Waraka wa Lema kwa Rais: Hongera Mhariri wa gazeti la Mtanzania kwa kuuchapisha gazetini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,388
Mhariri wa gazeti hili amefanya kile ambacho hata mimi jana nilishauri Wahariri wakifanye kwa kuripoti waraka wa Lema kwa Raisi katika magazeti yao.Inawezekana kabisa Mhariri hakuona hata ushauri wangu ila kafanya hivyo kwa utashi wake ila kwa vyovyote vile bado nampongeza kwa kuona umuhimu wa kufanya hivyo katika chombo chake cha habari.

Ushauri kwa Wahariri wa Magazeti nchini

Leo gazeti la Mtanzania habari kuhusu waraka huo ndio habari kuu katika gazeti hilo.

Nampongeza Mhariri kwasababu ni wazi ule waraka haukupaswa kuishia mitandaoni tu na ulipaswa kuripotiwa pia na vyombo vya habari.

Asante Mhariri.
 
Mhariri wa gazeti hili amefanya kile ambacho hata mimi jana nilishauri Wahariri wakifanye kwa kuripoti waraka wa Lema kwa Raisi katika magazeti yao.Inawezekana Mhariri hakuona hata ushauri wangu ila kafanya hivyo kwa utashi wake ila nampongeza kwa kuona umuhimu wa kufanya hivyo katika gazeti lake.

Ushauri kwa Wahariri wa Magazeti nchini

Leo gazeti la Mtanzania habari kuhusu waraka huo ndio habari kuu katika gazeti hilo. Kwakweli ule waraka haukupaswa kuishia mitandaoni tu na ulipaswa kuripotiwa pia na vyombo vya habari.

Asante Mhariri.
Mkuu hvi ndo viwango vyako ila hapo nyuma nilikua sikuelewi.
Much thanks
 
Asante sana mhariri amefanya Jambo jema kabisa najua mweshimiwa ameupitia
 
Asante sana mhariri amefanya Jambo jema kabisa najua mweshimiwa ameupitia
Naona haya magazeti sasa wahariri wake tangu juzi wamebadilisha upepo wa kiuandishi kabisa maana tumeona Jambo leo juzi na leo hii mtanzania!
 
Nilijiulza sana ni jinsi gani ule waraka utamfikia President
Mkuu kuna watu wanafuatilia kila neno katika hii mitandao mno...Unadhani wale unaosikia wamekamatwa kwa makosa ya kutumia lugha mbaya dhidi ya Rais wanajulikanaje? So hao watu huchukua zuri na baya pia...
 
Ule waraka kama mtukufu Rais akiupata kama ulivyo, akausoma kwa utulivu,akatafakari kwa kina nina uhakika ataguswa.Ni waraka ambao umejaa busara,unyenyekevu,hekima na uzalendo uliotukuka.
Akiona kichwa cha habari na akiliona jina la Rema hawezai kuendelea kuusoma na badala yake atapuuzia mbali kabisa

Ili ujue atapuuzia mbali we fuatilia tu Bungeni wapinzani wanavyotoa ushauri mzuri sana lakn matokeo yake wanapuuzwa na matokeo yake wanatolewa nje na kupewa adhabu kabisa... Nchi hii bado sana tuzidi Kumlilia Mungu afanye mabadiliko kabisa tuliyeneye siye tuliyemtaka kabisa
 
Ule waraka kama mtukufu Rais akiupata kama ulivyo, akausoma kwa utulivu,akatafakari kwa kina nina uhakika ataguswa.Ni waraka ambao umejaa busara,unyenyekevu,hekima na uzalendo uliotukuka.
Ni vema na mkewe mama Janet naye ausome ili awe anampa kaushauri ka karibu karibu itasaidia sana.
 
Back
Top Bottom