kweli wahenga walisema sikio la kufa halisikii dawa
hii ilitokana na kuwa kitu kinachokaribia kufa hata ukifanyie nini hakiwezi kufufuka tena

kuna baadhi ya madaktari huwaambia wagonjwa wao moja kwa moja kuwa hawawezi kupona maradhi yanayowakabili na hivyo kuwashauri waanze kuandika wosia.

Kutokana na hali ilivyo sasa chama cha ccm kinatakiwa kianze kuandika wosia wa jinsi maziko yake yanavyotakiwa kuwa.

Kwa miaka yote zaidi ya 50 wameshindwa kutoa matumaini kwa watanzania,
wameshindwa kuonyesha upi ni uhai wa nchi

hiyo ni dalili ya juu kabisa ya kufa kwa chama cha siasa.

Watanzania tuipige chini ccm 2015
 
Umesema kweli ndugu, ila mimi nataka tuipige ccm shimoni, siyo chini!
 
Mpaka sasa wameshakuwa wapinzani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…