dr. Kwanza ninaomba nichukua nafasi hii kwa namna ya pekee nikushukuru kwa namna mlivyoshirikiana na viongzi wenzako kuinua upinzani na kutufikisha hapa tulipo. Umepigana vita vya hatari bega kwa bega na wana mabadiliko hata kutoa mwelekeo wa njia tunayoiendea sasa. Kila wakati yanapotajwa mabadiliko tanzania, jinalako litatajwa.
Ninapenda nikushukuru kwa kuzungumza na watanzania ambao wengi wao ni wapenzi na wafuasi wako wakubwa mimi nikiwa miongoni mwao.
Nimekusikiliza vizuri na kukuelewa kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo nina masuala kadhaa ambayo ninaomba utusaidie kutupa maelezo kwa mtazamo wako ili tuendelee kuwa pamoja katika gurudumu la utetezi wa wanyonge uliotuthibitishia utaendelea kuwapigania bila kujali una chama ama hauna.
Kabla ya yote, ninaomba nionyeshe masikitiko yangu kwa uamuzi wako wa kuresign instantly baada ya kutofautiana na viongozi wenzako kwa sababu ninahakika tofauti zenu zilikuwa na ziko chini ya uwezo na hekima zenu za pamoja. Ninachokifahamu mimi, maamuzi yoyote yanayofanywa wakati wa hasira kali ama furaha kubwa sana, huwa hayazingatii maswala mengi ya muhimu na yenye tija kwa upana unaostahili.
Ninaomba nichukue nafasi hii kuomba ufafanuzi kwa masuala yafutayo.
1. Wakati mnapanga ujio wa lowasa, ulitaka kujua kama ni asset kama atakuja na wenzake makini viongozi wazuri na kama ni liability ikiwa atakuja na vijana wa barabarani.
Mheshimiwa, huoni kama ingelikuwa ni vizuri zaidi kumpokea bila ulazima wa kuja na idadi fulani ya watu wenye sifa kadhaa, kama vile ambavyo chadema mmekikuza kwa kumpokea mtu mmoja mmoja bila sharti la kuja na watu wengine kwa wakati huo? Kwa nini yeye lowasa mlimwekea sharti hilo ambalo kwa watu wengine halipo?
Hoja yangu nyingine, hao unaowatambua kama vijana wa mitaani, ndio watanzania ambao walistahili kuwa sehemu za kazi lakini wamewekwa barabarani kwa utawala mbovu wa ccm. Huoni kama wana haki ya kuheshimiwa na kutambuliwa uwezo wao katika suala zima la maendeleo ikiwa kutakuwa na serikali mbadala inayowajali na kwamba wana umuhimu katika kupiga kura na kuiondoa ccm madarakani ili ije serikali sahihi?
Suala la kuhitaji watendaji wazuri kutoka ccm waje na lowasa ili aqualify for membership, linanipa tabu. Dr. Wewe ni msomi mzuri na umekuwa kiongozi wa chadema kwa miaka mingi. Kama kulikuwa na knowledge gape, sikutegemea mtategemea ijazwe na watu wa lowasa kutoka ccm mahali ambako tayari umepafananisha na choo. Kwa hali yoyote, hata kama wengelikuja, hawawezi kuwa ready made kufit kwenye utaratibu na kanuni za chadema. Sasa kama ndivyo, hamkuona kabisa umuhimu wa kutengeneza watu wenu wawe kama mnavyotaka wawe kwa maslahi ya chama na taifa bila kujali wanakuja ktuoka wapi ama ni wenyeji wa mlemle chadema?
2. Umeongelea suala la demokrasia kwamba kama maamuzi ya wengi yanakuwa kinyume cha mawazo yako, unatakiwa uachie ngazi.. Ni kweli hili dr? Siyo kwamba ni kukosa uvumilivu wa kuwachukulia wengine? Kama katika vikao watu wakitofautiana kwa ajli ya demokrasia yule ambaye mawazo yake hajapitishwa anapaswa kuondoka, ni kwlei dunia ingelikuwa na amani au maendeleo? Watu wangapi wangelikuwa wanaondoka kwenye familia zao, maofisini na kila mahali kwa saa? Nilichokitegemea kwako dr. Ilikuwa ni uvumilivu wa kisiasa wa kuweza kuwachukulia wengine kwa kuamini kwamba, hata kama siku hiyo walikukatalia, siku nyingine au katika hatuanyingine wangehitaji hekima na maarifa yako.
Ninajua mchakato wa mabadiliko hauishii kwenye uchaguzi. Uchaguzi ni hatua za mwanzo sana lakini baada ya hapa kunahatua ya ujenzi wa taifa jipya ambapo ilikuwa ni nafasi yako nzuri kuongoza mabadiliko kwa kuhakikisha wanyonge uanaowatetea sasa wanakombolewa ki halisia.
Nili kutegemea kwamba wewe kama katibu mkuu wa chadema, ulitakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha chadema inapata wanachama wapya wengi bila kubagua na kuwakarabati ili makandokando wanayokuwa nayo kule wanakotoka, hayapati nafasi katika chadema. Kama ulivyosema kubeba kinyesi toka chooni na kukiweka chumbani ama sebuleni, kweli ni tatizo lakini kinyesi hicho kinaweza kuwa purified na kufaa kwa matumizi mengine ya binadamu. Kilichotakiwa ni uwezo na maarifa ya kuhakikisha kinakuwa bidhaa nyingine, inayofaa kwa matumizi badaala ya kukiacha kiendelee kuwa kero. Na hizi haiba za watu si kutoka ccm tu bali hata wasio na vyama vya siasa wanapojiunga, wanahitaji kutengenezwa.
3. Umezungumzia ufasadi wa lowasa, wakati huo huo ukihitaji aje na wenzake kutoka huko chooni. Kwenye list of shame, uliorodhesha majina ya mafisadi 11 lowasa akiwemo. Ni kwei mchakato wa richmond lowasa amekiri kuhusika lakini hakueleza in details nini kilikuwa nini. Hata hivyo amewataja viongozi wa juu yake. Nilitegemea katika suala kama hili, ni vizuri dr. Ukalisaidia taifa, kwa kuzungumzia mchakato mzima, naman ccm ilivyofanya ufisadi na kuwalinda mafisadi ambao si lowasa peke yake bali genge zima la ccm akiwemo mkuu wao kama laivyotajwa na lowasa.
Wewe mtetezi wa wanyonge, tulitegemea upaze sauti ya juu ukemee ccm na serikali yake, kushindwa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi ambao si lowasa wala richmond peke yake. Kitendo cha kuwasifia sita na mwakyembe kuongelea ufisadi bila kuonyesha kuguswa na kile alichokisema mwakyembe kwamba amekificha kwa kuogopa usalama wan chi, huoni kama umekuwa biased sana?
Tuanomba utamke report ya mwakyembe yote bila kuacha aliyoyoaficha iwekwe hadharani, na wahusika wa wizi ule wachunguzwe na watakaobainika kuwa na hatia za kimahakama wapelekwe mahakamani. Lakini pia ili uonyeshe fairness, usiache kuzungumzia ufisadi wa meremeta, kiwira, kagoda, escrow, miradi ya barabara, bomba la gas, mradi wa rea, nk. Nk. Kitendo cha kuishia richmond tu na kuyaacha haya mengine yanayotisha zaidi yaliyoendelezwa na mafisadi ya ccm, inaweza kutafsiriwa kama chuki binafsi dhidi ya lowasa. Makosa yote ya ufisadi yzungumziwe na yapewe uzito unaostahli bila upendeleo.
4. Dr. Kitendo cha kuwashambulia chadema kwa kumpokea lowasa, fisadi mmoja aliyeamua kubadilika na kufuata sera za chadema, huku ukiwalinda ccm ni kupigia kampeni ccm kwa kuwafichia makosa yao ambayo hasa ndiyo chimbuko la wewe kujibainisha kama mpigania haki za wanyonge (watu wa barabarani). Ninaomba upate muda mwingine, uzungumzie nini kilikufanya ujiunge na vyama vya upinzani, na nini sababu ya kuwa na wimbi kubwa la watu wanyonge tanzania ambao unahitaji kuendelea kuwapigania dhidi ya nani adui yao na ametoka wapi.
5. La mwisho katika orodha lakini la kwanza kwa umuhimu, ninaungana na wewe kukemea maneno ya waropokaji kwamba wataitoa ccm hata kwa mkataba na shetani kwa sababu ni maneno yanayovuta laana katika nchi. Haiti walitamka maneno kama yale wakati wanapigania uhuru na shetani amekaa kwao akiwatesa vizaz na vizazi. Hatumhitaji shetani katika ukombozi wa taifa hili. Ninafuta kauli hizi na ninaungama dhambi hii mbaya kwa niaba ya watanzania wote na vizazi vyetu, mungu atusamehee, asituhesabie uovu huu, katika jina la yesu kristo. Natamka atakayeendeleza kufufua maneno yanayompa shetani utukufu, kwa kiburi, afanye hivyo kwa gharama yake binafsi na si gharama ya watanzania.
Tulianza na mungu, tunaendelea mungu na tutamalizia na mungu ambayek sisi na vizazi vyetu tutamtumikia daima.
Vinginevyo sisi tunasonga mbele na ukombozi kama jeshi lenye nguvu na umoja. Tutapigana vita kwa kuheshimiana, kupendana na kushikamana. Wakati wote tutakapo tofautiana kim itazamo kwa kuwa ni binadamu, tutamaliza tofauti zetu kwa majadiliano bila kusalitiana na kuumizana. Atakayeonyesha kuchoka, hatutamtupa, tutamganga huku tukisonga mbele. Atakaye amua kurudi nyuma kwa sababu yoyote, tutalinda uhuru wake lakini tutaepuka madhara yake kwetu. Tumeshaamua kuiondoa ccm na kuweka utawala utakaojali watanzania badala yakusita sita huku ccm ikipanga kutumalizia.
Ninategemea utaendelea kuwa upande wa ukombozi wakati wote tunapopigana vita na wakati tutakapokuwa tukianza kujenga tanzanai mpya chini ya katiba mpya ya wananchi na mifumo mipya kwa maslahi ya tanzania ya sasa ni vizazi vijavyo.