Waraka Mwl Shukia kwa Mwigulu Nchemba

Waraka Mwl Shukia kwa Mwigulu Nchemba

Kuna mazingira ushauri kama huo inabidi mtu alipie lakini Nchemba anapewa bure, sasa ni kazi kwake kuufanyia kazi.
 
MIMI NAMUOMBEA KWA MUNGU AENDELEE NA TABIA YAKE YA HUJUA ILI 2015 TUWE NA IDADI YA WATU WA KUTOSHA WA KUPELEKWA MAHAKAMANI AU THE HAGUE KABISA.
ORODHA IYO WAMO
.MWIGULU
.JMK
.KINANA
.NNAPE
.MZEE MAKAMBA
.NCHIMBI
.LOWASA
.CHENGE
.ROSTAM
.MAHITA NA SAID MWEMa
 
Huyu jamaa ni kilaza kweli sijui amevimbiwa kiasi gani na huu ujangili na ufisadi wa masisiem,kwa reference akamuulize marsha pale mwanza wamemfanya nini kwa nguvu ya umma pamoja na kuwa yeye ndio alikuwa na majeshi yote..sasa hivi anazoa takataka ingawa nayo ina harufu ya ufisadi...shame on you chemba la ....
 
Unaweza kuwa na macho na usione, pia unaweza kuwa na masikio usisikie! But nakumbuka Mh. Lukuvi alisema mtu ukiwa unatajwatajwa sana manaake wewe ni mchapa kazi bila kujali unatajwa kwa lipi..Maybe hicho ndo kipimo kipya cha uchapa kazi and Mwigulu is really working on that.
 
Au wamemfanya Ndondocha ? kwa nini wanamtumia tu na yeye mwenyewe hashtuki ? Haoni kama kikinuka kitamnukia yeye mwenyewe ?
 
Hao ndio wasomi wa CCM ya leo, hupanda vyeo kwa kutukana CDM. Enzi za Mwalimu, tulikuwa na team ngangari iliyokomaa kisiasa.
 
kweli mmelalamika,lkn ktk barua ya mwl.sijaona tuhuma ama madhaifu ama makosa ya huyu mwigulu. Hebu tuwekeeni wazi makosa yake huyo.
 
shukia kumbe wewe ni wairamba. hongera kwa ujasiri na kusimamia ukweli.
 
Last edited by a moderator:
dah. mwl.umenikumbusha 2001 UDSM, ila jamaa zake wa economics walimwamini wakampa uongozi "class representative" sisi wa Bcom tukamgomea tukampa "u-course representative" kulingana na mapovu yake", kazi kwake salamu amezipata
 
Ujumbe mzuri kutoka kwa mwl makini hope atakuwa ameupata nakuufanyia kazi
 
Unajua kesho kukitokea machafuko Tz, akaja mwendesha mashitaka wa ICC akauliza maoni ya wananchi ni nani alichochea, nina uhakika mwigulu ataongoza kwa asilimia nyingi sana, hata kama hakuhusika...

Mkuu hapo rekebisha au futa kabisa.
Huyu bwana ni mhusika mkuu.Maneno yake mengi ni ya kichochozi na huhitaji kuwa Profesa kung'amua .jaribu kulinganisha na kesi ya Lema kutokana na Tukio la Cho cha Uhasibu Arusha.
Huyu bwana Chama chake ndiyo inamlinda wakidhani anawafanyia kazi nzuri lakini kwa wanaofikiri sawa sawa anafanya siasa za maji taka na hatari kwa ustawi wa Jamii.

Watu kama hawa wanafaa kushughulikiwa barabara wakati muafaka ukifika-(Kuwafikisha mbele ya Pilato)
 
Wanaomchukia mwigulu ni wale magaidi na wauwaji wanaopanga mauwaji gizani kisha wanajifanya jua likichomoza
 
Salaams,

Kila kukicha ni wewe na kila uchao unavuma kwa mambo ambayo hayana msingi na wala hayana mwelekeo wa kuiendeleza Iramba Magharibi. Yawezekana umesahau jukumu lako kama mbunge wetu matokeo yake unafanya kazi za CCM na serikali ndani ya Bunge. Kumbuka kuwa wewe haupo bungeni kuiwakilisha serikali, au usalama wa taifa au CCM, upo bungeni kwa niaba ya wana Iramba Magharibi. Mengi unayozungumza bungeni ni yale uliyonayo kichwani mwako na si yale ambayo wana Iramba wamekutuma.

Huna sifa za kuwa mwakilishi wa wana Iramba. Ulipoteuliwa na wana CCM kugombea ubunge wana iramba wengi walidhani wamepata mtu wa kuisogeza Iramba. Niliwaskitikia sana wana Iramba wenzangu kwa kuwa na mtazamo huo. Ni kwa sababu walikuwa hawakujui. Mie niliyepata kukufahamu japo kidogo nilisikitika sana. Nakumbuka ulipokuwa UDSM kipindi kile cha mgomo wa kushinikiza marehem Mkili atolewe magereza, kila uliposimama kutoa hoja watu walikuzomea na kukutaka ukae chini. Si kwa sababu walikuwa wankuchukua, ila kwa sababu hukuwa na uwezo wa kujenga hoja za kushawishi watu. Hilo liko wazi, watanzania walio wengi wanakuzomea kila uzungumzapo bungeni. Sidhani kama hiyo ni sifa nzuri kwa kiongozi mzuri.

Umekuwa ukihusishwa na mambo mengi ya hovyo, wahenga walisema lisemwalo lipo.... Sidhani sana kama unajitambua na unatambua uyafanyayo. Wakati mwingine huwa nafikiri huenda yale maisha yako ya kukaa porini kwa muda mrefu ukichunga ng'ombe yaliathiri ukuaji wako kiakili kiasi kwamba hujitambui, huwezi kujenga hoja zikashawishi watu, ukatumiwa na wenzako kwa kila aina ya jambo lisilojema na wewe ukalibebea bango pasipo tafakuri ya kutosha. Ama kwa hakika umekuwa limbukieni wa kila jambo. Kumbuka cheo ni dhamana, na hukuzaliwa kuwa kiongozi milele. Muda wako utakwisha watakuja wengine nao watapita. Ni vema sasa ukatumia muda huu kufanya mambo ambayo watu watakukumbuka nayo kwa wema.

Ulikuwa mchunga ng'ombe hebu kumbuka kufanya mambo ambayo yatawasaidia wale wachunga ng'ombe uliowaacha wanataabika. Think wider, achana na ulimbukeni wa kisiasa na kulewa vimadaraka ulivyo navyo. Jitambue kuwa wenzako wanakutumia, ukichujuka watakumwaga. Si unajua mwisho wa vuvuzela ni nini.

Shukia

mwl. shukia hakika umenena vema.
hilo jamaaa siku zote huwa ni kubwa jinga.
nawashangaa wanairamba kumchagua mtu mbwege kama huyo.
poleni kwa janga kubwa mlilonalo kwa sasa.
 
Mr mchemba that is a nice advice hope you will take it up if only you are wise

Mheshimiwa yuko wise ndio maana amejipanga na yuko tayari kwenda kutoa ushahidi wa ugaidi wa Lwakatare Hadi Mbinguni. Anataka kuvunja rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kutoa ushahidi mbinguni japo hajaeleza hakimu ni nani na mahakama za huko zinaendeshwaje na je zinakubaliana na sheria za huku duniani au laa.
 
Mwigulu ni kamanda wa kweli, lazima aisambaratishe chadema

Mimi mbona naona kinyume chake? Au wenzetu mmelala usingizi bado?
Hivi mnapopita mitaani mmevaa yale mashati yenu mnapozomewa inamaanisha nini?
Mwigulu ni virus mkuu. Mtakapokuja jitambua, Tanzania itakuwa chini ya utawala wa wananchi.
 
Kikwete anampongeza, ndugai anamsifu, kuna wabunge maccm wakiona amesimama basi ni makofi to. Naona sio yeye tu wakumlaumu bali wate wanaoshadidia kila ovu alifanyalo.
 
Huyu mwalimu kama kweli anania njema na kijiamini vema aweke bayana utambulisho wake humu jf ili tumjadili huyu ni mbumbumbu asiyejitambua ni hewa kama mahewa wegine aliyekutuma wote mko milembe day.
 
Back
Top Bottom