IGP Simon Sirro umeshindwa kabisa kukomesha Rushwa Vituo vya Polisi

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,727
2,000
Amani iwe nanyi

Hii hali kwamba ndugu yako akituhumiwa kwa uharifu wowote kisha kukamatwa kwenye mchakato wa dhamani inaleta tabu sana kwa wananchi wanyonge na walalahoi kwamba ndugu yako kutoka ni mpaka utoe RUSHWA yaani ile kuingia bure kutoka hela bado inaendelea mpaka kipindi hiki cha Magufuli.

Tunaomba mamlaka husika komesheni hii hali kama mtuhumiwa anastaili bail basi apewe Mara moja na sio kumlaza ndani mpaka mpewe hela ndio mumtoe.

Mwezi wa kwanza ndugu yangu alikamatwa kwa kupigana na kujeruhi dhamana ilikuwa issue kubwa mpaka nilipo amua kutoa RUSHWA ndio ikakubaliwa ( kituo cha Polisi Msimbazi ).

Kituo cha polisi Msimbazi Dar es salaam na vituo Vyote vya Polisi embu badilikeni bana mnatia kinyaa sana.

CC

Waziri Simbachawene

IGP Simon Sirro

Kamanda Mambosasa.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,033
2,000
Hulka ya kupenda kuomba na kupokea rushwa ni tabia binafsi ya mtu na sio msimamo wa jeshi la Polisi kama taasisi.

NB: Mimi sio mtumishi wa JWTZ bali ni raia mwema wa kawaida tu.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,690
2,000
Hao na rushwa sawa samaki na maji.

Kwenye hili la kushamiri rushwa awamu ya tano wamefaulu sana. Hapo hujaangazia zile za kubrashia viatu!

Mitano mingine!
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,358
2,000
KUINGIA BURE KUTOKA HELA.

Wameambiwa wachukue 5000 kwa kila gari ya ku-brashi viatu, na anayekupanga goli la kuchukua hiyo 5000 lazma jioni umpatie kama 300,000/- ya shukran kila siku.
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,885
2,000
Hulka ya kupenda kuomba na kupokea rushwa ni tabia binafsi ya mtu na sio msimamo wa jeshi la Polisi kama taasisi.

NB: Mimi sio mtumishi wa JWTZ bali ni raia mwema wa kawaida tu.
Polisi wengi hawana common sense kwa sababu raia wengi hawajui haki zao. Pia kuna kulindana hata kama polisi kakosea. Kuna siku mi polisi alinikuta sina fire ext. kwenye gari bahati mbaya siku hiyo kidude cha kuonesha expiry kilifyatuka, nikamueleza nitanunua nikifika mwisho wa safari ila aliniambia anaenda kuniweka ndani, bahati nzuri akatoea afande ninafahamiana naye akamuuliza then baadaye akaambiwa aniache, so polisi wengi common sense ni rushwa rushwa
 

Emiir

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
23,879
2,000
Man Mvua Umeongea point ya msingi sana kwa siku ya leo!
Hili swala linahitaji ufafanuzi maana imeshakuwa kama ndio sheria ambayo haijapitisha tu kuwa rasmi lakini imeshaanza utekelezwaji wake.
"Kuingia bure kutoka kwa pesa"
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,727
2,000
Suala la Rushwa limeshashindikana mkuu.

Kumbuka hii kitu 'If u can't beat them,join them',Itakusaidia sana na maisha yako yatakua laiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiini kama unanawa vile.
Jeshi la polisi linalaza watu ndani kwa tamaa za kijinga sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom