Waraka kwa Wabunge Wote TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa Wabunge Wote TZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Radio Producer, Nov 16, 2011.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ndugu Waheshimiwa,
  Nawapa pole kwa majukumu hasa vikao vya Bunge vinavyoendelea hapo Dodoma. Nimeandika HATARI kwa sababu ni mambo ya muhimu sana nataka kuwaambieni kupitia jukwaa hili:-

  1. Amani- Neno hili sasa limeanza kutokomea mbali sana hapa Tanzania. Tanzania haina amani tena kama ilivyokuwa hapo zamani. Matukio kadhaa yanayoweza kutowesha amani hii ni haya hapa: Mauaji yanayofanywa na Polisi, Waandamanaji wanavyokamatwa na kuwekwa Lumande, Maisha magumu kwa Watanzania, Migomo na migogoro isiyoisha katika vyuo, Ukosefu wa ajira kwa zaidi ya vijana milioni 2.5.

  Kiimani machafuko haya yanatimiza maandiko matakatifu katika kitabu cha Mungu, lakini kwanini nyinyi wanasiasa ndio mnakuwa chanzo kikubwa? Mmesahau kuwa maandamano ni haki ya raia? Na yanapotokea haya mbona mmefumba macho? Katika vikao vyenu hapo Dodoma mmejaribu kukemea hata siku moja mauaji haya yanayofanywa na Polisi? Amani mnaitokomeza wenyewe, gharama yake ni kubwa ambayo inaweza kuwaumiza hadi nyinyi. Ikitokea vita nyinyi mtakimbilia wapi? na mkikimbia mtakimbia na nyuma zenu? Tuacheni kusema Chama fulani kinasababisha uvunjifu wa amani, ni chama kipi kimefanya fujo na kuwapiga wanachi hadi wakafa? Mbona mnajificha peupe jamani?

  DAIMA MTAILIPA DAMU YA WATU WASIO NA HATIA.

  Leo yatafanyika haya na mtapongeza sana mauaji hayo tena mkiwa bungeni? Angekuwa ndugu yako kapigwa na Polisi mngefurahi na kupongeza? sisi raia tunayasikiliza sana hayo mnayoyaongea bungeni, nashangaa wengine wanaongea hadi unajiuliza kweli huyu ni Mbunge katumwa na wananchi? Damu ya watu wasio na hatia mtailipa tu hata mnaoshabikia adhabu yenu ipo.

  2. Suala la Katiba- Nazidi kusikitika sana maana muda mwingi mnatumia malumbano tu hakuna mnachojadili kuhusu katiba. Wengine hatuelewi hata maana ya katiba, mngetuelewesha kwanza. Ila kwanini mara ya kwanza mliahidi kuifanyia mabadiliko na leo mmeirudisha vile vile? Mbona mnatufanya wajinga jaman sisi wananchi tuliowapa kura zetu mkatusemee na kutuletea haki zetu. Wabunge wa CCM wasikilizeni wenzenu, nadhani hao wote sio vichaa wanakitu cha maana, mkilazimisha tu yatakuja kuwatokea puani kumbukeni mna watoto, wajukuu, na hata ndugu zenu, mnadhani wao watasalimika na katiba yenye masilahi ya mafisadi?


  Nimeshindwa kuendelea kuandika maumivu moyoni yamezidi, Yaani kweli wanasiasa mmeamua kutufanyia hivi? Mali zetu mnatupora halafu mnatuua tena mnataka mtugandamize katika suala la katiba?? Damu ikimwagika itakuwa juu yenu, Kumbukeni na nyinyi ni watu tu, ipo siku mtakufa, Je, Mnaweza kuingia mbinguni (Imani)? Huu ni ujumbe wenu wabunge, ikibidi usomeni bungeni ila kumbukeni sana nyinyi pia ni wanadamu, namaliza maneno machozi yananitoka Mungu ndiye hakimu wa Kweli, ipo siku mtakumbuka!!!!
  Radio Producer.
   
 2. j

  jigoku JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mkuu umenena kweli na ni vema,hakika damu ya watanzania hawa itakuwa juu yao,mimi sina utakatifu kama malaika ila kwa haya wanayofanya wabunge wa CCM wakisaidiana na CCM-B,amini amini nawaambieni hili jambo halitapita bure,lazima kujutia damu za watanzania hawa.pamoja na shida zingine za maisha zinazosababishwa na mafisadi,hakika kwenye hili nalo mtawajibika
   
 3. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aaah umeme umekatika ulikuwa unaongea kuhusu wabunge wa CCM ABC hao hukumu yao iikaribu.
   
 4. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,278
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  1. Je Wakifa watazikwa na hizo mali zao (walizotupora kwa nguvu)?

  2. Watazikwa na vyeo vyao?

  3. Pakitokea vurumai wataendelea kutukashifu na kusifu polisi?

  4. Wataficha wapi nyuso zao siku watanzania wakiamua kuhoji?

  5. Katiba kuna nini wanachotafuta nayo? Wanamlinda nani na kwa nini?

  6. CCM kama mnajiona safi kwanini mnatumia muda mwingi kuwajadili CHADEMA kuliko mswada wenyewe?

  7. Hao wananchi mnaosema wamewatuma ni lini mara ya mwisho mmeongea nao?...

  8. Kama nyie wabunge mngekuwa wapinzani mngejisikiaje bunge kuwasengenya kwa hasira na mapovu?

  9. Kama nyie mngekuwa wananchi wa kawaida (ie. Wamachinga, wanafunzi wa vyuo, graduate jobles, raia wanabambikizwa kesi, wapigwa mabomu, wanyang'anywa nyumba, na wote wapigwa virungu), mngejisikiaje kuona pumba za wabunge wanaokula kodi zenu?

  Najua baadhi yenu mtaliona bandiko hili na kulidharau maana mnakula mema huko dodoma kwa kujadili na kukiponda chama kingine na kusahau mlichotumwa, msisahau magari yenu na posho ni kodi zetu.
  Iko siku inakuja na sio mbali sana machozi yangu yatageuka ya furaha pale tutakapoirudisha nchi yetu kwetu sis walipa kodi wenye uchungu nayo.


  Msigeuze Bunge letu kumbi ya Taarab
   
 5. M

  MyTz JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkuu hii kitu hata mi sijaielewa...
  iv mswada ulioko mezani ni wa KATIBA au WALK OUT YA CHADEMA?
  nafikiri hawajui wakifanyacho, cha msingi wanatakiwa wajitazame na wabadilike hawana jinsi...
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Tunakoelekea ipo siku mambo yatakuwa mabaya kweli, 2015 haitakuwa kama leo!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hii siyo lugha ambayo CCM wanaweza kuielewa kirahisi...Natamani nchi hii yote ingekuwa Mbeya!!!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  o
  Mkuu, umenena jambo la msingio sana.
  Lugha hii ya mazungumzo, hoja, maandamano, walk out..........hii lughahawaielewi hawa!!
  Mi nimesema na nitaendelea kusema. It is a very very painful truth!!
  Kikinuka ndo wataelewa!!

  Muswada utapita kwa makofi ya mikono na masaburi, Kikwete atapitisha itakuwa sheria, atachagua hiyo tume yeye.........Je hiyo itakuwa katiba ya nani??

  Some action is needed........
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Huwa nakumbuka sana enzi zetu za college....Hadi maprofesa walikuwa wanatupigia magoti tukisha weka silaha chini!!


  Ila naamini somo la Mbeya litakuwa limewaingia...labda kama ni sikio la kufa...!!
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Watu wakishachoka na uonevu, wakiamua sasa tunataka haki yetu.......hakuna bomu wala pingu itakayoweza kusaidia!

  Unajua,wanaona haya maandamano na jinsi wanavyoweza kuyasambaratisha wanajisikia kwamba wanaweza saaaana!!
  Wnasahau kwamba, maandamano hayo hayakuwa na nia ya kupambana na polisi, kwa hiyo ni rahisi tu kuwasambaratisha.

  Watu wakisema sasa hatumtaki mtu huyu!!! hayo mabomu watapiga mpaka watachoka!!
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni kweli ila CCM hawawezi kuyaamini haya hata kama angeyatabiri Mnajimu wao mkuu wa enzi zile Shekh Yahaya Hussein!
   
 12. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Muda na nyakati hubadilika, umaskini unaoshamiri kwa kasi utaichosha jamii ambayo mwisho wa siku itaamua liwalo ma liwe.
  Ule muda unakuja hawataamini
   
 13. S

  SIKUOGOPI Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitabu Kitakatifu Cha BIBLIA:Chuo cha Nabii ISAYA Mlango wa 33 Kifungu cha Kwanza 1: Imeandwikwa!: Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendewa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwishwa kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.

  CCM Mmetutenda kwa Hila Bungeni nanyi pia Subirini wakati wa Mungu Mkuu asiyeshindwa na jambo lolote anakwendwa nanyi kuwatenda Vivyo hivyo Mnavyotutenda Hila sisi. Maana Andiko la Mungu si Uongo hata lisitimie Kamwe!

  Katiba ni Haki yetu wananchi kwa Tamaa na Ulafi wetu Mmetunyang'anya katika Mikono yetu Mkiamini Mko salama! Kwa yote Mliyoyafanya! Nataka niwaambie kitu cha Msingi sana leo Hii.

  Mungu si Mwanadamu hata Alipinge Neno Lake! Hivyo CCM Mungu atawapiga Haijawai kutokea! Maana Anakwenda Kuandaa Meza Moja na Watesi wenu CHADEMa nanyi Mtakuwa watumwa Kwao CHADEMA nanyi Mtateswa na Kupigwa na Mabomu huku Mkiandama nanyi Hakuna atakaye wasikia Maana Bwana Wa Majeshi asema! Mimi ni Mungu nisiyeshindwa jambo lolote!

  Mfalme Daudi alitumwa na Mungu kuhesabu Israeli na Yuda tu naye kwa Kiburi cha Uzima akawa Mkaidi akahesabu Kabila zote yaani Kutoka Dani Mpaka Beer-sheba! Je wajua nini kilitokea kwa Mfamle Daudi aliye Kipenzi cha Mungu?

  Mungu akampa Mfalme Daudi adhabu Tena kwa Masharti Matatu na katika hayo achague Moja ili Liwe Adhabu kwake!:

  Sharti la kwanza: Miaka Saba ya Njaa ikujie katika Nchi yako?

  Sharti la Pili: Miezi Mitatu ukimbie mbele ya Adui zako, huku wakikufuatia

  sharti la Tatu: Siku tatu iwe Tauni katika Nchi yako?

  Nami nimemuomba Mungu Sharti la Pili Limfike Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili CHADEMA wawe Maadui zake na Chama Chake! Maana wametunyima Katika Iliyo Halali yetu na Kuiweka Kuwa Halali yao!

  Hakika Vita ya Mungu itakuwa Juu yako Kikwete na Chama Chako kwa Unafiki wa Kutupokonya Haki yetu! Na Mungu si Mwongo
  lazima atakupiga Tu!

  Haki yetu wananchi huwezi kuipeleka kwenye
  chama Chako wakati ni Haki ya Watanzania wote!
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  RADIO PRODUCER you don't have to cry anymore, futa machozi yako simama na udai haki yako. Hata maandiko yamesema JISAIDIE NAMI NITAKUSAIDIA.
   
 15. M

  Mfwalamanyambi JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  , Arusha, Iringa, Moshi na Tarime.
   
 16. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Mi naona kama hawajaweza kufikiria vyema tu. kuna mtu kama GADDAFFI KWELI HAPA? Yaliyomfika hawakuyaona? wacha waendelee kulewa. ki ukweli wao kama kweli wanaenzi amani wawe wasikivu na waondoe hang over yao wawasikilize wananch4 wanataka nini. wamekuwa na sifa kama ya iresponsible baba ambaye akisema au kutoa amri pale nyumbani mtoto au mke anaguna kwanza. mimi ningekuwa wao nisingesikiliza ushauri wa kina CHENG AU EDU kwa kuwa wenzao wameamua kuozesha samaki wote. wabunge wa ssm wanaozeshwa bila wao kujua tena kwa faida ya wenzao wanaojisafishia makanisani kila kukicha. wale wa zenji sio wajinga na msiwapuuze. wanajua watendalo hao.
   
 17. P

  Penguine JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Asante Sana Mkuu kwa Waraka huu Mzito. Kila Mwenye akili na upeo apaswa kuutafakari Waraka Wako. Ni Waraka wa Mwitongo au? Nafikiri tuite WARAKA WA MWITONGO
   
 18. n

  nyantella JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Umeandika vizuri na ujumbe utawafikia waheshimiwa wote kwa ujumla wao. Ila hapo kwenye blue napata taabu saana kwa sababu wewe mwana JF unasema huelewi maana ya katiba! a graet thinker? sasa watu wa vijijini watasemaje? tafadhali jitahidi japo ku-google upate japo ABC za katiba. goodday.
   
 19. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  si mliwapa kura wenyewe bora mi nilimpigia kura MPENDAZOE.....

   
 20. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kwa sasa wameshiba hao na wamesahau kuwa jioni watasikia njaaa tena
   
Loading...