Mzee Kijana
JF-Expert Member
- Nov 25, 2011
- 1,405
- 1,086
....! Kudai haki kwa kupotosha ni dhambi! Serikali ya JMT haijawahi jenga kanisa wala msikiti kwenye shule ya serikali!!! NO RISECH NO RAIT TU SPIK
Acha uongo wewe!! Kuna msikiti pale Tabora Boys Secondary School. Nimesoma pale miaka minne na tulikuwa tunaruhusiwa kuswali bila bughudha. Hii ni shule ya serikali. Je, ule msikiti uliota kama uyoga? Unaposema serikali haijawahi kujenga au kuruhusu kujengwa misikiti au makanisa kwenye shule zake ni upotoshaji na kuongea bila data.Ona aibu mtu mzima kuongopa! Madai ya TAMSYA yana msingi na wakati umefika sasa wa watendaji wa serikali kufanya kazi kwa weledi badala ya kutanguliza dini zao na kubagua wanafunzi wa Kiislam kwani nao wana haki kama Wakristo kwenye nchi hii. Iweje mwanafunzi mkristo aruhusiwe kuvaa rozari na mwislam azuiwe kuvaa hijabu au kofia? Laana za Mungu ziwafikie wote wanaoendekeza dhuluma hizi kwa wanafunzi wa Kiislam kwenye mashule na vyuo vya umma nchini.