Waraka Mwl Shukia kwa Mwigulu Nchemba

Waraka Mwl Shukia kwa Mwigulu Nchemba

shukia

Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
46
Reaction score
53
Salaams,

Kila kukicha ni wewe na kila uchao unavuma kwa mambo ambayo hayana msingi na wala hayana mwelekeo wa kuiendeleza Iramba Magharibi. Yawezekana umesahau jukumu lako kama mbunge wetu matokeo yake unafanya kazi za CCM na serikali ndani ya Bunge. Kumbuka kuwa wewe haupo bungeni kuiwakilisha serikali, au usalama wa taifa au CCM, upo bungeni kwa niaba ya wana Iramba Magharibi. Mengi unayozungumza bungeni ni yale uliyonayo kichwani mwako na si yale ambayo wana Iramba wamekutuma.

Huna sifa za kuwa mwakilishi wa wana Iramba. Ulipoteuliwa na wana CCM kugombea ubunge wana iramba wengi walidhani wamepata mtu wa kuisogeza Iramba. Niliwaskitikia sana wana Iramba wenzangu kwa kuwa na mtazamo huo. Ni kwa sababu walikuwa hawakujui. Mie niliyepata kukufahamu japo kidogo nilisikitika sana. Nakumbuka ulipokuwa UDSM kipindi kile cha mgomo wa kushinikiza marehem Mkili atolewe magereza, kila uliposimama kutoa hoja watu walikuzomea na kukutaka ukae chini. Si kwa sababu walikuwa wankuchukua, ila kwa sababu hukuwa na uwezo wa kujenga hoja za kushawishi watu. Hilo liko wazi, watanzania walio wengi wanakuzomea kila uzungumzapo bungeni. Sidhani kama hiyo ni sifa nzuri kwa kiongozi mzuri.

Umekuwa ukihusishwa na mambo mengi ya hovyo, wahenga walisema lisemwalo lipo.... Sidhani sana kama unajitambua na unatambua uyafanyayo. Wakati mwingine huwa nafikiri huenda yale maisha yako ya kukaa porini kwa muda mrefu ukichunga ng'ombe yaliathiri ukuaji wako kiakili kiasi kwamba hujitambui, huwezi kujenga hoja zikashawishi watu, ukatumiwa na wenzako kwa kila aina ya jambo lisilojema na wewe ukalibebea bango pasipo tafakuri ya kutosha. Ama kwa hakika umekuwa limbukieni wa kila jambo. Kumbuka cheo ni dhamana, na hukuzaliwa kuwa kiongozi milele. Muda wako utakwisha watakuja wengine nao watapita. Ni vema sasa ukatumia muda huu kufanya mambo ambayo watu watakukumbuka nayo kwa wema.

Ulikuwa mchunga ng'ombe hebu kumbuka kufanya mambo ambayo yatawasaidia wale wachunga ng'ombe uliowaacha wanataabika. Think wider, achana na ulimbukeni wa kisiasa na kulewa vimadaraka ulivyo navyo. Jitambue kuwa wenzako wanakutumia, ukichujuka watakumwaga. Si unajua mwisho wa vuvuzela ni nini.

Shukia
 
Unajua kesho kukitokea machafuko Tz, akaja mwendesha mashitaka wa ICC akauliza maoni ya wananchi ni nani alichochea, nina uhakika mwigulu ataongoza kwa asilimia nyingi sana, hata kama hakuhusika...
 
Ni kweli jimbo lake ni masikini amekalia siasa za majitaka na kuwa producer wa filamu za kigaidi!kweli ametumwa na wana iramba huo upuuzi?anakuwa kama vile mbunge wa viti maalum hawana majimbo wale kila issue wanairukia na kukimbizana nayo!yeye atawaambia nini wana iramba?au ndio anategemea kutumia dola kuiba kura?
 
Huyu mtu ni hatari kuliko anavyojijua yeye. Lakini ujinga wake unakuzwa na hao waliomuweka kwa kumsifia kila kukicha. Ameenda bungeni anawaita viongozi wazito kitaifa akina Mbowe na Slaa kwamba ni magaidi na hajachukuliwa hatua hadi leo. Nasikia alipotoka nje alisifiwa sana na hao wanaojifanya wanakemea uchochezi. Ndipo anapopata kiburi.
 
Kwa vile mwalimu kataja jina lake kamili basi tusishangae kesho tukisia yu mahututi au marehemu..otherwise ni ushauri mzuri nchemba uchukue na ujichunguze.
 
Ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
ngoja tuone vijana wa 7000/= watakuja kumteteaje boss wao mpuuzi!!!!
 
Huyu hajui siasa,amechangia kuingiza nchi ktk sintofaham ya ugaidi na udini.
 
Kama hawezi kuamini anayoambiwa naomba atafakari ya Julius Malema wa Afrika Kusini. Alikuwa DAMU DAMU NA ANC Leo hadi jengo lake linauzwa kwa amri ya ANC.

Mwigulu Nchema kama una wazazi nenda kapate ushauri wao kumbuka ndiyo waliokufundisha kwenda choo!!!
 
awekewe ulinzi huyo mwalimu na ikiwezekana mwezi huu angalieni kama mshahara wake utaingia bank
 
i used to know this human being na hata picha zake akiwa amevaa ngozi na mkuki akichunga,alikwa kijana mzuri na nimesoma naye ila hadi leo sijui ana ugonjwa gani uliomdadilisha hadi kwa zuzu kiasi hichi,huwa nafikiria ccm vibaya kuwa kina kitengo cha kutengeneza watu kama yeye,he wa a sweet boy,like leadership,bright in acedemics but today just a mug
Salaams,

Kila kukicha ni wewe na kila uchao unavuma kwa mambo ambayo hayana msingi na wala hayana mwelekeo wa kuiendeleza Iramba Magharibi. Yawezekana umesahau jukumu lako kama mbunge wetu matokeo yake unafanya kazi za CCM na serikali ndani ya Bunge. Kumbuka kuwa wewe haupo bungeni kuiwakilisha serikali, au usalama wa taifa au CCM, upo bungeni kwa niaba ya wana Iramba Magharibi. Mengi unayozungumza bungeni ni yale uliyonayo kichwani mwako na si yale ambayo wana Iramba wamekutuma.

Huna sifa za kuwa mwakilishi wa wana Iramba. Ulipoteuliwa na wana CCM kugombea ubunge wana iramba wengi walidhani wamepata mtu wa kuisogeza Iramba. Niliwaskitikia sana wana Iramba wenzangu kwa kuwa na mtazamo huo. Ni kwa sababu walikuwa hawakujui. Mie niliyepata kukufahamu japo kidogo nilisikitika sana. Nakumbuka ulipokuwa UDSM kipindi kile cha mgomo wa kushinikiza marehem Mkili atolewe magereza, kila uliposimama kutoa hoja watu walikuzomea na kukutaka ukae chini. Si kwa sababu walikuwa wankuchukua, ila kwa sababu hukuwa na uwezo wa kujenga hoja za kushawishi watu. Hilo liko wazi, watanzania walio wengi wanakuzomea kila uzungumzapo bungeni. Sidhani kama hiyo ni sifa nzuri kwa kiongozi mzuri.

Umekuwa ukihusishwa na mambo mengi ya hovyo, wahenga walisema lisemwalo lipo.... Sidhani sana kama unajitambua na unatambua uyafanyayo. Wakati mwingine huwa nafikiri huenda yale maisha yako ya kukaa porini kwa muda mrefu ukichunga ng'ombe yaliathiri ukuaji wako kiakili kiasi kwamba hujitambui, huwezi kujenga hoja zikashawishi watu, ukatumiwa na wenzako kwa kila aina ya jambo lisilojema na wewe ukalibebea bango pasipo tafakuri ya kutosha. Ama kwa hakika umekuwa limbukieni wa kila jambo. Kumbuka cheo ni dhamana, na hukuzaliwa kuwa kiongozi milele. Muda wako utakwisha watakuja wengine nao watapita. Ni vema sasa ukatumia muda huu kufanya mambo ambayo watu watakukumbuka nayo kwa wema.

Ulikuwa mchunga ng'ombe hebu kumbuka kufanya mambo ambayo yatawasaidia wale wachunga ng'ombe uliowaacha wanataabika. Think wider, achana na ulimbukeni wa kisiasa na kulewa vimadaraka ulivyo navyo. Jitambue kuwa wenzako wanakutumia, ukichujuka watakumwaga. Si unajua mwisho wa vuvuzela ni nini.

Shukia
 
Hata hapo alipo jamaa huyu amefika kwa Ushirikina maana anaamini na ni muumini mzuri sana wa FREEMASON hata hilo linaweza kumpa kiburi pia lakini muda si mrefu atajuta maana Kitila alishaanza na mungu na atamaliza na mungu kwani hakuna ushirika kati ya nuru na giza
 
TISS mmalizeni mwigulu,vinginevyo itagharimu nchi baadae
 
Back
Top Bottom