Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar (?)

Status
Not open for further replies.
Iko haja ya kuwatafuta wachawi hawa wanaojaribu kutuvurugia amani ya nchi kwa mambo kijinga kama haya. Watanzania wa leo sio wa kuzungumzia UDINI.
 
Iko haja ya kuwatafuta wachawi hawa wanaojaribu kutuvurugia amani ya nchi kwa mambo kijinga kama haya. Watanzania wa leo sio wa kuzungumzia UDINI.

Nakuunga mkono
Nadhani hii mada tuifunge sasa, tuzungumzie mambo mengine kwa Manufaa ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Utachukuaje taarifa usiyoijua na kuileta hapa, basi mwanzoni ungeweka angalizi kwamba hii siyo taarifa yangu, nimeitoa katika blog. Ungekuwa wa maana ungefanya utafiti japo kidogo tu kabla ya kuweka taarifa ya kipuuuzii kama hii.
Kuweka mada za kipuuziii ambazo hazijafanyiwa utafiti, mada na mwenye mada wote ni wapuuuziii, tena wakubwa.
Yatakiwa uombe msamaha kwa kosa hilo

Ndugu kujua taarifa itakusaidia nini usipoelewa kilicho andikwa kwenye hiyo taaarifa? teh teh teh kazi kweli kuelimisha watu.

Nimechukua huu waraka na kuuleta hapa ili tuone upande mwingine washilingi ni jinsi gani watu wanavyo fikiri na kufanya mambo yao.Huoni huu waraka ni wakichochezi? je hauoni kama mimi kuuleta hapa utasaidia watu kujua hali halisi inavyo kwenda ? unajua maana ya upuuzi? au unaandika tu kwa sababu umepewa vidole vya kuandikia?
 
Jamani mnisamehe maana nilijua huyu ndo mwandishi naomba anisamehe, nimepata kazi kubwa ya kufuta vyote nilivyoandika kwakutumia simu maana sikuwa karibu na computer.
Lakini huyo mchochezi tutamgundua tu kutokana na kiswahili chake maana kwenye jukwaa la dini hauto mkosa huyo mpendwa.
 
Naona waislam wachache waliouandika huu wako low sana. Inshangaza sana watu wachache wapuuzi kuandaa waraka wa kichochezi kama huu na kuuweka katika midomo ya viongozi wa kanisa. Kwa mara ya kwanza aliuweka "Mwiba", halafu ghafla ukatoweka, leo umerejea tena.

Waraka huu ungekuwa wa kanisa Kwa ufupi ungeonyesha, salamu ya kikristo na ya kumtanguliza kristo kabla ya hiyo phrase ya "Wapendwa katika bwana" ambayo waisalmu huitumia katika mihadhara kuwabeza wakristo.

Pili waraka mrefu kama huu kutotaja jina "Yesu" haiwezekani, inaonyesha jinsi jina hili linavyotisha!

Waraka umejengwa katika misingi ya wakristo kusifia kazi walizozifanya kama watu na sio kufarahia matendo makuu waliyofanyiwa na Bwana!
Makanisa yote yana muundo unaoeleweka, waraka huu haunyeshi kuwa

unafungamana na kanisa lipi. Wakristo hawajawa low kiasi hiki!

Haya ni kwa uchache tu!

Bwana Cathbert wape pole, bado safari ni ndefu!
 
Mpaka hapo nsha mjua huyu mpotoshaji na lazima nimuumbue wait a minute.......
Hilo suala si kweli mkuu, kwani kwa habari nilizozipata za uhakika ni kwamba watu wengi wenye sifa hawapendi kufanya kazi za academics maeneo kama ya mzumbe kwani mtu akiwa mtaani analipwa vizuri zaidi kuliko kuwa mzumbe, hivyo inapelekea uhaba wa wahazili. Pia tatizo lingine lipo kwenye vyuo vingi vya elimu ya juu, kwa mfano mlimani hawakuwa wanaajiri mpaka walivyoona wengi wanastaafu ndo wakaanza, sasa hili ni tatizo sugu vyuoni. Ninamengi ninayoweza kusema kuhusu vyuoni maana hari si shwari sana.
 
Ukisoma huu waraka vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho utaelewa waliouandika ni watu wa aina gani.kwa kawaida barua zilizo andikwa na watumishi waki kiristo utazijua tu hawezi kuanza na wapendwa,ili neno wapendwa wanapenda kutumia sana ndungu zangu hawa ****** kwenye mihadhara yao kukashifu wakristo.

Hakuna sehemu iliyo mtaja Yesu ni barua gani ya kikiristo isiyo mtaja Yesu? neno Yesu kwa wenzetu wanaliogopa sana ndio maana hawajaweza kulitumia au kulitamka .Dhumuni la waraka huu naona wanataka kujenga chuki na wakiristo na kususia taasisi zile ambazo zinaendeshwa na wakiristo,pia na kuwashawishi waislamu wasiwauzie wakiristo ardhi eti itatumika kujenga makanisa hivyo ukiristo utapanuka Zanzibar.hii naona ni ufinyu wauelewa Mbona waislamu wengi tu wanasoma shule za seminari na pasipo kulazimishwa kufuata imani ya kikristo ,pia wanatibiwa kwenye hospitali zinazo milikiwa na makanisa..

Kwa style hii itakuwa ngumu sana kupatikana muhafaka Zanzibar maana wanadhani muungano wetu ni kueneza ukristo huko visiwani kwao.....
 
Hilo suala si kweli mkuu, kwani kwa habari nilizozipata za uhakika ni kwamba watu wengi wenye sifa hawapendi kufanya kazi za academics maeneo kama ya mzumbe kwani mtu akiwa mtaani analipwa vizuri zaidi kuliko kuwa mzumbe, hivyo inapelekea uhaba wa wahazili. Pia tatizo lingine lipo kwenye vyuo vingi vya elimu ya juu, kwa mfano mlimani hawakuwa wanaajiri mpaka walivyoona wengi wanastaafu ndo wakaanza, sasa hili ni tatizo sugu vyuoni. Ninamengi ninayoweza kusema kuhusu vyuoni maana hari si shwari sana.
Mkuu naona unachanganya hoja hapa.Hii thread haiusiani na maswala ya Mzumbe
 
hivi ni lini watanzania tutakaa chini kwa pamoja bila kuangalia tofauti zetu za kidini/ukabila N'K tukafanya jambo la maendeleo kwenye nchi yetu na vizazi vyetu vijavyo?.Watu kutwa nzima tuna bishana juu ya dini ambazo tulizaliwa tukazikuta..Sijajua haswa kusudi la watu wanaoleta haya mambo ya udini dhumuni lao ni nini hasa? ili swala tuna liona ni dogo lakini siku zinavyo zidi kwenda mbele ilinazidi kukuwa.Itafikia wakati tutaanza kusema ili duka ni la muislamu usinunue vitu hapo, na mengineyo kama hayo.
 
Mbona yapo hayo tena ndani ya Dar, kama unapoishi hayapo mshukuru mungu! mie nimewahi kuona hii ndani ya kitongoji kimojawapo Dar,
 
Mbona yapo hayo tena ndani ya Dar, kama unapoishi hayapo mshukuru mungu! mie nimewahi kuona hii ndani ya kitongoji kimojawapo Dar,

Aisee! bado sijayaona hayo,ninapo ishi karibu maduka yote yana milikiwa na wapemba na watu wa dini ya kislamu na hakuna kitu kama hicho tunashirikana vizuri tu.Ndio maana nikapata wasi wasi uenda tukafika huko.
 
haya mambo yapo sana hasa sisi tunaoishi huku uswahilini,labda mwenzetu unaishi kwa watu waliostaarabika.
 
mwandishi wa kimakala hiki,atafaidika nini yakitokea machafuko tanzania kwa sababu za udini. Bahati nzuri ni kwamba, tulivyokuwa informed tufikiao internet, ni tofauti kabisa na hali ilivyo tanzania,miongoni mwa wananchi. wapo na hamsini zao, wala hawajali cha ufisadi au udini. tunamshukuru Mungu kwa hilo, japo kama wangeaccess internet wote sijui ingekuwaje.
 
Imekuaje upuuzi huu umerudi tena humu JF. Kwanza aliuleta jamaa anayejiita MWIBA tukaupiga madongo ukaondolewa, sana imekuaje tena. Mods, are you there?
 
Hapo sasa pasinge tosha nchi hii,sasa hivi tungekuwa tupo kama somalia,unajua ni kwa nini waraka huu umempamba moto kwa sasa? kwa sababu wakati unatolewa watu wengi kipindi icho walikuwa hawana access na internet.Kusudi la mwandishi wa waraka huu unaonekana ni anataka kuwatenganisha waislamu na wakiristo.
 
Imekuaje upuuzi huu umerudi tena humu JF. Kwanza aliuleta jamaa anayejiita MWIBA tukaupiga madongo ukaondolewa, sana imekuaje tena. Mods, are you there?

Mkuu ni kwa nini unataka kukwepe hali halisi iliyopo. Mods pls msiondoe WARAKA HUU KWANI KWA NJIA MOJA AU NYINGINE UNATUPA SOMO,NA KUTAMBUA KADHIA ILIYOKO MBELE YA JAMII YETU.
 
Watu wanaosoma gazeti hili, wana shida, mimi kwanza nikiona tu huwa nalipisha kwasababu huwa naona kama limeandikwa na osama.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom