- Thread starter
- #21
Katika biblia kuna Mtu Mmoja aliitwa sauli, ambae ndio Mtume Paulo
Alikuwa muuaji na akiwatesa sana Wakristo, siku moja akakutana na Mungu akamwambia mbona unawatesa watu wangu, akambadili jina palepale akamwambia Tangu leo wewe ni Paulo, Uutangaze Ukristo
Tangu siku iyo huyu jamaa akabadilishwa ndio alitangaza ukristo haijawai tokea. Katika biblia ana vitabu Zaidi vitano kaandika. wagalatia, waefeso, wafilipi, watesalonike, wakolosai. nk nk
Muuaji aliekuja kuwa shujaa wa Ukristo.
Nakifananisha kisa hiki na story za kumuita Edward Lowasa fisadi, Sawa, yawezekana ni kweli, kama Paulo alivokuwa Muuaji, lakini Mungu amemuita Lowasa, asiwe tena Sauli Mtesaji na Muuaji bali (Paulo Mueneza ukristo).
Mungu hutumia wadhambi maana hajawai zaliwa malaika.
Lowasa, umetumwa na Mungu kutupeleka kaanani, TUTAFIKA.
Musa hakuiona kaanani lakn waisrael walirudi Nyumbani na walifika. Lowasa ameletwa kuturudisha Nyumbani. Tutafika.
Na haturud Misri.
Mkuu Dumelang; umesema sahihi. Maumivu yetu tunayougulia sisi na watoto wetu tuliyopewa na ccm tunayajua sisi. Tunasonga mbele hadi ukombozi umepatikana.
Ccm adui yetu na mtesi wetu anajitahidi kutuchonganisha, kutugawa na kutukatisha tamaa kwa kushadadia hotuba ya Dr. slaa wakidhani watanzanai ni majuha hawatatumia akili kuchambua punje na mchanga.
Hata hivyo imekula kwao na aibu inabaki kuwa yao milele. Wapiganaji wamepata mori wa ajabu na sasa wanakwenda kwa speed ya mwanga, kuizika ccm.
Uharamia wa ccm haujatuvunja mioyo bali umetuongezea nguvu. Tumetambua kweli ccm ni mumiani aliyekusudia kuliua taifa na kufuta kizazi chetu katika uso wa dunia. Sasa kazi ni moja tu. Kuikomboa Tanzania kutoka kwa mafisadi wakoloni wa ndani ccm.
Watanzania wamepania kuwaonyesha ccm kwamba wao si mapumbavu au wa barabarani kama wanavyowaita.
Kwa mara nyingine dunia inakwenda kushuhudia Tanzania yenye neema Ikiongozwa na Lowasa chini ya UKAWa.