Ric gifted
New Member
- Dec 21, 2015
- 4
- 0
Natumai u mzima sana wa afya Dada yangu mpendwa, mie ni bukheri wa afya namshukuru MUNGU kwa kutujalia uzima mpaka sasa tupo mwishoni mwa mwaka.Dada yangu mpendwa,naandika waraka huu nikiwa na majonzi tele juu yako! Duniani kote ndoa ni tendo la baraka na heshima tele,lakini najiuliza kwako kikwazo nini? Elimu unayo yakutosha, uzuri maulana alikutunuku, hata tabia yako mujaarabu. Sio kama naandika Haya kukubeza wala kukusema lengo langu haswaa ni kukumbusha kuwa `Mambo hufika mwisho`,lazima hali yako ya u single ifike mwisho Dada yangu kipenzi.
Nakumbuka Dada yangu uliwahi kupata kijana aliyekuwa na wajihi wakuvutia,kifua kipana(wenyewe mwaita six pack),aliyeishia kukupeleka samaki samaki,mlimani city na beach kwenda kuogelea, siukumbuki mwisho wa mahaba yenu ila hamkudumu, yupo kijana yule wa kilokole aliyekufuata kwa heshima na taadhima lakini ukamwanga kwa sababu eti hakuwa na swaga unazozitaka.Dada yangu,Mimi kaka yako ni mwanaume hivyo najua vipaumbele vyetu pindi tutafutapo wanawake wakuoa.
Dada yangu kwa tabia ya kujadili zaidi story za social media, Mara ooh Wema kafulia, Diamond kachepuka,na kujua zaidi series za movies kuliko kujadili mbinu za kujiongezea vipato,unadhani kuna mwanaume mwenye malengo yake atakufuata? Dada yangu kipenzi kwa tabia yako hii yakufuga kucha za bandia na nywele za maiti nadhani utaendelea kuwapata wale wenye vifua vipana kama salender brigde ambao wataishia kukupeleka mlimani city,lakini husband material wakukupeleka madare kukuonyesha viwanja na apartment utaendelea kuwaota.
Badilika Dada yangu,usimdharau mwanaume yeyote yule kumbuka Ardhi ililaaniwa kwa yake ili apate lazima atoke jasho na pia kumbuka `Mwanaume huchekwa akishafariki`lakini akiwa hai usijaribu kumcheka kwani mafanikio huletwa na juhudi zake.Dada yangu ninayo mengi ya kukwambia ila kwa Leo naishia hapa.Nasikia umenunua smartphone hivyo bhas kwa sasa unatumia email mpya,usisite kunitafuta kwa email yangu www.giftedlawyer@gmail.com.Nimekuandia waraka huu uwe taa yako kwa mwaka ujao.Ni Mimi kaka yako NIKUPENDAE BILA UFISI WALA UFISADI