Waraka wa TAMSYA kwa vyombo vya habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa TAMSYA kwa vyombo vya habari

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kalanjadd, Jan 16, 2012.

 1. k

  kalanjadd Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  IN THE NAME OF ALLAH, THE ALL-COMPASSIONATE, ALL - MERCIFUL
  [FONT=&quot]TANZANIA MUSLIM STUDENTS AND YOUTH ASSOCIATION[/FONT][FONT=&quot] ([/FONT][FONT=&quot]TAMSYA)[/FONT][FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]HEAD OFFICE[/FONT]
  [FONT=&quot] P.O BOX 35491, [/FONT]
  [FONT=&quot] DAR ES SALAAM[/FONT]
  [FONT=&quot]TANZANIA –EAST AFRICA [/FONT] [FONT=&quot]Website: [/FONT][FONT=&quot]www.tamsya.org[/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Email: info@tamsya.org[/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Phone: +255732994703[/FONT] [FONT=&quot]Fax: +255732994703[/FONT] [FONT=&quot]Mobile: +255715 944514[/FONT]
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  NDUGU WANAHABARI
  Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote. Pili tuna kushukuruni kwa kuitikia wito wetu licha ya kuwa na majukumu mengi ya kutoa taarifa kwa wananchi.Kwa mara ya kwanza tumeamua kukutana nanyi. Nasi tunatoa taarifa yetu hii kwenu ili muifikishe kwa Watanzania na wapenda amani wote duniani. Tunakuusieni juu ya ukweli na uaminifu katika kuripoti taarifa hii.Tuna kuusieni tena kuripoti taarifa hii bila ya kupotosha maana iliyokusudiwa. Kutakuwa na nafasi ya maswali ili kuuliza ikiwa kunasehemu ambayo haikueleweka.
  NDUGU WANAHABARI
  Tuliowaita ni viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Tanzania yaani Tanzania Muslim Students & Youth Association (TAMSYA). Jumuiya yetu inatambulika kisheria na inafanya kazi zake kwa kufuata sheria za nchi.
  NDUGU WANAHABARI
  Jumuiya yetu kama inavyojieleza inashughulika na malezi ya wanafunzi wafuasi wa dini ya kiislamu waliopo katika shule, vyuo vya kati na vyuo vikuu na vijana wa kiislamu kwa ujumla. Jumuiya hii inawalingania waishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Uislamu.
  NDUGU WANAHABARI
  Tumeamua kukutana nanyi ili kuzungumzia mambo ambayo yanawapata wanafunzi waislamu waliopo kwenye shule na vyuo vya serikali kwa muda mrefu. Wanafunzi waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kuwekewa vipingamizi vya makusudi ambavyo vinasababisha kufanya vibaya katika masomo yao pindi wakiwapo shuleni.  NDUGU WANAHABARI
  Sheria ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu na kuchagua dini. Kwa mujibu wa dini yetu ya uislamu ibada haimaliziki kwa kuingia msikitini na kuswali tu bali Uislamu wenyewe ni mfumo kamili wa maisha. Ibada ni kila jambo analolifanya muislamu na linaloridhiwa na Mwenyezi Mungu likiwa katika muundo wa vitendo au kauli za dhahiri na kificho.
  NDUGU WANAHABARI
  Tumepata malalamiko kutoka kwa wanafunzi waislamu wakikatazwa kuvaa HIJABU shuleni,
  Tumepata mashitaka kutoka kwa wanafunzi waislamu wakinyimwa sehemu za kusalia/kufanya ibada ya sala katika mazingira ya shule na vyuo.
  Tumepata mashitaka juu ya kupangwa makusudi matukio mbali mbali ya shule katika nyakati za sala za waislamu. Mfano sherehe za Mahafali zinapangwa kufanyika siku za Ijumaa muda wa sala, Ratiba za mitihani vyuo vikuu hazizingatii muda wa swala ya Ijumaa .kurefusha muda wa kusimama mstarini (Parade) mpaka muda wa swala unapita.
  Wanafunzi waislamu wamekuwa wakikatazwa kuvaa kofia au kanzu baada ya muda wa masomo katika shule za bweni huku wakristo wakiwa wanashinda na Rozari masaa 24.
  Waalimu wanaofundisha somo la maarifa ya uislamu wanawekewa vikwazo mbalimbali wakati wachungaji wanapishana katika shule bila vikwazo kwenda kufundisha baibal knowledge.
  Vipindi vya dini vinawekwa katika ratiba za shule muda wa saa saba mchana siku ya ijumaa wakati ambao wanafunzi wa kiislam wanapaswa kuenda msikitini kwa ajili ya swala ijumaa.
  NDUGU WANAHABARI
  Tutatoa mifano kadhaa katika maeneo tofauti ambayo wanafunzi waislam wamefanyiwa madhila, manyanyaso na udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na kutukaniwa Mungu wao,mtume wao na kitabu chao (Quran tukufu) na TAMSYA imefuatilia bila ya mafanikio.
  SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO
  Mwanafunzi wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011 mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa shule.
  Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa na viongozi wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.Tukio hili liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu Mkoa Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.

  PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM
  Siku ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupiga picha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na haukuagiza hivyo.


  SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO
  Mkuu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. Lakini sikweli kwa kuwa zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda, Shule ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.
  SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA
  Mkuu wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa tuliyo letewa ya 17/03/2011.
  SHULE YA SEKONDARI LUGOBA
  Mwalimu aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.
  Siku ya 21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke katika chumba hicho wakati wa swala.
  Makamu Mkuu huyo alikwenda tena siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira na kundi kubwa lililo sheheni wanfunzi wakristo kwa ajili ya kuwafanyia fujo waislamu waliokuwa wakiswali. jambo ambalo lileta tafrani kubwa shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.
  SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA
  Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka kuingia msikitini.

  SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA
  Mwaka 2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu wa dini nyingine.
  Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule alileta kikundi cha kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za ibada ya kikristo.
  Wakati alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali swala tano kwani hii siyo seminari.
  Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa mavazi yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake.
  Mnamo tarehe 02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu kama kanzu kuwa ni Mashoga
  NDUGU WANAHABARI
  CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
  Madhila haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM) ambako wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua kujitowa katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia njema ya kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine, lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na kukashifiwa wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.
  NDUGU WANAHABARI
  Tukio kubwa na la kusikitisha kwa wakati huu ni hili la shule ya sekondari NDANDA iliyopo mkoa wa MTWARA wilaya ya Masasi tarafa ya Chikundi kata Mwena kijiji cha Ndanda. Mpaka hivi sasa tunapozungumza nanyi wanafunzi ishirini (20) wa kiislamu wamefukuzwa shule watano (5) wakiwa ni kidato cha tano na kumi na tano ni kidato cha sita ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa mwisho mwanzoni mwa mwezi wa pili.
  Aidha wengine waliosalimika kufukuzwa shule wamewekewa masharti magumu ya kusaini ikiwa wanataka kuendelea na shule hiyo ya serikali.Miongoni mwa masharti hayo ni kutojihusisha na dini yao wakiwa shuleni sharti ambalo linapora haki ya kikatiba ya kuabudu.
  Sababu na kosa la kufukuzwa wanafunzi hao wa kiislam likiwa ni kuuomba uongozi wa shule uwape eneo maalumu la kufanyia ibada (Msikiti) kama vile walivyotengenezewa wanafunzi wakirsto kanisa kubwa shuleni hapo, kulalamika lugha za kashfa na dharau ambazo zinatolewa na mkuu wa shule dhidi ya wanafunzi wa kiislamu uislamu shuleni hapo.
  Kilichowaponza wanafunzi waislamu ni kupinga udini wa mkuu wa shule na upendeleo kwa wanafunzi wakristo, mfano kitendo cha mkuu wa shule kuteua viongozi wa serikali ya wanafunzi kiholela na kiupendeleo kwa wakirsto huku wakitoka nje ya shule wakishangilia na kusema Muhammad ameshindwa katika uchaguzi mwache bwana Yesu atawale shule!!! Haya yamefanyika mkuu wa shule akiyaona bila ya hata kukemea na kuwaadabisha wanafunzi wahusika jambo ambalo linaonesha wazi wazi kuwa ni mpango maalum ulio sanifiwa kwa mfumo maalum.
  NDUGU WANAHABARI
  TAMSYA mikoa, wilaya na matawi, shule na vyuo kwa muda mrefu imefanya jitihada mbalimbali za kuonana na wakuu wa shule na watendaji husika katika kadhia hizi na kuishia kupuuzwa bali na kupewa majibu ya kejeli na jeuri. Na baadhi ya wakuu wa shule kuomba msamaha na kuahidi kutorudia tena, lakini baada ya muda mfupi hurejea na kuendeleza dhulma na madhila kwa wanafunzi wakiislam kwa kasi ya ajabu.
  Pia walimu walezi wa wanafunzi wa kiislamu au hata walimu waislamu wanao thubutu kuhoji juu ya ubaguzi wa kidini pia huonekana vioja huku wakichekwa na hatimae kupewa adhabu ya kuhamishwa kituo cha kazi kiholela mfano dhahiri ni walimu wawili pekee wakiislam wa Ndanda Sekondari ambao wamefungashiwa virago vyao na kupelekwa vijiji vya mbali kosa lao likiwa ni kutaka haki itendeke baina ya wanafunzi wote, na wakati mwingine walimu waislam hujikuta wakiambulia vichapo na vipigo kama alivyofanyiwa mwalim Halima wa Ifunda sekondari pale alipopinga dhulma, uonevu na udhalilishwaji dhidi ya wanafunzi waislam shuleni hapo mwaka 2009 akajikuta anaambulia kipigo kutoka kwa mwalim wa kikristo.
  NDUGU WANAHABARI
  Hapa tumeonesha sehemu ndogo ya madhila yanayowasibu wanafunzi wa kiislam nchini kama mifano tu. kwani ni vigumu kueleza madhila ya kila shule au chuo kwa njia hii. Jambo la faraja ni kuwa kila mtanzania anajua haya hata watu wa kawaida pia.
  Kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu na baadhi ya viongozi wa serikali mfano Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mh. Benjamin Mkapa alipoulizwa juu ya hali ya uwiano wa waislamu na wasiokuwa waislam katika sekta ya elimu alikiri kuwepo matatizo na uduni kwa upande wa waislam na matatizo mengi huku akisema kuwa si kosa la serikali bali ni tatizo la kihistoria.
  Sisi wanafunzi wa kiislam Tanzania tunasema wazi na tunao ushahidi kuwa hili si tatizo la kihistoria bali ni mpango maalum uliosanifiwa na serikali ya awamu ya kwanza kwa lengo la kuwadhulumu na kuwakandamiza waislam kielimu kwa mbinu mbalimali kama hizi zilizotumiwa na uongozi wa shule ya sekondari Ndanda na wanaharakati wengine wa mfumo kiristo katika sekta zote za elimu nchini.
  Wanafunzi wa kiislamu Tanzania tunajua kuwa kitendo kilichokifanywa na mkuu wa shule ya Ndanda na Bodi ya shule pamoja na maafisa elimu cha kuwafukuza shule wanafunzi ishirini (20) wa kiislam na wengine kuwekewa masharti magumu ya kuacha wito wa dini yao ili waruhusiwe kurudi shuleni si kitendo kipya bali ni muendelezo wa dhulma ambayo walifanyiwa babu na baba zetu ambapo walilazimishwa wachague aidha kuacha dini au kusoma, Alhamdul llah tunashukuru kwa kiasi Fulani walifanya maamuzi magumu ya kulazimika kuacha kusoma na kubaki na dini yao kwani kama wangechagua la pili basi huenda nasi leo tusingekuwa katika dini ya haki ya uislam.
  Ama leo hii sisi wanafunzi wa kiislamu Tunasema kusoma ni sehemu ya dini yetu kama tulivyoamrishwa na Allah (sw) Quran (96:1-5) kwa hiyo hatutokubali tena kuacha wito wa dini yetu kwa kutenganisha dini na elimu kwani ikiwa tutafanya hivyo basi itakuwa tumefanya dhulma kubwa kabisa.
  Hapa tunawapongeza wanafunzi wa kiislam wa Ndanda sekondari kwa kujitambua na kujua haki zao za kiiman na kikatiba kwa kutoutii uongozi wa kidhulma wa shule ya ndanda pale ulipowalazimisha kuacha wito wa dini yao ili wasome, wanafunzi wa Ndanda wamefanya jambo tukufu linalopaswa kuungwa mkono na kuigwa na kila mtu mwema. Na napenda kutoa wito kwa wanafunzi wakiislam nchini kote ya kuwa wanapaswa kuwaiga na kuungana na ndugu zao zao wa Ndanda sekondari kwa kutokubali dhulma ya namna yoyote ile.
  NDUGU WANAHABARI
  Kadhia ya Ndanda ni mzito sana ambayo imegusa hisia ya kila muislam na kila mtanzania mpenda amani na haki, ukweli wa hili unathibitika wazi wazi kwa kila mwenye uhuru wa kufikiri kwani vijana wale wa kidato cha sita waliofukuzwa ni nguvu kazi muhimu sana kwa ujenzi wa taifa ambao tayari kusoma kwao wangeweza kuiokomboa jamii na taifa kiujumla.
  Lakini jambo la kusikitisha ni kuona viongozi wenye dhamana katika wizara ya elimu wakilichukulia swala hili kisiasa kinyume na uhalisia wake. Kwa kufanya ziada na uchunguzi wa kubahatisha bila umakini hatimae kutoa taarifa zilizojaa usiasa ndani yake, kuwa eti maamuzi ya bodi ya kuwafukuza wanafunzi (20) wa kiislam ni sahihi huku akieleza kuwa amefika Mtwara na kuongea na Bodi ya shule, mkuu wa shule, walimu na serikali ya wanafunzi hatimae wanafunzi wote Paredi bila ya kuwaruhusu kuuliza maswali au kutoa maoni yao hatimae kutoa hukumu.
  Hukumu hii haiwezi kuwa sahihi kwani hajawashirikisha wahusika wa upande wa pili wa mgogoro ambao ni wanafunzi wa kiislam kwa kuwasikiliza hoja zao madai yao ya msingi, huku ni kuisaliti katiba ambayo wameapa kuilinda ambayo inarususu uhuru wa kutoa mawazo na kila mmoja kuheshimiwa kwa nafasi yake. Jambo zito zaidi ni kuona naibu waziri anaungana na watu madhalimu waliovunja katiba ya nchi kwa kuwalazimisha wanafunzi kuacha wito wa dini yao ili warudi shule sharti hili linavunja katiba Ibara ya (19:1-2) kinachozungumzia uhuru wa imani na kuabudu.
  Kutokana na uzito na unyeti wa kadhia hii na madhila haya yanayoendelea kufanywa dhidi ya wanafunzi wa kiislam nchini leo hii tunapenda tuutangazie uma kuwa sasa basi hatutaki kuendelea tena kudhulumiwa na kunyanyaswa, sisi ni watanzania na tuna haki zote kama wanajamii wengine.

  Kwahiyo tumeitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya mambo yafuatayo;
  Tunaitaka wizara ya elimu kuwarejesha wanafunzi wote walofukuzwa na wengine bila masharti yeyote ndani ya siku tano (5) kuanzia tarehe 13/01/2012.
  Tunaitaka serikali kuunda Tume huru itakayo chunguza kero wanazopata wanafunzi waislamu katika shule za serikali nchi nzima.
  Tunaitaka serikali kuwawajibisha watendaji wa sekta ya elimu wanaoendekeza udini ubaguzi na unyanyasaji kwa wanafunzi wa kiislamu.
  Tunaitaka serikali ithibitishe au ikanushe juu ya madai ya mkuu wa shule Ndanda na badhi ya viongozi wa serikali kuwa mashule yaliyotaifishwa na serikali, serikali inamiliki majengo tu ama ardhi na mamlaka ya matumizi yake yako chini ya Taasisi zake za asili.
  Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa ajili ya watu wa dini zote.
  Asilimia kubwa ya wakuu washule za sekondari za serikali ni wakristo, hivyo basi tunaomba serikali iweke mgawanyo sawa wa nafasi hizo.
  Kila jambo linapaswa kuwa na mwisho, hatuwezi kuendelelea kuvumilia uonevu wa wazi wazi siku zote.Hatuwezi tena kuendelea kuishi kama wanafunzi daraja la pili katika nchi yetu. Lazima haki sawa na uhuru upatikane kwa wanafunzi wa dini zote na sio kukandamiza waislamu. Hivyo basi tunalazimika kupaza sauti zetu kwa kuingia barabarani kuonesha hisia zetu katika hali ya unyonge wetu
  NDUGU WANAHABARI
  Tunakusudia kufanya maandamano ya amani nchi nzima 20 Januari 2012 ambayo yatapeleka ujumbe kwa kila kiongozi wa Elimu katika mkoa yaani Afisa Elimu Mkoa na waislam wa Mkoa wa Dar es salaam watapeleka ujumbe moja kwa moja kwa waziri wa elimu.Kwa lengo la kutaka azingatie madai yetu ya kutonyanyaswa na kubaguliwa katika shule ya serikali.Lakini hatutoishia katika maandamano iwapo hali ya ubaguzi haitokoma.Tutatumia njia nyingine za kujikomboa katika madhila haya.
  Tunasema “tumenyanyaswa,tumedhaliliswa, tumebaguliwa kwa miaka 50 ya uhuru na tukavumilia na kusubiri vyakutosha leo tunasema inatosha na tumechoka tunaitaka serikali itambue haki,heshima na utu wetu kama wanavyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine mashuleni na mavyuoni.”
  Tunataka tuheshimiwe kama wanaadamu, kama wanatanzania huru, wanafunzi halali mashuleni na vyuoni kama wananyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine. Tumeanza muda mrefu kudai haki zetu kwa njia za kidiplomasia lakini hatujasikilizwa na leo tunatumia njia nyingine ya kidiplomasia na kikatiba ambayo ni MAANDAMANO ya amani huenda kwa njia hii serikali na jamii itasikia kilio chetu. ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI.

  Ahsanteni. JAFARI SAIDI MNEKE RAISI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA WA KIISLAMU TANZANIA (TAMSYA)
   
 2. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi kila kikundi au jumuiya ya kikundi chochote kikiipa au kuitaka serikali kufanya mambo wayatakayo patakalika kweli!!!!!!!!!!!!!!!1 Serikali ina mambo mengi ya kufanya na sio kwa vikundi na kama haitoshi kwa mtoe taarifa za upande mmoja mmoja? mngeweka na upande wa pili wa hizo shule wamejibu nini baada ya ninyi kufuatilia,saikolojia inahitajika hapa.
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  • Kabla ya kutishia maandamano ndugu zangu Waislamu, toeni elimu kwa umma. Kwa kuwa baadhi ya matukio ninayoyasoma hapa hayatokani na walimu/maafisa/wanafunzi kuwa "Wakristo" bali yanatokana na ufinyu na uelewa mdogo kuhusu baadhi ya mambo. Mf. kuingia msikitini wakiwa wamevaa viatu.
  • Hivi tukizungumza rationally, suluhisho la Ndanda Sekondari baada ya kutaifishwa llikuwa ni kuvunja kanisa lile lililokuwepo au kujenga msikiti? Kwa kuwa shule ile haikujengwa kwa ajili ya wote (I stand to be corrected), ilijengwa na makasisi waKatoliki kwa ajili yao na malengo na nia walizokuwa nazo wakati huo na sidhani waliwahi kufikiri kuhusu kuwepo kwa wanafunzi wa imani tofauti shuleni pale. Tatizo la kutokuwepo kwa msikiti ni mapungufu ya mfumo uliopo sasa?
  • School parade/assembly ni component muhimu sana kwa shule yeyote makini. Tuhuma kwamba muda unarefushwa hadi muda wa swala upite haina mashiko, kuna matukio yanayohitajia kuwepo kwa hali kama hiyo. Hii sio non-spontaneous issue.
  • Awali ratiba za shule nyingi zikuwa na kipindi cha dini siku ya Jumatano, ratiba ilibadilika na kupelekwa siku ya Ijumaa ili kuwapa wanafunzi Waislamu nafasi ya kuhudhuria ibada ya Ijumaa. Vinginevyo wasingepata nafasi ya swala siku ya Ijuma kwa kuwa vipindi vingeendelea kama kawaida. Najaribu kuielewa hoja, lakini sioni kama lipo suluhisho la kweli na ambalo halitaleta muingiliano wa vipindi vya kawaida vya shule.
  Ngoja niendelee kusoma na kutafakari, nitarudi. Kwa sasa senti zangu hamsini ndio hizo.
   
 4. S

  Smarty JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  watendaji wa nchi hii bana..hopeless mandazi, sijui haya maadili wanayatoa wapi? What kind of citizens (useful members of the society) are we prepring?? This country has a very long way to go....
   
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kama kila kitu anachofanya muislamu wakati wowote, yaani saa 24 za siku ni ibada basi kuna tatizo kubwa katika kuitafsiri dini hii!
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kama ni kweli haya mnayoyasema nipo pamoja nanyi.
  ila kuna madai ambayo hata nchi za kiislamu hawawezi kuyafanya kwa sababu ya mfumo wa dini.

  kuhusu maandamano viongozi wa kiislamu waliipinga chadema sana na kudai ni vurugu naomba ufafanuzi,
  je ni vurugu kwenye siasa tu?
  kwenye dini ni sawa?

  katika tanzania sikubaliani na ubaguzi wa aina yoyote uwe wa kidini au wa rangi auwa kikadila au wa kikanda ila naamini katika kutofautiana.msandawe asilazimishe serikali iwape haki ya kumiliki biashara kama wachaga,hapo itakuwa kuionea serikali na kuipa kazi isiyo ya kwa ke.
  mmetoa mfano wa mkapa si vibaya je rais aliyepo madarakani anasemaje?serikali yake ina mpango gani?je hiyo dhulma anaiona?
  kwa nini maandamano yaende wizara ya elimu?
  kama ni tatizo kweli la miaka 50 kwa nini maandamano yasiende ikulu?au kwa sababu ni muislamu mwenzetu hatutaki kumbughudhi?
  haya madai si ya kudai shulu,si ya wizara ni ya nchi na fumo kwa jumla tumkabe rais,na kwa sababu chadema ni wazoefu wa maandamano tuungane nao kupeleka malalamiko ili tuandae maandamano kani hakuna chama cha siasa kitakachoweza kudai kinataka kuwatetea watanzania wote kama kundi la dini moja kati ya wakristo au waislamu linabagiliwa.
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tatizo lenu waislam hamko pamoja leo wakija Bakwata watasema hawana taarifa ya madai yenu, jengeni kwanza umoja mnaweza kufanikiwa. Nimefurahi uliposema maandamano ni njia ya kidiplomasia, kawafundisheni wazee wenu hasa wa Dar na Bakwata hajui hilo.
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Unaona badala ya kuzungumzia matatizo yenu unakimbilia kuihusisha CDM hujui hata waliofukuzwa kuna wana Chadema mule kwa hali hii mtalalamika hadi mwisho wa dahali kwa vile adui yenu hammujui.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Heko vijana wa Kiislam kumbukeni mnatakiwa kuiondoa dhulma hiyo kwa mikono yenu na sio kuchukia moyoni. Kwani hiyo ni imani dhwaifu kwenu.

  Mola yu pamoja nanyi na sisi sote tupo pamoja kwa hilo kwani hiyo ni haki yake sio tu kisheria bali hata kibin'Adam.

  Kudai haki ni wajibu kwa sote. Haki haiombwi bali unadai.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Bakwata ni nini?
   
 11. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,366
  Trophy Points: 280
  Mko sahihi kutoa madai yenu, lakini mngejitahidi sana kutoonesha ujinga na kulialia na hasa kwenye hoja ya wanafunzi wa Ndanda
   
 12. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeona eeee! Tatizo hawa jamaa uwezo wa kufikiri ni mdogo sana,hawana reasoning hawana,wala adui yao hawamjui ni ukristu,serikali,chadema? Maana kama hujui target utapiga wapi sasa? Ni kuwapuuza tu.
   
 13. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Katiba ya Nchi Ibara ya 3.-(1) inasema hivi:Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
  my take:
  (1)Hivi huyu Mwenyekiti anapoinukuu katiba kule ndani kuhusu uhuru wa kuabudu ni sawa,lakini kwa nini anaruka hii sehemu ambayo ipo just ukurasa wa kwanza tu,tena juu kabisa?Tulitegemea aipongeze Serikali kwa Kutojenga Makanisa au Misikiti kwenye maeneo ya Shughuli za Serikali kwa sababu haina dini,lakini sasa yeye anahamasisha ujenzi wake,ukisema Elimu dunia iliwapita pembeni wanawaka kama FF na MS,why?Kumbuka Hizo Ndanda,Pugu,Tosa,Kigonsera,Mazinde,Ihungo Zilikuwa Seminary,zilijengwa kwa minajiri hiyo,kwa hiyo hata hayo Makanisa Serikali wakati imamua "KUIBA" mchana kweupe haikuwa na namna ila kuacha kila kitu kama kilivyo,lakini yenyewe haijawahi kujenga,haijengi na katu,haitathubutu kujenga any religious related block or whatever utaita katika maeneo yanayofanya shughuli zake kwa sababu haijui dini ni nini,japo watu wake kama JK ni waswali sunna wazuri tu.The same applies to say Al-Haramain,sijui Kinondoni Muslim,au pale Bondeni r-chugga,na sasa mnayo MUM,Jengeni Misikiti,ikiwezekana Mikubwa zaidi kuliko hata Ule pale Roma aliojenga Qaddafi enzi za uhai wake,au Ule wenye jina lake pale Dom,no one ever will ask you about anything,maana ni maeneo yenu ya kujidai.Kuliko kulialia tu kila siku,tutashindwa sasa kuwasaidia kimawazo,maana sometimes kama huwa mmedata kidogo mnapotoka katika press.Poleni sana.
  (2)Watu wa kulaumiwa katika Taifa hili ni wawili tu,japo kwa mtazamo wako nawe unaweza ongeza wako:
  (a)Alhadji Ally Hassani Mwinyi:Huyu akijua kabisa ni kuvunja katiba ya nchi,alitoa rai(sina hakika kama ni waraka au la hasha) kwamba Wanafunzi wa Kike wa Kiislam Wawe wanavaa Hijjab mashuleni,bila kuangalia kama ni za Serikali isiyo na Dini au ni shule zao.Sasa hata Vyuo kama Tumaini,SAUT wanavaa tu,wala hawasumbuliwi.Japo mtazamo wangu walitakiwa wavae huko kwenye Maseminary yao(Taasisi za Elimu zenye Mlengo wa dini yao).Nadhani kwa kuwa hawana basi ikabidi wavae tu hukuhuku.Lakini to me it was against Constitution.Hapa ndio Source of all blames and claims of these people began,wakidhani kumbe ni haki yetu,ila ni kuvunja katiba ya nchi.Katiba inaposema uhuru wa kuabudu ni hukohuko kwenu,sio katika mazingira ya Serikali.Hivi Freemason iki-establish openly na wao kudai haki ya kuvaa mavazi ya kutambulisha dini yao itakuwaje?Au sisi wapagani,kupiga Ulabu,benghe,unga ndio zenu mahala pa kazi,na sisi tunataka haki yetu,nadhani itoshe tu kusema hapa ndipo mambo yaliharibika.
  (2)JK huyu wa sasa.Huyu sasa amepalilia,ameweka dawa ya kuua magugu na ameweka mbolea kali sana kwenye hili suala,hii ni baada ya Uongozi kumshinda,sasa anatafuta huruma ya Jamaa zake.Huyu ni Mission accoplishment agent.Sasa kwa ushauri tu,Vijana waache kulumbana na Dini ambazo sote tumezikuta,na hata waliotuletea wanatushangaa.Ni kweli Imani yenu inasema Allah aliwateremshia Through Muhhamad SAW,sawa lakini how it comes to you those times?Mwarabu,Mzungu et al. Sisi kwa sababu hii Tumuombe Mungu /Allah atujaalie ufunuo tuone utukufu wake badala ya kukaa na kuanza kutafurtana jambo ambalo haliwezi tusaidia sana.
  Mimi vilevile nawashauri Muandamane Mwende Magogoni maana pale ni karibu sana na Wizarani,nendeni kwanza kwa JK halafu yeye atawadirect other channels,zaidi mtamuonea Ustaadh Prof.Dihenga na Alwatan sheikh Dr.Kawambwa na yule dogo Kafir Mulugo,maana watakuwa hawana majibu,wasije watia kichefuchefu kwa majibu mepesi kama Sheikh Kasim Majaliwa kule Ndanda.
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Katiba aisomwi hivyo.
  Soma ibara nzima ili ilete maana. Soma haki za kuabudu utaona hapo.

   
 15. j

  joely JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kanla ya kulalamika angalieni history ya shule husika pengine shule hizo awali kabla ya kutaifishwa zilikuwa ni za dini ndo maana kuna makanisa siamini kama serikali ndo inayojenga makanisa,
  nawakilisha
   
 16. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hivi JKT inaanza lini kwa wanafunzi? Huko nafikiri wanafunzi waliomaliza kidato cha sita hawatauliza masuala ya Rozari, hijabu n.k!
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lakin swala za ijumaa na ijumaa pili zinakuwa kama kawaida.

  Nakumbuka Ruvu tulivyokuwa tunaswali kule vibwende au kwa babu. na siku ya ijumaa Mlandizi town.
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Ilboru kuna Kanisa. Na waisilam wamepewa darasa wanalituia kama msikiti.
   
 19. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #19
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wakuu acheni kejeli haya madai ni ya msingi. Na ni kweli yametokea kama yalivyoelezwa hasa hii ya ndanda basi juhudi za dhati zinahitajika kutatua mgogoro huu.
   
 20. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #20
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa mi huwa nawashangaa,wenzao walipoona wanataka mapadri na wachungaji walio chimba dini wakajenga shule za seminary ambazo na wao wanasoma. Hizi za serikali wakatuachia sie ma easy taker. Sasa wao wanataka kuleta misimamo mikali hata huku kwetu? Si wajenge shule za waislamu tu? Mbona ardhi kubwa tu nchi hii? Nakumbuka iyunga walipewa eneo wakajenga msikiti ila wakristo walikuwa wanatoka nje ya shule kwenda kusali, hakuna anayelalamika. Mwisho watadai mpaka shule za kata zijengwe misikiti na muda wa wao kuswali masomo yasimamishwe.
   
Loading...