Waporaji wa bodaboda 'Vishandu' wampeleka IGP Sirro ghafla Vituo vya Stakishari, Kawe, Tabata

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro, mapema leo amefanya ukaguzi wa ghafla kwenye Kituo vya Polisi cha Stakishari, Tabata na Kawe jijini Dar es Salaam.

IGP Sirro amebaini changamoto ya uhalifu wa uporaji kwa kutumia pikipiki pamoja na makosa ya uvunjaji.

“Nimekuwa nikipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu kituo cha Stakishari, Tabata Reli na Kituo cha Kawa, nikaamua kufanya ukaguzi wa dharura, nimebaini kuna matukio ya vijana kutumia pikipiki kupora, hawa vijana ambao jina la mtaani wanaitwa Vishandu.

“Vishandu wameongezeka, mtu kashika mkoba wake, dereva bodaboda anatokea kwa nyuma anakwapua, nimeelekeza oparesheni za nguvu zipafanyike ili kuhakikisha matukio kama haya yanapungua

“Pia kuna matukio mengine madogomadogo ikiwemo uvunjaji wa usiku, nimeelekeza oparesheni za nguvu kufanyika kuhakikisha matukio haya yanapungua kwa kiasi kikubwa, vikundi vya ulinzi shirikishi vitasaidia matukio kama hayo.

“Sisi askari pekee hatutoshi, ni lazima tushirikiane tuone uharifu unapungua lakini kimsingi tuko vizuri sana, matukio yanaendelea kupungua, wananchi watupe ushirikiano,” anasema Sirro.



FMwCfqSWQAQ0hVs.jpg


FMwCgs_WQAAML4o.jpg
 
Kwa kushindwa kupeleleza na kukamata waliomshambulia Lissu mchana kweupe,huku ana nyenzo na mamlaka zote,yeye mwenyewe hana tofauti na hao wahalifu.
 
Naye ni mhalifu tu
Lazima kuna mahali kwenye sheria zetu panasomeka kuwa "Mtu yeyote mwenye mamlaka aliyopewa chini ya sheria,akashindwa kutekeleza mamlaka yake pasipo na sababu ya msingi,mtu huyo atahesabika kuwa anatenda kosa...." Visingizio anavyotoaga Siro kwenye vyombo vya habari juu ya kushindwa kuwakamata waliomshambulia Lissu ni vya kitoto mno na vinakera.Tukiacha siasa ,Lissu ni raia kamili mwenye haki za kikatiba kama Siro,lakini kwa sababu tunamuangalia kwa miwani ya siasa,basi haki zake zinakanyagwa
 
Back
Top Bottom