Waraka wa Kingunge (Hayati) Kuhusu kanisa/dini.

BIGURUBE

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
6,743
4,227
A TRUE SON OF AFRICA

HISTORIA YA PHILOSOPHY ZA KINGUNGE

_"Kwangu mimi kuwa “Mwanafikra huru” ni “evolving of ideas” — “zamadamu” ya mawazo._

_"Kwamba nilibatizwa Mkristo wa Roman Catholic na nilifuata hatua zote za utaratibu wa kanisa isipokuwa tu zile za kuwa Padri,_

_Ilikuwa ni wakati wa enzi za mkoloni, mkoloni Mwingereza, sikuwepo wakati wa mkoloni Mjerumani,"_
_"Nilivyozidi kukua nilijikuta najiuliza sana maswali mengi mengi…juu ya dini, dhehebu la RC, najiuliza toka darasa la kwanza mpaka la kumi…"_

_"Nilipochaguliwa kwenda sekondari Tabora, akili yangu juu ya kuendelea kujiuliza maswali makubwa ikapanuka…"_

"Niliendelea kujiuliza maswali ya msingi kuhusu dini, utatu mtakatifu…niliuliza sana na nilipata matatizo nilipokuwa nauliza maswali kuhusu masuala hayo…"_

"Nilijiuliza kuhusu imani yangu pia…_

_Nikaacha kwenda kanisani…"_

_"Lakini pia nilikuwa najiuliza kuhusu ukoloni…maana kwa wakati ule, “upande mmoja unakutawala, upande mwingine unakulazeni”_
_"Nilitofautiana na kupata matatizo na viongozi wa kanisa katoliki…"_

"Niliambiwa kuwa mimi ni “Mkomunisti” (tukio hilo nikiwa darasa la 6)_

_…ilitangazwa kabisa kanisani, nilitengwa (ex-communicated) kwa tangazo la Padri mmoja mzungu raia wa Switzerland kwa jina Padri Clement…"_
"Baba yangu alikwenda kumuona Askofu Edger Malanja ambaye alikuwa anafanya kazi na kuishi Kigurunyembe TTC Morogoro…_

"Askofu Edgar Malanja hakuwa na taarifa, hakujua kuwa tayari Padri Clement aliisha nitenga na kanisa (ex communicated..!)_ _"Ilitangazwa, ilisemwa kuwa mimi nilikuwa ni Mkomunisti, ingawa kwa wakati huo mimi mwenyewe sikujua “ukomunisti” ni nini.!_
_"Nilitangaziwa ubaya…kuwa mimi ni mtu muovu, Mkomunisti…ndivyo ilivyotangazwa…_
_"Mkakati wa ushawishi (Lobbying) ukafanywa kwa Mkuu wa shule ili nifukuzwe shule, yote haya yalifanywa na yule Padri Mzungu Mromani katoliki raia wa Switzerland..!_
"Mkuu wa shule hakukubaliana na ushawishi huo, hakuona kwanini mambo ya kanisani yaje kushawishi mambo ya elimu ya shuleni_
_"Zaidi pia ilikuwa kwamba, shule yetu ilikuwa muda mrefu haijatoa mwanafunzi kuendelelea zaidi na masomo ya juu…ikaonekana ikiwa mimi nitafukuzwa pengine hilo halitatokea kwani nilikuwa mwanafunzi ambaye darasani nilikuwa naendelea vizuri sana na masomo yangu, hivyo nilikuwa na uwezekano mkubwa kufaulu na kuendelea mbele zaidi…_
"Na kweli nilifaulu shule ya kati (middle school), na kutoka Dar es salaam nilipokuwa nasoma (ni pale ambapo sasa ni shule ya msingi ya Uhuru), nilikwenda shule ya sekondari ya *Tabora*._
_"Baada ya hapo nikajiunga na chama cha TANU kwa harakati zake za kutafuta UHURU…_

_"Ni katika kusoma vitabu ndipo nilipokutana na vitabu hivi vya Bw Thomas Paine: “The Age of reason”, “The rights of man” na “Common sense”…_ _"Nilipenda sana kusoma vitabu na nilisoma vingi…baadhi ya vitabu vilipigwa marufuku, lakini hata hivyo navyo nilikuwa mdadisi kutaka kuvipata na kuvisoma…_
_"Huyu Tom Paine alikuwa Mwana fikra huru (Freethinker)._"Tom Paine aliuliza kuhusu imani za kidini, kuhusu pia tawala za kifalme na kimalkia (monarchy), pia alitetea mapinduzi ya Ufaransa, na aliunga mkono vita vya wamarekani kuwa taifa huru, kutoka utawala wa Mwingereza…_

_"Maandishi ya huyu bwana (Thomas Paine) yalinipeleka hatua nyingine ya juu katika kuijua dunia na jamii_
_"Yalinipaisha upeo wangu wa kuhoji mpaka ikafikia hatua ambapo kwa mambo ya imani za dini nikaanza kuwa na mtazamo tofauti..!_
_"Nilijiuliza kuhusu imani yenyewe, kumbuka nilikuwa najiuliza toka enzi za shule, nilihoji imani ya Kikristo, halafu imani za dini kwa ujumla wake, imani ya maisha baada ya kifo- jee ni kweli kama dini zinavyodai..? hata hilo nilijiuliza pia_
_"Chama cha TANU kilinipeleka Liberia mwaka 1958 kwenda kusoma. Kwa wakati huo upeo wangu katika kuhoji na kudadisi ulikuwa wa juu sana…_

_"Tulikwenda Liberia watatu, kule tulikutana na Dr Gay. Tulifundishwa somo maalum, somo hilo ni FALSAFA (philosophy) yenyewe!_

"Sisi watatu tulikwenda Liberia tukiwa tumechelewa (wengine walikwisha anza). Kwanza tulipewa questionaires — maswali mengi kila mmoja kujibu, lengo likiwa ni kutaka kujua kiwango cha uelewa cha kila mmoja kimasomo na ki — imani (na pia kuchunguza kama kuna ushawishi wa siasa za mlango wa kushoto, ukommunisti)._

_"Ninajihesabia kuwa mtu wa bahati sana kusoma somo la FALSAFA (Mkongwe Kingunge alisema), kupitia kusoma Falsafa tulisoma vitabu vingi vya wana fikra wakubwa na mawazo yao; — Marx, Lenin nk._
_"Tulijifunza sana, Waalimu wetu wamarekani wakitaka kutusawishi tuone ya kuwa mfumo wa ukomunisti si mzuri hata kidogo..!_

_"Ndio…nakili falsafa ya wanafunzi wa kuhoji wa Hegel (Young Hegelians) ya kina Karl Mark ilinivutia,_

_"Yule mmoja nani yule aliyesema…“si kuwa Mungu kamuumba binadamu kwa mfano wake ila ni kuwa binadamu kamfikiria mungu kwa mawazo yake”…hiyo ilinifanya nielewe alaa kumbe Miungu imeumbwa na mawazo ya binadamu..!_

_"Huyo Ludwig Feuerbach, nilimsoma sana, nilisoma sana kitabu chake hicho…_

_Yeye (Ludwig Feuerbach) alinifanya mimi niwe Mwana fikra huru — Freethinker_ _"Ninaheshimu imani za dini lakini mimi sipo (sijaji identify na ) yoyote…_

_"Kwa imani za asili yetu, Wamatumbi wa Kilwa kusini Tanzania wanaamini na kuomba kwa “Mungu wa chini”, na “Mungu wa juu”…_

_"Kwangu mimi hulka hii ya kudadisi na kutafuta kutaka kujua inaendelea…siyo dogma (ng’ang’anizi), na wala si dini nyingine..!_

_"Marafiki zangu “makomredi” wao ni wafuasi wa Marx…mimi ni “Marxian”, nakubaliana na kipengelele chake cha “Historical materialism” (mgongano wa nguvu za ukinzani — na za hoja pia) kama njia ya kuiangalia / kuichambua jamii.._

_"Waumini wa moja kwa moja wa falsafa ya Marx wao wanakataa uwepo wa Mungu kama vile wao wana ushaidi kwa hilo…itikadi yao inageuka kuwa _"Kuna wakati fulani Balozi wa Urusi ya zamani (USSR) alitutembelea pale chuo cha Kivukoni — Dar es salaam, badala ya kujibu kisayansi kwa kushuku (scepticism), yeye alijibu kama vile wao tayari wana ushaidi, alisema:- sisi Warusi tumekwenda kwenye sayari ya Mwezi (kupitia mwana sayansi wetu Yuri Gagarin ) na kule hakumkuta Mungu…jibu hilo lilinikasirisha kwani mimi nilikuwa ndiye ninayejulikana pale chuoni kuwa nilikuwa naishi bila imani ya dini yoyote…kweli hilo ndio jibu toshelezi..?_

_"Mimi siamini lakini sina uhakika, (Agnostic)_
_"Ndio…“Living without religion” kuishi bila dini, maadili bila dini hayo ndiyo maisha yangu_

_"mimi sina shida na hilo, mke wangu yeye ni Mkatoliki kabisaa kwa imani yake, hamna tatizo…_ _"Nilipozaliwa mimi, Kipatimu huko kilwa, wengi ni Waislamu._

_Nimekulia na kusoma Dar es salaam, Pwani, wenyeji ni Wazaramo na ni waislamu pia._

_Kwamba pengine kulikuwa na dalili za ubaguzi wowote wa kidini..? hapana_

_"Nilipokwenda Tabora sekondari (katikati ya Tanzania), kule wengi wakawa wakristo…_

"Sihitaji consolation (faraja) ya dini, kwani unafikiri watu wengi wanategemea makanisa au misikiti kwa hilo..?_
_"Sihitaji kumbadili mtu yoyote kwenye imani yake, kuishi kwangu bila dini ni msimamo wa kifalsafa_

_"Dhana ya uumbaji katika kitabu cha mwanzo (genesis) inakwendana na hadithi (myth) ya Waisraeli katika historia yao, na pengine ni sahihi kwao kwa dini yao inayokwendana na utamaduni wao
Kingunge Ngombale Mwiru
 
Duh

Hivi neno Kingunge tofauti na jina maana yake nini?
Si tafsiri rasmi, ila kwa kuwa miaka nenda miaka rudi mwenye jina hilo yaani Kingunge Mwiru alikuwa na madaraka ya juu katika chama chake na serikali, ikachukuliwa kuwa yeyote aliye na cheo sehemu fulani ni kingunge.
 
Back
Top Bottom